Sijaona mbadala wa Mkude Simba VS Platinum

Sijakuelewa mkuu, yani madhaifu ya mkude yameanza kaonekana baada ya fraga kuanza kuchezeshwa, unajua kama hao wanacheza namba tofauti? Na kama unataka mkude acheze vizuri inabid kuwe na Natural namba 6 ambae ni fraga ambae anampuguzia majukumu ya kukaba kwakuwa hiyo sio kazi yake namba 1, mkude ni holding hivo kazi yake sio kukaba na ndomana anafanya makosa mengi kwenye kukaba.
Mnajikuta wachambuzi kumbe hewa tu.
 
Mkuu mkude anacheza pamoja na fraga, na siku ya derby ni kweli alisababisha faul iliyozaa goli ila Haina maana kwamba alikuwa anacheza kiungo mkabaji, siku ile kiungo mkabaji alikuwa ni mzamiru, sikatai mkude sio mzuri kwenye kukaba ila sishangai kwakuwa sio kazi yake namba 1 ispokuwa ni ziada tu, mkude acheze mbele ya mtu kama fraga au kotei ndo utamuonea raha

Ila akicheza na mzamiru mambo yanakuwa tafrani maana mzamiru anakaba sana ila anapoteza sana mipira hivo kupelekea mkude kuvaa jukumu la kuanza kukaba ilhali hayupo vizuri kwenye discipline ya ukabaji ndo hapo anakuwa kwenye hatari ya kupata njano mara kwa mara, ila kama kuna 6 mzuri kazi yake ni kusambaza mipira kwa mawing back wanapo overlap pamoja na viungo maana ni mzuri sana kwa kupeleka timu mbele kwakuwa anapiga long range za accuracy sana
Nkukumbushe pia, faulo ya udisongo iliyosababisha goli ilifanywa na mkude kwenye mazingira ambayo mabeki walkua was kutosha na mshambuliaji angewezwa kubanwa tofauti bila madhara
 
Nkukumbushe pia, faulo ya udisongo iliyosababisha goli ilifanywa na mkude kwenye mazingira ambayo mabeki walkua was kutosha na mshambuliaji angewezwa kubanwa tofauti bila madhara
Na ile ya kumkwatua Morrison mechi na Yanga wakatufunga goli moja kwa hiyo adhabu alifanya huyohuyo mtu.
 
Kwangu mimi bora Muzamiru anayekaba sana dakika zote 90 pamoja na mapungufu yake ya kupoteza pasi anakuwa anaisadiia timu kwa kiasi fulani kuiweka salama kuliko mapungufu ya Mkude ya kushindwa kukaba na akizidiwa huwa anacheza rafu za kijinga kabisa na matokeo yake anawapa kazi Wawa na Onyango kufuta makosa yake.

Na watu wengi wanamuona Mkude mchezaji wa maana kutokana na zile pasi zake fupi fupi kwenda kwa mabeki wakati na wa pembeni badala ya kupiga "long pass" na "penetration pass" kusogeza timu mbele kwa haraka. Kiungo mzuri wa nyuma anatakiwa afanye kazi mbili kwa pamoja kwanza atulize mashambulizi ya timu pinzani ili mabeki wake wa katikati wasipate kashi kashi na pili ni kuanzisha mashambulizi ya haraka haraka kwenda kwenye lango la timu pinzani. Mkude hana uwezo wa kutimiza majukumu yote hayo mawili kwa asilimia 100% ndio sababu toka amefungiwa timu imeimarika kwa kuwa wachezaji waliopewa hayo majukum wametimiza kwa ufasaha japo hawajafikia kiwango cha mwamba Fraga.
 
Back
Top Bottom