Sijui Nifanyaje

Sijui Nifanyaje

yaani nyie wote hamjitambua mnataka nn?
Tuambie unmpenda nani kati ya hao?
..na ushauri wa bure ni kuwa bora utengeze na uliyezaa nae,ht mtt atapata mapenzi ya wazazi, hii bness ya mtt akienda kwa mama kuna baba wa kambo, akienda kwa baba kuna mama wa kambo sio nzuri jamani,mnawatesa watt kisaikolojia


Eti mtoto wa kambo pande zote!!!!!

Kambo camp!!???
 
Wana MMU, niko katikati na sijui cha kufanya.
Sio mzuri sana wa kuelezea lakini nitajitahidi ili mpate picha halisi ya ilivyokuwa na ilivyo sasa.
Nilimpata msichana amabaye baada ya muda mfupi sana wa kufahamiana tukaanza kukaa kinyumba, bila mimi kuufahamu undani wake na yeye kuhufahamu undani wangu..

Mapenzi motomoto mara ujauzito nao ukagonga hodi. Hapoo ndipo mambo yakaanza.
Nikawaeleza wazazi wangu na kutafuta kujua yupi ni wa wapi. Ikaja kugundurika kwamba kuna maunganiko kati ya familia yetu na ya kwao ina mahusiano, mmoja wa familia yetu ameoa upande wao.


Ikajadiriwa na pande zote kila moja kivyake. Kwao walikuwa hawana shidaingawa ni baada ya msuguano mkubwa. Ila upande wangu waligoma kabisa na vitisho vya radhi na maneno makali mengineyo nikapewa na wazazi. Kwa sisi ambao tangu utoto haujawahi kusikia maneno kama hayo yakitoka kwa mzazi. Nikingiwa na hofu kubwa kiasi kwamba nikaangukia kwenye chochote watachoamua wazazi Sawa muda ukaenda mtoto mzuri akazariwa na akapata nguvu baada ya miezi michache ikabidi kwa uchungu mkubwa nimruhusu mama na mtoto wangu waende mbali na mimi.

kwa upande wa mama watoto ilikuwa ngumu sana na kwa kweli alinilaumu sana kwa kuachia hii hali itokee lakini sikuwa na jinsi.

Miaka ikapita, namuahudumia mtoto na nakwenda kumuona, kila mazingira ya mtoto anapoishi kwa kweli, leo kaishi kwa huyu leo kaishi kule na tofauti ninayoiona ukilinganisha na angekaa na mimi mwenyewe na mama yake ilikuwa hainiridhishi kabisa. Na kibaya zaidi mwanangu ananipenda kupitiliza. kila ninapoonana naye kwa kweli ikifikia wakati wa kumuaga unaona kabisa furaha inapotea usoni pake. kwa hiyo naiodoka sijarishika na na hiyo hali inazidi

Baada kama miaka mitatu, ukilinganisha umri unaenda na nimeshachoka kukaa mwenyewe, nikaanza mahusiano na mtu ambaye Moyo wangu unaniambia atakaa na mwanangu na atampenda kama ninavyokaa naye mimi. Baada ya kuona mambo yanakoelekea nikaanza kujaribu kumwomba mama watoto msamaha ili kama akiniridhia niachane na huku niliko nimrudishe yeye na tujenge familia yetu.

Baada ya majaribio kadhaa za kumshawishi mama mtoto turudi pamoja, ikashindikana. Nikaona imeshindikana ikabidi niendelee. Hatua niliyochukua ni kumwambia kwamba basi kama imeshindikana kabisa basi itabidi nimwambie kwamba niendelee na yeye aendelee, kila mtu awe huru na akipata mtu amtaharifu mwenzake. sijapata pingamizi hapo.

nikaanza process za upande wa pili, lakini kabala sijaendendelea na ni baada ya muda kupita nikamtaarifu kwamba nimepata mtu kwa hiyo nitaendelea naye.. kwa siku hiyo kama alipanic flani hivi na baadaye akaniambia nakutakia kila la kheri katika maisha yako.
mimi nikaanza na process, tukapeleka barua na tunataka kwenda chukua majibu. mama watoto kaja juu na ananiambia sawa unaendelea lakini mimi sijaridhika kabisa..

nikamuuliza sasa mbona nilikuwa nakwambia kila hatua ambayo naishukua. akaniambia hata kama sikuwa vizuri kwa hiyo sikuwa ninajua ninachokujibu .. sawa endelea lakini moyo unaniuma sana.

wadau ni mkasa mref nimewachosha lakini ... . tusimuangalie mama watoto ambaye ameshindwa kunipa Go head mara ya kwanza na kunipa nguvi ya kwenda kulianzisha kwetu... tumuangalie mtoto... naamini kabisa mtoto anatakiwa kuwa na baba na mama yake. nitamchukua sawa , lakini kunakuwa na complications sana kwa watoto ambao baba ameoa mke mwingine wakai mama yake yupo na hajaolewa.

Kingine ni kwamba hatua huku zimefika kusiko, tunatakiwa tukachukue majibu na mambo mengine yaendelee.
Niko katikati. wadau kuna makosa mengi hapo nimeyafanya lakini its too late now tuangalie jambo la msingi. na kingine ninataka nitengeneze familia yenye furaha na amani na bila kumuumiza mtu.

Akhsanteni

Huu ni utoto and don't play with our mind. wewe ni sitaki nataka ( according to ur thread inaonyesha ni miongoni mwa wanaume zaifu)
 
Scenario yake ni tofauti wao walishatongozana na mtoto wakazaa kabisa

halafu tangu jana nilikwambia tukikubali haraka mnasema tunajirahisi,

tukichelewa eti tunaringa hamna jema nyie!!!!!!!!!!
Nami nilikwambia tangu jana kuwa hata ukubali haraka, au uchelewechelewe, kwangu hakuna tofauti.... Kwa sababu yule aliyechelewa, nikimuuliza kwa nini alichelewa, huwa hanipi sababu za msingi
 
Nami nilikwambia tangu jana kuwa hata ukubali haraka, au uchelewechelewe, kwangu hakuna tofauti.... Kwa sababu yule aliyechelewa, nikimuuliza kwa nini alichelewa, huwa hanipi sababu za msingi

Si alikuwa anafikiria Ombi lako!!!!!
 
Pole sana ndugu! sijajua undugu uliopo kati ya familia yako na ya huyo mwanamke hadi ikapelekea kuanza kuishi kinyumba bila kujuana, au labda ulijua undugu wenu ila unajaribu kutuficha, mimi siamini kuwa unaweza kuishi karibu na ndugu zako ambao wazazi wako wanawafahamu harafu wewe usiwafahamu. ila kwa sababu maji yameshamwagika nakushauri ujaribu kuongea vizuri na wazazi wako kama watakataa jaribu kutafuta msaada kwa wazee wanaoheshimiana na wazazi wako uombe wakusaidie.
 
Back
Top Bottom