Sijaona mpinzani aliyehama CHADEMA ila naona waliokuwa CCM wakirudi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Hama hama ya wabunge na madiwani ni somo kwa vyama vyote.

Na Dotto Bulendu

Asubuhi ya leo tumeamka na habari nyingine iliyoambatana na picha ikimuonesha mbunge wa Monduli Bwana Julius Kalanga akiwa na Katibu mwenezi wa CCM Humphrey Polepole huku akitutangazia kuwa amajivua uanachama wa Chadema na kurejea CCM na hivyo kujivua na ubunge.

Anakuwa mbunge wa pili ndani ya wiki moja baada ya mbunge wa Ukonga kupitia Chadema Mwita Waitara na kufanya kama alivyofanya Kalanga usiku wa kuamkia leo bila kupima gharama ambazo serikali inakwenda kutumia kutokana na uamuzi wake.

Nimefanya tathmini kuhusu wabunge watatu walioachana na Chadema na kurejea CCM hususani historia zao nikagundua ni vijana waliokulia na kupitia mafunzo yote ya ndani ya CCM.

Mwita Waitara mpaka anatoka CCM miaka kumi iliyopita alikiwa katibu wa UVCCM mkoa wa Tanga,Goodluck Ole Mollel aliyekuwa mbunge wa Siha na baadae kujiuzulu kabla ya kutejeshwa kupotia CCM kabla hajajiunga na Chadema alikuwa kiongozi ndani ya UVCCM huko Sia,kama ilivyo kwa Kalanga ambaye nae amekulia ndani ya CCM na kupata mafunzo yote ya kiitikadi,kimkakati na kipropaganda ndani ya CCM na wote waliwiva.

Vijana hawa walikuwa mahiri ndani ya CCM lakini kutoka kwao CCM hakukuwa sababu za kiitikadi ama mahaba yao na CCM bali wote waliondoshwa na minyukano ndani ya chama hususani suala la Uongozi.

Mwita akiwa Katibu wa UVCCM mkoani Tanga,nafasi aliyoipata mara baada ya kumaliza masomo yake UDSM aliondoka bada ya kupishana na aliyekuwa mwenyekiti wake wakati huo Dr Emmanuel Nchimbi,Kilikuwa kipindi ambacho Nape alitaka kuvuliwa uanachama na Mwita alikuwa upande wa Nape.

Utaona Mwita hakwenda Chadema kwa sababu za kiitikadi bali matatizo binafsi ndani ya chama cha mapinduzi aliyoyapata,hivyo Mwita alikuwa Chadema kimwili,ila kiroho na kiimani alikuwa CCM.

Kama ilivyokuwa kwa Kalanga,alikuwa mmoja wa wafuasi kindakindani wa Mzee Lowasa,Kalanga hakutoka CCM kwa sababu hakuipenda CCM alitoka ili kumfuata Lowasa,kama Lowasa asingekatwa CCM Kalanga asingeondoka CCM,nae alikuwa Chadema kimwili,kiakili,kiimani alibaki kuwa CCMna ilikuwa lazima siku moja atoke Chadema na ndivyo alivyofanya usiku wa kuamkia leo.

DR Goodluck Mollel,kila mtu anamjua alikuwa kiongozi ndani ya UVCCM ,lakini mbali ya kuwa kiongozi,ndoto yake kubwa ilikuwa awe mbunge,mwaka 2015,hakuona dalili za kuwa mbunge kupitia CCm akaamua kuondoka na kwenda Chadema ili kutimiza ndoto za kuwa mbunge,aliondoka CCm si kwa sababu alivutiwa na falsafa ya Chadema,la hasha alikuwa anasaka ubunge lakini alikuwa Chadema kimwili,Mollel kakukia CCM tangu utoto wake.

Upinzani una makundi mawili,waliokulia kwenye upinzani na wanaufia upinzani na watu walioingia kimwili kusaka ubunge na udiwani,hili ni funzo kwa vyama vya upinzani na ni ushindi wa CCm kuwa jinsi inavyowakuza vijana wake,hata wakiondoka bado wanakuwa wanaikumbuka CCM na inakuwa rahisi kwao kuvitikisa vyama walivyokimbilia.

Mtazame Nape,Mtu aliyepitia kwenye Tanuru na moto,alitembea nchi nzima,alifanya kampeni za kijitoa mhanga tangu kwenye mchakato ndani ya CCM na wakati wa uchaguzi mkuu,Nape akaondolewa kwenye baraza la mawaziri,akatishiwa Risasi,akazuiliwa kuongea,lakini hakusema anaachia ubunge ili asimame kupitia upinzani

Kama haitoshi,Nape akijaribu kuwapigania wananchi wake,anakutana na maneno kama,"Kawaambie wale hizo mbaazi kwani zina protin" alipolilia Pesa za korosho,akaambiwa aondoke kwenye chama,lakini Nape yupo Buyungu anasaka kura za CCM.

Naamini haya wangekutana nayo waliohamia Upinzani kusaka ubunge tu,leo sijui wangekuwa wapi?sijui wangeongea maneno gani?

Lakini leo Nape anatoa funzo kwa vyama vyote kuhusu umuhimu wa kuwakuza vijana wake,kuwafunza itikadi na falsafa,wawe wafia chama kwanza,bahati mbaya Chadema mwaka 2015,iliwapokea wafia CCM na kuwapa nafasi ya kugombea na sasa wapo bize wanatafuta sababu za kurejea CCM.

Mfia falsafa kabla hajaachia udiwani ama ubunge angejiuliza maswali mengi,angejiuliza hivi gharama hizi nasababisha mimi?

Chadema na vyama vya upinzani wasilizwe na haya yanayotokea,wayachukue kama tathmini ya nini kilichotokea miaka mitatu iliyopita na nini wafanye miaka ya mbele katika kuijenga zaidi taasisi zao.

Wimbi ka wana CCM kuhama na kwenda Chadema mwaka 2015,litarejea tena na kwa kishindo mwaka 2019,watakapoanza kurejea CCM na utakuwa upepo mkubwa utakayoicha Chadema asili ya kabla ya 2015.

Mamia ya wana CCM waliondoka na kwenda upinzani hususanj Chadema mwaka 2015,wengine wakapewa nafasi za kugombea ubunge na udiwani si kwa sababu walivutiwa na falsafa ya Chadema la hasha wengi walimfuata Lowasa,kumbuka Lowasa alivyokuwa na wafuasi wengi na wengi ni vijana waliokulia kwenye Chipukizi na wakapanda mpaka UVCCM,vijana wengi waliondoka si kufuata itikadi ya Chadema bali walimfuata Lowasa.

Vyama vya upinzani bado vina nafasi ya kujifunza na kuimarika zaidi kutokana na haya yanayotokea,kikubwa ni kujenga watu wao,viongozi wao wa baadae ambao watazifia na kuzipigania falsafa za vyama vyao.

Julius Nyerere alihakikishia anawajenga wana CCM watakaoifia falsafa na itikadi na ndiyo maana Kingunge alitoka CCm ila hakuchukua kadi ya Chadema kwani alijengwa kuifia falsafa.

Mtu ambaye si mfia falsafa yako ni rahisi sana kuondoka tena kwa sababu nyepesi,Mtazame Nape mfia falsafa ya Ujamaa,yupo CCM kifalsafa na si kwa sababu alimfuata mtu,hivyo hawezi kimbia kirahisi,naamini waliokwenda upinzani kusaka uongozi na si kuifuata falsafa wataendelea kutoka pale tu watakapohakikishiwa nafasi zao na maslahi yao.

Bahati mbaya wanatoka kipindi kibaya,wanasababisha gharama kubwa sana,pesa ambayo ingesaidia kutatua kero za kiuchumi.

Wengine tunadhani wangetoka 2020 ili kutosababisha gharama za uchaguzi kama walivyofanya Mzee Lemberi wakati akitoka CCM na Zitto wakati akitoka Chadema.

Bado naamini wengi waliokwemda Chadema kutoka CCM na wakashinda uchaguzi kwenye nafasi ama ya Udiwani au Ubunge,wakihakikishiwa nafasi zao kwa maana ya kugombea kwenye uchaguzi mdogo wataendelea kutoka na watakaobaki ni wale waliopo upinzani kifalsafa tu.

Nadhani sasa vyama vya upinzani vitapata nafasi ya kufanya tathmini ila visistushwe na hili wimbilazima upite na pia CCM wanaweza tumia fursa hii kufanya tathmini juu ya maudhui ya mafunzo ndani ya jumuiya zao,naamini wana alama nzuri hapa.

Kwa mfia falsasa na itikadi ya chama,hawezi kuondoka kwenye chama kwa sababu haelewani na Mwenyekiti,

Pendekezo langu kwa upinzani

Kama ilivyo kwa CCM ni vizuri sasa wakawa na Program maalum ya kutengeneza vijana na watoto wafia vyama vyao,naamini wanao ila wanahitaji kuwa nao wengi zaidi na wawe wafia falsafa zao.

CCM wamekuwa wanafanya hivi na wanaendelea kufanya hivi na sasa wanajenga chuo huko Bagamoyo,nafahamu Chadema walifanya hivyo miaka ya nyuma,CUF nadhani wanayo mafunzo kwa vijana wao,Chadema nakunbuka waliwapa vijana mafunzo vijana wao wakati wa Dr Slaa na hata baadhi kwenda nje,ila wanahitajika kuwa na vyuo na wakufunzi wao watakaowaandaa vijana wafia falsafa ya chama.

Wasalaam
 
Last edited:
Asilimia 90 ya wanachama wa CDM walikuwa CCM ndio wakahama. Kama ukweli ni maandishi ya uzi huu basi cha muhimu ni kwa CDM kuwa wabunifu katika kutafuta wanachama wapya ambao hawajawahi kuwa na ukaribu wowote ule na CCM.

Uzi utakuwa umeandikwa wakati mtu akijiuma meno kwa sababu ya hasira.
 
Na mnyampala alisha sema.....
Wote wanao rudi zizini wanakua wamekatwa mikia, hivyo anawajua.... tehteehhh
 
Back
Top Bottom