Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,971
Mkurugenzi wa Tanesco,William Mhando
Leon Bahati
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema linakusudia kukata rufaa kupinga hukumu inayowataka kuilipa kampuni ya Dowans fidia ya mabilioni ya fedha, lakini likatahadharisha kuwa kuna siri nyingi zilizo kwenye kesi hiyo ambazo ikibidi watalazimika kuziweka hadharani.
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja juzi aliitaka Tanesco kutoa maelezo ya kina kuhusu hukumu ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Dowans kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC), ikitaka ilipwe fidia na shirika hilo baada ya kukatisha mkataba wa kuzalisha umeme mwaka 2008.
Mahakama hiyo iliitia hatiani Tanesco na kuitaka ilipe fidia ya zaidi ya Sh185 bilioni kwa Dowans.
Jana Tanesco ilitangaza nia hiyo ya kukata rufaa huku ikijigamba kuwa iliibuka kidedea kwenye kesi kampuni ya Richmond Development LLC na sasa italipwa dola za Marekani 1.2 milioni sawa na Sh 2.9 bilioni.
Taarifa maalumu iliyotolewa na Tanesco jana iliweka wazi kwamba inasubiri ICC isajili hukumu hiyo kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, ili shirika hilo liweze kutathmini na kuamua hatua nyingine za kuchukua.
Hapo kwenye red pananitia mashaka! Hizo siri kwa nini zinataka kutolewa wakati mambo yamekuwa magumu? Hizo siri ziko kwa manufaa ya nani hasa? Akina Lowasa wanakula kuku kwa mrija na wametuachia hasara kubwa sana tunayoendelea kuingia baada ya kujihusisha na kampuni hewa ya Richmond!
Kwa habari zaidi soma MWANANCHI.