Ukweli kuhusu Lwakatare: HUENDA WAKAPATA DHAMANA LEO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli kuhusu Lwakatare: HUENDA WAKAPATA DHAMANA LEO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 20, 2013.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2013
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145


  • HUENDA WAKAPATA DHAMANA LEO

  na Mwandishi wetu

  WAKATI Mkurugenzi wa Usalama na Ulinzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilfred Lwakatare akifikishwa kizimbani kwa makosa ya ugaidi, mjadala kuhusu video inayodaiwa kumwonyesha akipanga njama za kumdhuru Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communication Ltd, Dennis Msacky umeshika kasi na kuacha maswali mengi, Tanzania Daima Jumatano limebaini.


  Mjadala huo umeshika kasi hasa ndani ya wanachama wa CHADEMA ambao wanaamini si jambo la kupuuzia kwani lina matokeo makubwa sana kwa siasa, demokrasia, usalama, intelijensia na dhamira ya wanamageuzi kutaka mabadiliko ya watawala.

  Baadhi ya maswali hayo ni pamoja na nani alimrekodi Lwakatare? Swali hili ni muhimu kwa maana ya kwamba kama siyo vyombo vya usalama (undercover) huyu aliyemrekodi ni nani?


  Je, mtu huyo alikuwa na mamlaka ya kumrekodi? Je, katika kuingilia mawasiliano ya mtu hajavunja haki za kikatiba? Kama mtu yeyote anaweza kutumia ushahidi wa video aliyerekodi mwenyewe bila kupewa mamlaka na polisi au vyombo vya upelelezi je, inawezekana watu wakamtega rais, waziri mkuu au kiongozi wa umma kwa kipimo hicho hicho na polisi watatoa uzito ule ule?


  Je, ushahidi ulitunzwaje tangu uchukuliwe Desemba mwaka jana? Swali na changamoto kubwa ni kwamba video hiyo na nyaraka nyingine hazikuchezewa?


  Kama ushahidi umekusanywa na raia tu na akakaa nao kwa miezi mitatu (tangu Desemba hadi Machi) swali linapaswa kuuliza je, mkanda huo umekuwa salama muda huo wote? Nani mwingine aliyeuona na kuupitia?

  Kama ambavyo video hiyo inavyoonekana imetolewa kwenye mtandao wa Youtube, swali kabla ya video hiyo kusambazwa, ilikuwa wapi na kwa nani?

  Kwa wale wanaojua mambo ya audio/visual technology, siyo kazi kubwa sana kubadilisha kitu chochote ambacho kiko kwenye mfumo wa kidijitali. Kuanzia sauti, picha na hata mazingira yanaweza kubadilishwa vizuri tu kwa kutumia kompyuta.


  Pamoja na ushahidi huu, ni jukumu la vyombo vya usalama kuhakikisha vinakusanya ushahidi mwingine ili kuupa nguvu ushahidi walionao.


  Hii ndiyo sababu ya vyombo vya usalama kwenda kupekua nyumbani kwa Lwakatare na baadaye katika ofisi za CHADEMA.


  Wadadisi wa duru za siasa nchini wanasema kuwa endapo ushahidi wa video hii iliyorekodiwa na kurushwa kwenye mtandao utakubaliwa na mahakama, mlango mpya wa vita dhidi ya ufisadi utakuwa umefunguliwa.


  Wananchi mahali popote walipo wataweza kutumia simu na nyenzo zao mbalimbali kuwarekodi wahalifu wa kila njama za rushwa au wakipokea rushwa na kurusha taarifa hizo kwenye mitandao bila kujulikana, na polisi watatakiwa kufanyia kazi bila kulazimika kujua nani amerekodi au kama katika kurekodi taarifa zimebadilishwa kwa namna fulani.


  Mmoja wa wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema kuwa ukiiangalia video hiyo, utabaini kuwa kipande kinachoonesha sehemu ya mpango au mkakati wa kufanya hivyo ni kweli na kipande cha pili kinaonesha kwamba video hiyo ni feki na imetengenezwa kwa ufundi wa hali ya juu kuweza kufanya ionekane njama ikipangwa.


  “Katika hilo la kwanza inaonekana ndio msimamo wa polisi, Lwakatare amekamatwa, kusachiwa nyumbani kwake na kulala rumande kuendelea na mahojiano na hatua nyingine.


  “Inaonekana polisi wanaamini kuwa video hiyo ni kweli inaonesha njama za aina hiyo na ndiyo maana wamechukua hatua. Na ni kutokana na hili bila ya shaka ndiyo maana wamemfikisa mahakamani,” alisema mhadhiri huyo.


  Alisema hata kama video hiyo ni ya kweli na haijachakachuliwa, haitoshi bado kuwa ushahidi wa mpango uovu wowote hasa kama sehemu yake ya mwanzo (ilikoanzia) na mwisho wake (ilikoishia) havipo.


  “Kwa kutegemea kipande cha katikati tu bado video hiyo inakosa muktadha wa kueleweka. Ni muhimu kwa polisi kuhakikisha wanapata sehemu ya mwanzo na ya mwisho ya video hiyo ili kuweza kuelewa. Hili wanaweza kupata kutoka kwa huyo aliyenao huo mkanda au aliyechukua video.

  Wanaweza kumuomba awapatie mkanda mzima na ninaamini mawakili wa Lwakatare nao watadai waone mkanda mzima siyo sehemu tu kama ilivyooneshwa,” alisema.


  Kama si kweli

  Kama sakata zima la Lwakatare sio la kweli, basi wanachama na mashabiki wa CHADEMA wanapaswa kuendelea na harakati za mabadiliko kwani bila shaka kuelekea 2015 yanaweza kuibuka mambo mengi makubwa.

  Kama suala zima la Lwakatare si kweli, polisi bado wana jukumu la kuhakikisha wanamtafuta na kumpata mtu aliyetengeneza mkanda huo na kumtia mbaroni kwani anafanya uchochezi kama wanavyomtuhumu Lwakatare.


  Tena mtu huyo anaweza kufanya uchochezi wa hatari zaidi kwa namna yake kwani amejaribu kuwaaminisha wananchi kuwa chama kizima cha kisiasa kinahusika na matukio ya utekaji nyara kama mtu kasoma maelezo ya huyo aliyeiweka kwenye mtandao video hiyo, kwani hakuishia kumtuhumu Lwakatare tu bali CHADEMA kama chama na viongozi wake wakuu.


  Hata hivyo, jukumu la kuthibitisha ukweli wa video hiyo kama inaweza kukubaliwa kuwa ni ushahidi liko mikononi mwa polisi.


  Haitoshi tu kusema Lwakatare ameonekana akisema hili au lile; ni jukumu la polisi kuonesha kuwa ushahidi huo umepatikana kwa njia halali na ambao haukuharibiwa kwa namna yoyote ile.


  Kama sio kweli na mahakama ikashindwa kuwatia hatiani wahusika, basi uongozi wa polisi nao utatakiwa uwajibike kwa kuboronga uchunguzi huu na zaidi ya hapo itabidi ihakikishe kuwa wahusika waliotengeneza video hiyo (kama imechakachuliwa) nao wanakutana na mkono wa sheria vile vile.


  Na hata kama itaonekana ni kweli Lwakatare alisema anayodaiwa kusema, ni jukumu la polisi kuonesha kuwa alikuwa amevunja sheria.


  Kama ni kweli

  Kama ni kweli Lwakatare amehusika na mkanda ni wake, basi Jeshi la Polisi halina jinsi isipokuwa kufuata mwanzo wa hilo sakata hadi mwisho wake kuwakamata wahusika wote yaani Lwakatare, yule aliyekuwa anahojiana naye, na wale ambao walikuwa wameamua kuufadhili mpango huo.

  Endapo utakuwepo ushahidi wowote wenye kuonesha kuhusika ama moja kwa moja au kwa namna moja wamehusika, basi CHADEMA inapaswa ijichunguze yenyewe.


  Kama Lwakatare alikuwa anapanga hayo akiwa anatekeleza amri au agizo kutoka kwa kiongozi yeyote wa chama basi kiongozi huyo akitajwa na ikithibitika mahakamani kuhusika kwake atapaswa kujiuzulu mara moja.


  Kama video itaonekana kweli imechakachuliwa basi vyombo vya usalama vitatakiwa kutumia ari na nguvu ile ile waliyoitumia kwa Lwakatare kuitumia dhidi ya wahusika wa video hii kwani kuwaachilia, kuwapuuzia ni kukaribisha watu wengine kuanza kutengeneza makorokocho ya aina hii.


  Lwakatare na Ludovick Joseph ambao walikamatwa katika tarehe tofauti mapema mwezi huu wanatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ya ugaidi.


  Katika shitaka la kwanza, watuhumiwa hao wanadaiwa kula njama kwa nia ya kumdhuru Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky kwa sumu, kinyume na kifungu cha 227 cha sheria ya kanuni ya adhabu.


  Katika shtaka la pili wanadaiwa kwa pamoja kula njama za kutaka kumteka Msacky na katika shitaka la tatu wanadaiwa kufanya mkutano wa vitendo vya kigaidi.
  Katika shtaka la nne linalomkabili Lwakatare peke yake ni la kuwezesha kutendeka kwa kosa la ugaidi kinyume na kifungu cha 23 (a) cha kuzuia ugaidi nyumbani kwake.


  Washitakiwa hao ambao wako mahabusu, huenda wakapewa dhamana leo wakati mahakama itakapokuwa ikitoa uamuzi wa kupewa dhamana au la.


   
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2013
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,373
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  kosa kubwa la polisi ni kuweka politics mbele ya kazi ambayo inahitaji utahalamu wa ki ulinzi, kitu cha kwanza wamekifanya cha mwisho kisa politics au presha kutoka kwa wanasiasa especially nchimbi. kitu cha kwanza polisi walitakiwa kukifanya ni kuakiki clip hiyo(authenticity) ili kupata picha kamili ya tukio zima ikiwemo kupata mazungumzo
  yote yakiwemo yaliyo editiwa sasa unapeleka so called evidence ambayo ni vipande vipande je vile vipande vingine
  viko wapi ambavyo kwa namna vinaweza kubadilisha picha nzima ya tukio. Polisi watajiaribia sana kwy tukio na huenda
  wakaumbuka vibaya sana kwa kukubali kutumiwa na wanasiasa.
   
 3. Open-Minded

  Open-Minded JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2013
  Joined: Mar 17, 2013
  Messages: 278
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tusubiri mahakama ifanye kazi yake
   
 4. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2013
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  hii movie imeivua gwagulo jeshi la polisi...hivi wameshindwa hata kuangalia ile nyimbo ya bush na tony?...kazi kwelikweli...
   
 5. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2013
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,563
  Likes Received: 917
  Trophy Points: 280
  :nono::nono: ....................................
   
 6. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2013
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,500
  Likes Received: 3,978
  Trophy Points: 280
  Mahakama za Tanzania ni huru;team ya utetezi wa Lwakatare ni wazoefu sana na wamewahi shinda kesi nyingi ngumu lkn watapata wakati mgumu kutoka kwa wakili wa serikali Prudence Rweyongeza;namfahamu kijana huyu anajua anachokifanya!Kwa haraka naona akina Lissu walikosea waliposhindwa kumpa reference hakimu kuwa kwa nn Lwakatare ashtakiwe kwa kosa zito lisilo na dhamana la ugaidi kwa kuhisiwa tu kuwa 'alitaka kutenda kosa'ili hali aliyekamatwa akihiswa 'tayari katenda kosa' kumteka na kumjeruhi Dr Ulimboka alishtakiwa kwa kosa jepesi!
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2013
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145

  Mbona toka kifo cha MWANGOSI polisi wamekuwa wanatumiwa na Wanasiasa wa CHAMA TAWALA? Hii sio DEMOCRACY VYOMBO VYA DOLA kuwa UPANDE wa SERIKALI TAWALA...
   
 8. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2013
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,593
  Likes Received: 488
  Trophy Points: 180
  Hivi ile sheria ya kukataza kuzungumzia kesi zilizoko mahakamani imefutwa au Tanzania Daima kwa mara nyingine linatafuta sababu ya kuchukuliwa hatua ili waseme wameonewa?

  Hili gazeti sasa halina weledi hata chembe. nadharia za nini wakati kesi inaendelea?
   
 9. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2013
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,497
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Gaidi hana dhamana. Lwakatare na Ludovick wakipata dhamana basi na viongozi wa uamsho kule Zanzibar wapewe dhamana.
   
 10. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #10
  Mar 20, 2013
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,332
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 145
  Tanzania Daima bana,
  We have no choice, hivi ndivyo vyombo vyetu vya habari Tanzania.

  Kwanza kuichambua kesi iko mahakani ni kukaribisha PREJUDICE AND DEFAMATION, pili kuwafundisha polisi nini cha kufanya ili kesi ifanikiwe wakati tayari ikiwa mahakani ni kutowatendea haki waendesha mashitaka,watuhumiwa na wananchi.

  Kwa kusoma katika mistari, inaonyesha gazeti liko upande gani. Journalism ethics zinataka mwandishi kupata habari ambayo iko balanced kwa maana kwamba, kama wanataka kupata mawazo/maoni kuhusu tukio lenye utata (Disputable) lazima wapate kutoka pande mbili ili kumuwezesha msomaji kujenga picha positive and fair.
  Hata huyo anayetoa maoni hataki hata kutajwa jina lake (Why) kama yeye ni mtaalamu, anaogopa nini jina lake kuandikwa?. is it a fictitious interview? AKILI MKICHWA
  Cha kushangaza ni pale gazeti linatoa amri kwa polisi. Ni hili hili gazeti linakuwa mstari wa mbele kulalamika kama polisi inafanya kazi kwa maelekezo ya wanasiasa. Halafu lenyewe linakuja na AMRI kwa polisi
  Haliishii kwenye kuamlisha polisi tu, linaenda mbali zaidi na kujipa madaraka ndani ya CHADEMA kwa kuelekeza ni cha kufanya kwa mtuhumiwa/watumiwa wakati CHADEMA ina taratibu, imani na sheria (Ethics) za kukabiliana na maswala kama haya.
  Kwa ujumla, Tanzania Daima katika article hii, limekuwa lenyewe ndiye mtazamo wa watu, judge, wanasheria na CHADEMA kwa lengo mahsusi la kuwaosha watuhumiwa.

  Yetu ni macho na masikio.
   
 11. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #11
  Mar 20, 2013
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 8,695
  Likes Received: 8,419
  Trophy Points: 280
  Kinchosumbua hapa kimeundwa kacoalition kati ya Polisi, TISS na CCM na wao kujiapiza kuwa watafanya njia yoyote kuhakikisha CDM haiingii 2015 ikiwa hivi ilivyo sasa.

  Wananchi sasa ndiyo tunapaswa kutafakari hizi kauli za mara kwa mara zilzokuwa zinatolewa na Wassira kuwa lazima CDM itakufa kabla ya 2015, je haina uhusiano na hili sakata lililoshupaliwa kwa nguvu zote na Polisi kuhusu huo mkanda unaodaiwa kurekodiwa na Lwakatare?!

  Kama kweli Polisi hawashupalii kesi kwa maelekezo ya CCM, ni sababu zipi zinazofanya mtu kama Ulimboka ambaye alitekwa na kuteswa sana karibuni mwaka sasa, waliofanya tendo hilo hadi leo hawajakamatwa, lakini hili tukio la kufikirika la Lwakatare limepelekwa kwa speed ya kifastjet??!!

  Kwa kweli kwenye hii kesi ya Lwakatare ndiyo tutaupima uhuru wa mhimili wa mahakama, kama nao utayumba na kutaka kutimiza matakwa ya watawala basi ni dhahiri Taifa linaelekea kwa
   
 12. Msolopagazi

  Msolopagazi JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2013
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 659
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Sipati picha hii movie itaishia wapi
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2013
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,091
  Likes Received: 2,775
  Trophy Points: 280
  Walichondika ndivyo ambavyo tumekuwa tukizungumza hapa JF kwenye jukwa hili.
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2013
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 164,958
  Likes Received: 444,596
  Trophy Points: 280
  Tatizo la mwandishi wa hii makala hakugusia uwezekano wa ya kuwa hii kideo huenda ni kweli na madhara yake ni nini? Nionavyo kideo ni kweli na Lwakatare atujuze kupitia mahakamani malengo yake yalikuwa ni nini? Sioni hata chepe ya kuwa mkanda umeghushiwa hapo sauti yake tunaifahamu na kukohoa kwake tunakujua vizuri sana....................sasa kughushiwa kupo wapi na tunasikia hata maandiko yake yamenaswa sasa kwanini polisi wasipekuwe ofisini kwake na nyumbani kwake kuona kama kuna ushahidi mwingine wa kumuunganisha kwenye hili sakata?

  Sioni siasa hapa ila mtuhumiwa wa ugaidi ambaye anahitaji kujitetea alikuwa na malengo yapi katika kufuatilia nyendo za mwenzake na huku akikusudia kumlisha sumu au dawa za usingizi?
   
 15. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2013
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,508
  Likes Received: 798
  Trophy Points: 280
  Leo umetoa angalizo la muhimu sana hii sio siasa. Viongozi wako wa CDM wangefikiri kama wewe leo stori ingebaki ya Lwakatare na kesi yake wala sio chama na kesi ya ugaidi.
   
 16. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2013
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,500
  Likes Received: 3,978
  Trophy Points: 280
  Mahakama ya Kisutu leo itakachosema ni kuwa"haina uwezo wa kusikiliza kesi za ugaidi";watasisitiza kuwa ni "Mahakama kuu tu yenye uwezo huo na leo kesi itatajwa tu"!Lwakatare atarejeshwa mahabusu!Akiwa mahabusu atapangiwa jaji na siku ya kuanza kusikilzwa kesi yake Mahakama Kuu ambapo ndipo sheria zitakapo anza kupekuliwa vilivyo!Nina imani kubwa na Prof Safari na team yake!
   
 17. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2013
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 17,049
  Likes Received: 4,458
  Trophy Points: 280
  Litokee lolote lile, polisi wana kazi kubwa...
   
 18. Baraka Sawema

  Baraka Sawema Senior Member

  #18
  Mar 20, 2013
  Joined: Dec 18, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hicho ndo mlikuwa mnataka kukamata watu, kuwafunga alafu kudai tunaingilia uhuru wa mahakama. Hata hivyo waandishi wanayo haki ya kuripoti habari za mahakama.
  Na kimsingi sheria za nchi yetu imepitwa na wakati angalia kenya tv zinaruhusiwa kuonyesha mambo yote yanayoendelea mahakani hata wakitaka kufanya hivyo live.
   
 19. UPIU

  UPIU JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2013
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 602
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Gazeti limeamua kutohoji lwakatare alimpa nani sumu ya kwenda kumzuru mwandishi?
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2013
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,177
  Likes Received: 877
  Trophy Points: 280
  Rutashubanyuma hunaunacho kijua zaidi ya kujaza uhalo tu hapa.. Unataka wanajf waamini hakuna mtu anaweza kuingiza sauti ya lwakatare, unataka kuaminisha watu kuwa video hiyo haikuchezewa, je unaelewa nini tunaposema kuchezewa..kama kichwa chako kina akili nenda kapitie upya videohiyo na urudi urudi huku ukishirikisha ubongo wako na siyo tumbo lako...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...