falcon mombasa
JF-Expert Member
- Mar 5, 2015
- 9,186
- 9,287
Wakuu habari,
Moja kwa moja niende kwenye hoja. Mimi nikiwa kama mmoja wa wamiliki wa vyombo vinavyobeba abiria hapa nilikuwa na maswali kadhaa najiuliza.
Kwanza ieleweke sipo kwa lengo la kusifia chama fulani bali nitazungumza hali halisi
wakati wa mgomo uliopita nadhani miaka miwili nyuma mimi nilikuwa pale Ubungo, kwakweli makonda wakati ule alikuwa bado Mkuu wa Wilaya lakini kiukweli alishindwa kuuzima ule mgogoro na muda wote alikuja na kundi la askari (nasisitiza sisemi kwa mapenzi ya kisiasa) muda na siku zote za mgomo madereva walioandamana walikuwa na morale ya kujibizana na makonda kwa njia isiyosahihi ya ubabe na ugomvi.
Siku ya mwisho Mbowe alikuja Ubungo kwanza akazuiliwa na askari asiingie eneo la kituo lakini baadae aliruhusiwa akakutana na uongozi wa kituo. Baada ya dakika kadhaa Makonda akaja tena akamkuta Mbowe anaongea na madereva, lakini Makonda alipotokea taharuki ikarudi upya huku madereva wenye jazba wakitaka kumpiga.
Lakini Mbowe kwa ushawishi wake alifanikiwa kuwatuliza na mgomo ukaisha. Sasa ninachojiuliza hapa ni vipi Makonda atamudu kuondoa mgomo huu unaoanza siku ya jumanne akiwa kama Mkuu wa Mkoa ambaye ameandamwa na kashfa nyingi.