Sijashiriki kurekodi mkanda wa video unaomwonesha ndg Lwakatare

Status
Not open for further replies.
sampuli ka hii ndiyo eti ipewe uwaziri 2015, aisee Tanzania imekuwa kichwa cha kujivunzia kunyoa. sorry to say that ila yamenifika. mtu hujijui hata position yako katika jamii na upo ndani ya chama gani, je kina sifa gani katika taifa letu, pandikizi kuu la siasa za chuki nchini.
 
kwa nini huyo kiongozi ampe mwigiru mkanda wa video ya mauaji na si kwenye vyombo vya dola kwa nini? na je walipeana katika kazingira yapi? hawa wawili watakuwa na information nyingi sana juu ya hili jambo, mwigiru ni mtu muhimu sana inaonekana anajua mambo mengi mno.

Ndio, polisi wamtafute mtu wa pili waunganishwe kutoa ushahidi mahakamani.
 
Duh, hayo ndio mawazo yako!

Ndg wana JF sijashiriki kurekodi mkanda wa video unaomwonesha kiongoz mwandamizi wa CHADEMA akipanga mauaji ya mhariri wa gazeti. Mambo yako dhahiri kwani video inaonesha pale ni nyumbani kwak. Pili sikumtuma mtu akarekodi mkanda huo. Niliwahi kusema nina mkanda haina maana kuwa nilituma mtu.

Mikanda niliyokuwa nayo nilipewa na kiongozi wa CHADEMA anayechukizwa na vitendo hivyo vya kinyama. Ndugu zangu wa CHADEMA, najuanawakera na hampendi kusikia haya nawashauri msihangaikie habari ya Mwigulu ameshiriki bali hangaikieni kwanini kiongozi mwandamizi anafanya hayo pia kwanini anafanya kizembe mpaka mkanda unanaswa na tatu mjiulize. Kwangu mimi sioni kama kupata mkanda huo kwa kupewa au kwa hela ni dhambi kubwa kuliko ya kupanga mauaji.

Niwambie tu mkanda niliopewa sikuweka hata nukta na nilikabidhi vyombo vya usalama.
 
Ukitaka kujua ujinga wa mtu amini ujinga wake..........Waswahili walisema "Hakuna marefu yasiyo na ncha" Kama USSR ilifikia ukomo sembuse Dola nyingine...Ushauri ni viongozi wakubali nature kutake place.
 
Mwigulu Nchemba you are such a
A%20S-devil1.gif
 
Watanzania tukiwa wazalendo na mawazo huru hatutakumbatia ugaidi....tungehoji yale yanayozungumzwa kwenye video ie content badala ya kuhoji aliyesaidia kupatikana video

Hayo tulishayadili na yote ni upuuzi na uongo usiomithilika. Mlaumu Mwigulu anayejiumbua na kujiacha utupu mbele ya GTs.
Ashukuriwe Mungu, muumba wa mbingu na nchi aliyemfunua mdomo Mwigulu na kuanza kuyabwabwaja haya maneno kuanzia kwenye vituo vya TV, mikutano ya hadhara hadi humu jamii forums. Amini amini nakuambia siku yaja ya majuto na kusaga meno kwa Mwigulu na wote anaoshirikiana nao katika udhalimu huu.
 
Ndg wana JF sijashiriki kurekodi mkanda wa video unaomwonesha kiongoz mwandamizi wa CHADEMA akipanga mauaji ya mhariri wa gazeti. Mambo yako dhahiri kwani video inaonesha pale ni nyumbani kwak. Pili sikumtuma mtu akarekodi mkanda huo. Niliwahi kusema nina mkanda haina maana kuwa nilituma mtu.

Mikanda niliyokuwa nayo nilipewa na kiongozi wa CHADEMA anayechukizwa na vitendo hivyo vya kinyama. Ndugu zangu wa CHADEMA, najuanawakera na hampendi kusikia haya nawashauri msihangaikie habari ya Mwigulu ameshiriki bali hangaikieni kwanini kiongozi mwandamizi anafanya hayo pia kwanini anafanya kizembe mpaka mkanda unanaswa na tatu mjiulize. Kwangu mimi sioni kama kupata mkanda huo kwa kupewa au kwa hela ni dhambi kubwa kuliko ya kupanga mauaji.

Niwambie tu mkanda niliopewa sikuweka hata nukta na nilikabidhi vyombo vya usalama.

Kwanini wakupe wewe?usalamavwa taifa hawpo? kwa matendo yako huaminiki umaarufu haupatikani kwa nguvu ww unatumia nguvu kuupata hapo ndo tatizo lilipo. pia tutajie huyo kiongozi
 
kwahiyo kuna mikanda mingine zaidi ya huu? na kwanini usimtaje huyo kiongozi ili sisi watanzania tukaamini hiyo mipango kuwa ni ya kweli? ndugu mwiguli siasa si kuchafuana na kuharibiana, siasa ni sera zako ndo uuze kwa wananchi, maana mmehamia kwenye mauaji, baada ya kufeli udini na ukabila. ila tu kumbuka juu ya story ya DAUDI NA GOLIATI. mungu akisimama upande wetu hakuna tutakalolishindwa watanzania.

Kileo mikanda ni zaidi ya huo ndio. Nikuhakikishie jambo moja hapo sijamchafua mtu. Wenye kweli mioyoni mwao watajua nani mwenye kosa, ALIYEKUWA AKIPANGA MAUAJI AU ALIYEREKODI AU ALIYETOA HADHARANI. MIMI SINA SABABU YA KUFOJI KITU CHA AINA ILE. KINIONGEZEE NINI, NILIPATA KAZI BOT BILA KUSINGIZIA MTU, NILIPATA UBUNGE BILA KUSINGIZIA MTU, NILITEULIWA KWENYE CHAMA BILA KUSINGIZIA MTU, LEO NISINGIZIE ILI NIPATE NINI. KUNA MKANDA WA VIDEO UNAELEZA WAZI NA KARATASI ILIYOKUWA IKIANDIKWA NA MHUSIKA YENYE HAND WRITTING YAKE NA FINGERPRINT YAKE. HATUNA HAJA YA KULAUMIANA KILA MMOJA NAFSI YAKE IMWELEZE KILICHO SAHIHI KWAKE KATI YA KUFURAHIA MAUAJI KISA KAMANDA WA CHAMA NA KUMCHUKIA ALIONESHA UOVU HUU NA KUUITA NI PROPAGANDA ZA CHAMA. MY POSITION NAHITAJI MTU MMOJA TU AAMINI KUWA HILI HALIJAONGEZEWA HATA NUKTA WENGINE WOTE AMININI NI FILAMU TU
 
Mkuu unambeba mwigulu...
Kaweka hiki kiuzi hapa ili achote hoja za CDM azitafutie uongo kabla hajaenda mahakamani. Sasa haya uliyouliza hapa tayari keshampa mtu assigniment ayatafutie majibu. Tumpotezee hadi akakutane nayo kizimbani...

Mkuu bora unisaidie maana nasoma koments za Machadema menzangu yananiboa sana sababu yamekuwa yanakurupuka sana jamani si mtafakari advise mnazopewa? Tunaingizwa mkenge yaani naatamani niwatukane lakini ndo ndugu zangu tena
 
Napendekeza huyu ifikapo 2015 huyu Lameck afanyiwe kama Eliakim Simpasa aliyekuwa mbunge wa Mbozi,huyu kwa kuihujumu CDM akiwa m/kiti wa kamati ya bunge,Mbowe alimwapia kuwa hatarudi bungeni kwa namna yoyote,kwa mbinu nyingi CDM ilishiriki kuhakikisha hatapitishwa kuwa mgombea wa ccm,ndicho kilichotokea ingawa jimbo lilienda CCM!
 
Huyu Mwigulu ndio anajiita mchumi nambari moja? basi kama ni kweli anadhalilisha wachumi makini wa Tanzania. Halahala Mwigulu usije sema akaunti yako imechezewa na kuandikwa kilichoandikwa hapa maana ni u-ha-r-o mtupu. Saa ingine kukaa kimya nako ni busara
 
Watu hawa vichwa ngumu sana,ningependa waje mabwana zao FBI wathibitishe ili wakate mzizi wafitna, hawa jamaa wanachama na washabiki wao wanamahaba kupita kiasi kama wafuasi wa Kibwetere,jeshi la polisi hawaliamini kabsaa na wakibahatika kuchukuwa dola watafukuza Polisi wote.wameshaanza kulegea.
 
Kileo mikanda ni zaidi ya huo ndio. Nikuhakikishie jambo moja hapo sijamchafua mtu. Wenye kweli mioyoni mwao watajua nani mwenye kosa, ALIYEKUWA AKIPANGA MAUAJI AU ALIYEREKODI AU ALIYETOA HADHARANI. MIMI SINA SABABU YA KUFOJI KITU CHA AINA ILE. KINIONGEZEE NINI, NILIPATA KAZI BOT BILA KUSINGIZIA MTU, NILIPATA UBUNGE BILA KUSINGIZIA MTU, NILITEULIWA KWENYE CHAMA BILA KUSINGIZIA MTU, LEO NISINGIZIE ILI NIPATE NINI. KUNA MKANDA WA VIDEO UNAELEZA WAZI NA KARATASI ILIYOKUWA IKIANDIKWA NA MHUSIKA YENYE HAND WRITTING YAKE NA FINGERPRINT YAKE. HATUNA HAJA YA KULAUMIANA KILA MMOJA NAFSI YAKE IMWELEZE KILICHO SAHIHI KWAKE KATI YA KUFURAHIA MAUAJI KISA KAMANDA WA CHAMA NA KUMCHUKIA ALIONESHA UOVU HUU NA KUUITA NI PROPAGANDA ZA CHAMA. MY POSITION NAHITAJI MTU MMOJA TU AAMINI KUWA HILI HALIJAONGEZEWA HATA NUKTA WENGINE WOTE AMININI NI FILAMU TU

Well said mwigulu, tomaso na asubiri kupapasa
 
Wewe unachojaribu kufanya ni kupindisha kinachojadiliwa humu JF, Mwigullu kasema kilichofanyika. Tazama Tanzania Daima walivyopotosha kwenye ukurasa wa mbele kabisa, ni tofauti kabisa na walichokiandika, na kwa mtu muelewa katika gazeti lile anapaswa kushika tu yale maneno waliyo BOLD kuwa aliukabidhi kama ulivyo Polisi na si vinginevyo.
CHADEMA muache kulalalmika, siamini kabisa kuwa Watanzania wamefikia hatua ya kuamini kuwa ninyi ni watakatifu kiasi hicho hadi wafikie kudharau video ya wazi kabisa inayodhihirisha kuwa LWAKATARE kahusika na video ile, badala yake jitafakarini ninyi wenyewe, inawezekana kabisa miongoni mwenu kuna wenye nia njema, lakini pia sijui ni kwa nini mnashindwa kutafakari kwa kina na kujiuliza kama kuna wasaliti miongoni mwenu na ambao hawawatakii mema watanzania

ushabiki kwenye mambo ya msingi si mzuri. Hapo ulipo bold, km aliupeleka police moja kwa moja, ccm, mnataka kudai kuwa police ndiyo waliouweka mtandaoni?? Itafika sehemu hata hao policcm wataacha kuwasaidia kwa propaganda zenu za kipuuz.
 
siamini kwamba hukushiriki. Watu watakao vuruga amani TZ Mwigulu ni no.1 cause unasiasa za chuki na visasi
kabla ya kuja watu ka hawa sijui ccm imewatoa wapi? tulishuhudia siasa nzuri, nguvu za hoja zilitawala na kutaniana -- sasa hivi ni kutishana, kufanyiana mbinu za kimafia nk - hawa jamaa wanataka kupeleka wapi nchi yetu? tukivurugana 2015 huyu ndiyo kwa kwanza kupelekwa uholanzi kujibu mashtaka. Siasa gani hizi mnatuletea katika nchi yetu, mara muingize udini, sasa mmekuja na kutunga ugaidi hamuogopi hata nguvu za mwenyezi mungu, mtu unakuwa na roho ngumu bila huruma kwa ajiri ya madaraka tu?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom