Tamu chungu
Member
- Dec 20, 2015
- 85
- 64
Tangu nimalize elimu yangu ya chuo kikuu sijawahi kupata kuajiriwa na kampuni yoyote ile ya kunilipa walau hata 300k kwa mwezi ile niweze hata kusukuma maisha walau hata kwa kujibana.Naishia tu kupata vitempo vya mikataba ya mwezi mmoja au miwili ambavyo havinisaidii chochote zaidi tu ya kupoteza muda.
Napata uchungu sana ninapoona siku zinakwenda na sina chochote cha kufanya.Mwaka 2012 mwezi september nakumbuka nilifanya usaili na kampuni moja nisingepata kuitaja hadharani ambapo baada ya kufanya usaili nilipigiwa simu baada ya siku mbili kwamba nimefaulu usahili hivyo niende na vitu ambavyo wamenitajia.Nilifanya hivyo lakini chakushangaza baada ya kufika pale nikaambiwa kwamba zile nafasi wamezi cancel kwahiyo nisubiri nyumbani mpaka nitakapopigiwa simu.Nilisuburi mwishowe mpaka nikakata tamaa.
Baada ya hapo niliamua kujiunga hata na kampuni ya ulinzi ili tu nipate senti walau za kujikim na kufanya application.Nilijiunga na kampuni moja kubwa tu yenye makao yake kinondoni lakini nilifanya kwa muda kama wa miezi sita kisha nikaacha baada ya kuona mshahara wote unaishia kwenye daladala mana mpaka nifike kazini lazima nipande gari tatu kwenda tatu kurudi hapo bado sijanywa chai wala kupata chakula cha mchana.
Mwaka jana vilevile nilifanya usahili kampuni mbili ambapo mojawapo nilikua na uhakika kabisa kwamba nitaitwa kazini kulingana na jinsi nilivyojibu maswali.Daaaaaah nilisubiri na kusubiri lakini wapi mpaka ninavyoandika muda huu sijapata wala sms yao.
Niko kwenye hali ngumu na sijui hatma yangu itakuaje,kuna wakati mpaka najiuliza hivi nina mkosi gani mimi hapa duniani bila kupata majibu.Imefikia wakati mpaka ndugu zangu wananishauri niende kwa waganga wa kienyeji lakini mimi nimekua nikipinga vikali huo ushauri wao nikiamini kwenda kwa mganga ni kutokuamini uwepo wa mwenyezi Mungu kwa imani yangu mimi.
Kwa yeyote anaeweza kunisaidia walau hata connection ya kibarua ani PM nitashukuru na Mungu atamzidishia.