Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 505
- 887
Sasa kama ujafurahishwa mbona umefika huko Bungeni? au unatuletea unafiki wako hapa!
Wewe kama umeona kuna hali mbaya kwa Watanzania wakati huu ungekataa, ila ukakubali kabisa na kufika hadi huko. Pesa tamu wewe tuache sisi kutulamba mikono wakati unataka kuvila vidole vyetu.
===============
Mbunge Mteule wa Viti Maalum kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Sigrada Mligo, amesema hajafurahishwa na uteuzi wake wa nafasi hiyo, akidai kuwa alinyang’anywa ushindi wa Ubunge wa Jimbo na kupewa nafasi ya ubunge wa Viti Maalum.
Mligo ametoa kauli hiyo leo, Novemba 10, 2025, katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mara baada ya kujisajili kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 13, unaotarajiwa kuanza Novemba 11, 2025.
Mligo amesema hajafurahishwa na namna alivyoteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalum katika Mkoa wa Njombe, hasa katika kipindi ambacho Watanzania wanapitia hali ngumu ya Kisiasa na Kijamii.
Soma Pia: Tume Uhuru ya Taifa ya Uchaguzi INEC yatoa orodha wabunge viti maalum CCM wapo 113, CHAUMMA 2
"Wakati mimi naapishwa, kuna watu Mtaani wamezika ndugu zao, watu wamekufa. Taifa liko kimya. Mimi sijafurahia kuwa Mbunge katika Bunge ambalo taifa linavuja damu,” amesema Bi. Mligo.