1. Pole kongozi naona majani yamekakamaa/hajarelax, nadhani kuna shida ya baridi, au maji (kiasi kidogo) ,au kuna shida ya wadudu (white flies)=Elezea kuna shida yoyote kati ya hizo?
2.Udongo wako unaonekana una mfinyanzi kiasi fulani kwa ndani ndio maana unaona hiyo nyufa, sasa kaka hukuupiga hallo vizuri wakati wa maandalizi maana yake mizizi ya mmea inashindwa kupita kwa urahisi (Hard Pan).
3.Sina hakika sana na dawa za wadudu unazotumia kama ni sahihi, jitahidi kutumia dawa za wadudu ambazo pale chini karibu na kitako cha kopo , ukute kuna ufito wa rangi ya blue au Kijani, ukitumia zenye ufito wa rangi ya njano au red, hizo huua nyuki, na hufanya mmmea kuwa weak kidogo hasa kama unaspray mchana wa jua kali , na hakna maji ya kutosha. Dawa za ufito wa njano au nyekundu huua nyuki wanaosaidia uchavushaji, wakifa nyuki uwezekano wa kupata maua na matunda dhaifu ni mkubwa.
4. Hiyo mbegu uliyopanda ni aina gani (Kito?. Zebra?, Sukari F1?Sugar king?....).
5.Je umetumia booster (Maua/Matunda) yoyote?