SIIONI ELIMU YA VIWANDA!

MAKA Jr

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2016
Posts
267
Reaction score
209
Ninachoweza kusema ni "Mungu atusaidie" kwa huruma yake na akipenda vinginevyo tunachezacheza tena bila utaratibu.
Jamii inajua kuvuruga vichwa vya watu haiwezi kuwa na msingi wa jambo lolote lile. Nasema haya kwa sababu wizara ya elimu imekuwa ikichezewa kama vile haina msingi kwenye maendeleo ya nchi.
Leo tunaambiwa tunaenda kwenye 'Uchumi wa Viwanda', neno ambalo naogopa hadi kulisema maana nahisi linaonewa tu. Unawaandaje vijana wa kufanya kazi viwandani kama mfumo mzima wa elimu unawajenga kufanya kazi ofisini? Hapa tunacheza tu.
Leo hii kamuulize Mwanafunzi wa kidato cha NNE alime bustani ya mbogamboga halafu uone mwitikio wake!
Tuna safari ndefu!
 
Tumetembea nchi nyingi sana duniani. Na safari nyingi tumejikuta tuko viwandani.

Tukisikia "Industrialist" tusirudi kwenye karne ya 17 enzi ya Mapinduzi ya viwanda.

Mzawa mwenzangu, nataka kukudokeza tuu, teknolojia imefika mbali sana.
Kuwa "Industrialist" kwenye hii karne ni rahisi sana.

Ndio maana tunasema serikali ina uwezo wa kuwawezesha wananchi wake bila kutegemea wawekezaji.

Viwanda ni kama utamaduni fulani, na ina jamii yake, na kuingia kwenye duara hili, hamna ugumu wowote.

Suala kubwa ni kutafuta soko na kupambana na mashindano, pja kudumisha ubora wa bidhaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…