Sijaona Tamko lolote toka Nchi za Kiarabu kulaani tukio la Kigaidi la Brussels!

bazoka

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
300
141
Heri ya Pasaka kwenu wapendwa wa jamiiforum ni matumaini yangu mpo salama kabisa!

Kuna jambo leo nahitaji kupata uelewa zaidi toka kwenu maana sometimes naweza kuwa sipo sahihi ila kwa majibu na maoni yenu naweza kupata mwangaza sahihi!

Wiki iliyopita yametokea matukio mawili ya ulipuaji wa mabomu katika mji wa Brussels huko Ubelgiji lakini cha kushangaza sijaona popote pale Mataifa ya Kiarabu yakikemea kilichotokea Brussels as if hawajasikia chochote!

Lakini swali la kujiuliza mbona akiuwawa Mpalestina mmoja pale Gaza basi Mataifa yote ya Kiarabu yakilaani kwa Kiwango kikubwa na Mataifa mengine kama Iran yakitishia kuishambulia Israel kwa makombora ya Nyuklia!

Lakini pia tumeona hata madhila wanayofanyiwa Wapalestina na Waisrael Marekani na Mataifa ya Ulaya yamekuwa mstari wa mbele kukemea mambo hayo lakini Waarabu wao wenzao wakifanya Ugaidi wanaona ni kama kawaida sana na hao magaidi hawafai kulaumiwa wala kukemewa!

Naomba kuwasilisha!
 
Mtoa posti jaribu kutafuta maarifa ya kutosha kwa kile unachotaka kupost, Iran hana nuke, lakini Syria anapambana na hao magaidi ambao Marekani anawaita wapigania uhuru, anawapa silaha, fedha, mafunzo kwa kushirikiana na ukoo wa Saud.
 
Twendeni na hoja sio kelele zisizo na msingi maana kuna watu washahisi haya mandiko yangu yana mlengo wa kidini!
 
Mtoa posti jaribu kutafuta maarifa ya kutosha kwa kile unachotaka kupost, Iran hana nuke, lakini Syria anapambana na hao magaidi ambao Marekani anawaita wapigania uhuru, anawapa silaha, fedha, mafunzo kwa kushirikiana na ukoo wa Saud.
Juda pale Syria anachofanya Marekani ni kuwadhibiti Isis wasizidi kujipachulia maeneo kumbuka Syria na Uturuki ni majirani na Uturuki ni sehemu ya Ulaya na pia mwanachama wa NATO kama ilivyo Marekani lazima wahakikishe ISIS wanamalizwa!
 
Mtoa Mada nadhani si mtazamaji au mtafuta Habari so anakurupuka tu nchi kibao zimelaani Wairan japo si waarabu ila kumbo moja na Muslim ndio wa kwanza kulaani hii kitu.... kuliko hata Marekani..
 
Unafki hapo upo wapi?niambie lini na wapi washawahi kutoa tamko?wewe tatizo ushaingiza upepo wa kidini hapo!
mbona walilaani tena masaa machache baada ya tukio?,
hadi assad,iran,dubai,saudi wote wamelaani.

Ila mbona uturuki mataifa mengi hayakuulaani na hushangai?

Pia fuatilia kule pakstani leo wamelipua kwenye shughuli za pasaka ,napo pia wataalani wala usihofu
 
Matamko mbona mengi sana, nimerudi kutoka dubai juzi, nilikuwa huko wiki nzima, TV zao na magazeti yao yote yamelaani HUO uharamia, na zaidi ya hivyo wamewafunga wananchi Wao wengi wanaojulikana kujihusisha na mafundisho kama hayo. Hakuna anayefurahiya mauuaji ya wanadamu au ukatili kama HUO. Hawa wachenzi hawana dini na ni majangili wakumalizwa bila huruma
 
mbona walilaani tena masaa machache baada ya tukio?,
hadi assad,iran,dubai,saudi wote wamelaani.

Ila mbona uturuki mataifa mengi hayakuulaani na hushangai?

Pia fuatilia kule pakstani leo wamelipua kwenye shughuli za pasaka ,napo pia wataalani wala usihofu
Sasa kama chuki yao kubwa ni dhidi ya Mmarekani na Mataifa ya Ulaya iweje walipuane wao kwa wao mfano hapo Pakistani tena mbaya zaidi wakiua hadi wanafunzi wa shule?
 
Waarabu ni lazima Walaani Wazungu wakilipuliwa na Waarabu ila si lazima Wazungu kulaani Waarabu wakiuawa na Wazungu! Drone daily zinashusha Mabomu kwa Waarabu na wanakufa hakuna anaetoa Tamko la kulaani. Kama We are equal Waarabu hawana cha kulaani labda tuambiwe tofauti ya waliokufa Brussels na Syria kwa Mabomu iko wapi?
 
Nadhani Waarabu wana matatizo kwenye vichwa vyao sio bure na ni watu wepesi sana kuwa brainwashed kwa mitazamo au imani za kijinga kabisa ambazo hata mtoto mdogo anajua hizi ni sanaa!
 
Waarabu ni lazima Walaani Wazungu wakilipuliwa na Waarabu ila si lazima Wazungu kulaani Waarabu wakiuawa na Wazungu! Drone daily zinashusha Mabomu kwa Waarabu na wanakufa hakuna anaetoa Tamko la kulaani. Kama We are equal Waarabu hawana cha kulaani labda tuambiwe tofauti ya waliokufa Brussels na Syria kwa Mabomu iko wapi?
Zile drones hazipo kwa ajili ya innocent civilians zipo kwa ajili ya kuteketeza ngome za magaidi na maficho yao kosa baya wanalofanya waasi wanaounga mkono Ugaidi ni kuwatumia Raia wasio na hatia kama human shield!sasa wakati mwingine wanaenda kujificha hadi kwenye mahospitali!
 
Tukiwa wakweli tutakuwa na mhadala huru na tuzungumze ukweli na sio mitazamo yetu binafsi!
 
Back
Top Bottom