Sijaona wanahabari Tanzania..

Aaron

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
3,019
4,693
Wana jukwaa,

Wanahabari ni watu muhimu sana kwa maendeleo ya taifa lolote kiuchumi..kisiasa hata kiutamaduni ndio wanayoimulika jamii na kutoa taarifa zitakazo wafanya wananchi wailewe vizuri jamii yao hata matukio mbalimbali.

Hapa Tanzania wanahabari siwaoni...kila ukifungua tv,radio hara magezeti maneno na taarifa ni zilezile,mara rais kasema hivi,waziri mkuu vile au wazili katembelea eneo fulani,chadema wamesema hivi kupitia kwa msemaji wao au Nape kasema vile kuhusu inshu fulani ya CCM.

Hizi taarifa hata mimi nisiye na taaluma naweza kuziripoti kama zilivyotolewa na wasemaji.

Kazi ya mwanahabari ni zaidi ya hapo,hapa tunahitaji taarifa za kiuchunguz yaani mwandishi anaenda field mwenyewe na kuibua taarifa ambazo chanzo chake ni yeye mwenyewe.Taifa letu lina matatizo lukuki ambayo wanahabari inabidi waingie mtaani bila kusubiri kuitwa.

Kidogo nalipongeza mwanaharisi na Mawio japo nao habari zao sana sana ni za kisiasa zaidi ila kidogo wanajitahidi kufanya uchunguzi bila kutegemea kupewa taarifa na wahusika ambazo zingekuwa zimechakachuliwa tayari.

Nawaona bbc aljazera na mashirika mengine ya kimataifa hata vyombo vya habari vya Kenya siku hizi vinajitahidi.

Wanahabari wa tz simameni sasa japo ni gharama kwa habari za uchunguzi.Chombo kinaweza kujiwekea utaratibu hata kuwaandaa wanahabari baadhi katika chombo chao na kuwa wanatafuta habari hizi.

aaron.chillo97@gmail.com
 
Last edited by a moderator:
Wana jukwaa.
Wanahabari ni watu muhimu sana kwa maendeleo ya taifa lolote kiuchumi..kisiasa hata kiutamaduni..ndio wanayoimulika jamii na kutoa taarifa zitakazo wafanya wananchi wailewe vizuri jamii yao hata matukio mbalimbali..
Hapa Tanzania wanahabari siwaoni...kila ukifungua tv,radio hara magezeti maneno na taarifa ni zilezile...mara rais kasema hivi..waziri mkuu vile au wazili katembelea eneo fulani....chadema wamesema hivi kupitia kwa msemaji wao...au Nape kasema vile kuhusu inshu fulani ya ccm...
Hizi taarifa hata mimi nisiye na taaluma naweza kuziripoti kama zilivyotolewa na wasemaji..
Kazi ya mwanahabari ni zaidi ya hapo..hapa tunahitaji taarifa za kiuchunguzi...yaani mwandishi anaenda field mwenyewe na kuibua taarifa ambazo chanzo chake ni yeye mwenyewe.... taifa letu lina matatizo lukuki ambayo wanahabari inabidi waingie mtaani bila kusubiri kuitwa..
Kidogo nalipongeza mwanaharisi na Mawio japo nao habari zao sana sana ni za kisiasa zaidi ila kidogo wanajitahidi kufanya uchunguzi bila kutegemea kupewa taarifa na wahusika ambazo zingekuwa zimechakachuliwa tayari... nawaona bbc aljazera na mashirika mengine ya kimataifa..hata vyombo vya habari vya kenya siku hizi vinajitahidi.....
Wanahabari wa tz simameni sasa japo ni gharama kwa habari za uchunguzi..chombo kinaweza kujiwekea utaratibu hata kuwaandaa wanahabari baadhi katika chombo chao na kuwa wanatafuta habari hizi...
Ndugu yangu tatizo dio kwamba wanahabari hawapo nchini,tatizo ni wamiliki wa vyombo vya habari ambao ndio wanaoamua kipi kiandikwe na kipi kisiandikwe.Habari za kiuchunguzi zinataka fedha sasa hawa wamiliki hawatoi fedha kwa waandishi wao sasa habari za aina hii zitatoka wapi? Hakuna chombo cha habari huru nchini kwetu,tunajidanganya kuwa tunahitaji uhuru wa habari kutoka serikalini,je wanajua kuwa wamiliki pia hawatoi uhuru kwa waandishi wa habari?
 
Habari za kiuchunguzi zina zengwe nyingi..Zinahitaji mtu mwenye uthubutu kuweza kufanya..Kitu ambacho wengi hawana
 
Wana jukwaa.
Wanahabari ni watu muhimu sana kwa maendeleo ya taifa lolote kiuchumi..kisiasa hata kiutamaduni..ndio wanayoimulika jamii na kutoa taarifa zitakazo wafanya wananchi wailewe vizuri jamii yao hata matukio mbalimbali..
Hapa Tanzania wanahabari siwaoni...kila ukifungua tv,radio hara magezeti maneno na taarifa ni zilezile...mara rais kasema hivi..waziri mkuu vile au wazili katembelea eneo fulani....chadema wamesema hivi kupitia kwa msemaji wao...au Nape kasema vile kuhusu inshu fulani ya ccm...
Hizi taarifa hata mimi nisiye na taaluma naweza kuziripoti kama zilivyotolewa na wasemaji..
Kazi ya mwanahabari ni zaidi ya hapo..hapa tunahitaji taarifa za kiuchunguzi...yaani mwandishi anaenda field mwenyewe na kuibua taarifa ambazo chanzo chake ni yeye mwenyewe.... taifa letu lina matatizo lukuki ambayo wanahabari inabidi waingie mtaani bila kusubiri kuitwa..
Kidogo nalipongeza mwanaharisi na Mawio japo nao habari zao sana sana ni za kisiasa zaidi ila kidogo wanajitahidi kufanya uchunguzi bila kutegemea kupewa taarifa na wahusika ambazo zingekuwa zimechakachuliwa tayari... nawaona bbc aljazera na mashirika mengine ya kimataifa..hata vyombo vya habari vya kenya siku hizi vinajitahidi.....
Wanahabari wa tz simameni sasa japo ni gharama kwa habari za uchunguzi..chombo kinaweza kujiwekea utaratibu hata kuwaandaa wanahabari baadhi katika chombo chao na kuwa wanatafuta habari hizi...
Kuna waandishi ni kiboko. Muandishi ninaemkubali ni Suzane Mungi wa TBC(kwa sasa), na BBC(Kabla ya kurudi Tanzania na Tido D Mhando).

Huyu atakumbukwa kwa uhodari wake akiwa BBC,alishiriki jangwani huko Iraq akiandikia BBC kwenye vita kati ya US na Washirika wake dhid ya Marehemu Saddam Husein. Huyu dada/mama alionyesha uhodari wa hali ya juu, japo mazingira yalikua hatarishi. Kama kuna mtu ana video clip ambayo siku moja ilirushwa na BBC kama sikosei, utakuja kuyaamini maneno yangu! Watanzania hawa hawa wakiwa nchi za watu wanadeliver sana. Lakini mtu ata awe mahiri vp, akirudi nyumbani kutokana na mifumo mibovu wanaishia kudharauliwa. Yuko wapi Tido Mhando, yuko wapi Mzee Omari Nundu,yuko wapi Prof Tibaijuka mtu ambae UN anaheshimika sana.

Mtangazaji mwingine ni yuke wa Kenya KTN-Mohammed Ally.! Huyu kila mmoja kwa habari zake za Uchunguzi, nadhan atakua ndiye namba moja Afrika Mashariki na ya Kati yote!
 
wanategemea press conferences, kumtafuta msemaji wa taasisi flani,tangazo kutoka taaasisi flani,makongamano nk.... kupitia hivi vyanzo huwezi pata details za kutosha. Habari za kiuchunguzi hazipo tz . inaonekana wanaendeshwa kwa ushabiki na Sera za vyombo labda zinawabana..
 
Wapuuzi tu wengi, juzi nikaona star tv habari ya kuwapo malaya wanafunzi na wapenzi wa jinsia moja, aliposema tuungane na mwanahabari wetu akili yangu niliiset kuona watu wakiojiwa hata kwakuficha sura zao kama wafanyavyo BBC, PRESS TV, ALJAZEERA wakieleza kuhusika nk nk.

Ajabu na kweli nilishangaa kuona tu eti ulikuwa mdahalo wakichambua utafiti uliofanyika na kutoa takwimu. Shame on them.

Sasa kweli kuchunguza habari kama hii pia ni hatari? Inahtaji kujihami?
 
Tanzania chini ya CCM siyo nchi ya kujivunia na usitegemee kamwe tutapata wanahabari mahiri chini ya hiki chama cha kinafiq mafedhuli na kenge. Angalia hata wanahabari na vyombo vya habar vilivyominywa wakati wa uchaguzi. Hata jipu ambaye huyo huyo eti mtumbua jipu alipozomewa walificha ila wajanja tulaipata humu jf.

JF nayo iliminywa wakati wa matokeo ya uchaguzi wakaja eti navisingizio eti cyber attacks sijui hackers wakati wajanja tulishajua waliminywa na mafisi ila tuliwaelewa na kuwasamehe
 
Tanzania chini ya CCM siyo nchi ya kujivunia na usitegemee kamwe tutapata wanahabari mahiri chini ya hiki chama cha kinafiq mafedhuli na kenge. Angalia hata wanahabari na vyombo vya habar vilivyominywa wakati wa uchaguzi. Hata jipu ambaye huyo mtumbua jipu alipozomewa walificha ila wajanja tulaipata humu jf.

JF nayo iliminywa wakati wa matokeo ya uchaguzi wakaja eti navisingizio eti cyber attacks sijui hackers wakati wajanja tulishajua waliminywa na mafisi ila tuliwaelewa na kuwasamehe
Ulishawah kuandaliwa muswada juu ya tathinia ya habari Tanzania kuwa waandishi wa habari wawe na degree ulijua nini kilitokea? Muulize Kubenea anajua
 
Back
Top Bottom