Jospina
JF-Expert Member
- Apr 19, 2013
- 2,421
- 1,395
Sijui ni kisomo au utandawazi siku hizi watu tumekuwa wavivu sana wa kazi za mikono. Mtu anaona bora atoe hela afanyiwe kazi ndogo kama kupiga rangi viatu kuliko kufanya mwenyewe. Mimi nilifundishwa kupiga rangi viatu vya shule na baba, siku hizi hata viatu vya watoto vinapelekwaa kwa shoe shiner. Huwezi kukuta mtu anaosha gari lake nyumbani hata kama maji yanatoka na anaeneo la kuoshea, kupalilia bustani ya maua ambayo ni kazi ya maraa moja kwa wiki hadi kutafuta mtu wa hela, kubadili balbu, kitasa au kuzibua sinki la jikoni hadi fundi atafutwe. Yani miili yetu imebakia kufanya kazi kwenye komputer na kuangalia tv. Yani hata tu kufunga kamba ya kuanikia nguo unamuita kijana wa kijiweni afunge umamlipa, unakuta wababa hawana kazi za kufanya nyumbani sababu zote wanawalipa watu wafanye. Ujue mkeo anapenda na anatamani kukuona ukifanya hili na lile hapo nyumbani, na sio kila kitu unatafuta kijana afanye. Kwa taarifa ni ndoto ya kila mwanamke kupata mume anayeweza kufix vitu nyumbani kwa mikono yake na sio kwa hela. Tafakari, chukua hatua