Sifurahii kuwa 'single woman', sijui nifanyeje

Mimi ni Mkristo, miaka 30, urefu wa wastani, mweusi, mwembamba. Kabila kutoka kusini mwa tz. Nina kazi na kipato kizuri tu. Nina ishi pekee yangu. Nina gari na kiwanja na if all goes well ninategemea kuanza kujenga mwakani. Elimu nina degree, na kwa sasa ninamalizia masters yangu.

Sijawahi kuolewa na sina mtoto.

Nimekua kwenye mahusiano ya mbali/long distance yapata miaka mitano sasa na mkaka (34yrs) ambae ninampenda na yeye naamini ananipenda ila naona miaka inazidi kuyoyoma bila dalili za kijana huyu kupropose.Tulifahamiana tukiwa chuoni lakini baada ya kugraduate tukapata kazi miji tofauti. Wote ni waajiriwa wa serikalini. Tunawasiliana kwa simu na kuonana ni mara chache mno.

Natamani sana kuolewa na baadae kupata mtoto lakini hilo bado halijatokea. Nikimuuliza anasema bado, nisubiri, kwa sasa familia yake bado inamtegemea.

Najua yote ni mipango ya Mungu na niko tayari kwa lolote alilopanga juu yangu lakini ukweli ni kwamba inaniuma sana kuona wenzangu wa rika langu wana familia na mie. In a sense najihesabu kama I am a single woman.

Naomba ushauri na maneno ya kunipa faraja ili nijisikie siko peke yangu kwenye situation hii.

PoleeeH, Mungu ATAKUSAIDIA...
 
Pole mpendwa Sonnet kwa yaliyokukuta. Mimi nakushauri endelea kuwa mvumilivu huku ukimwomba Mungu ili impendeze aweze kukujalia mume ambaye alikuandalia tangu kuumbwa kwako.
 
Last edited by a moderator:
Sonnet vp umewahi kwenda anakoishi huyo jamaa yako?
Maana unaweza kulaumu tu wakat hata ww hueleweki.
 
Last edited by a moderator:
Ndio ni mtihani Mgumu. Tafuta watumishi wenye maono ya kuomba wakusaidie pengine unahitaji utakaso bahati/nyota ( Mama jusi) ya kuolewa imefungwa na mapepo nielewa hapo. Mimi nina miaka 38 lakini sijao sababu mipago yangu sijakamisha kwa miaka 3 ijayo pengine. Na huyo kaka yaweza kuwa hivyo tu. Uwe makini tu mlango uliongia katika ndoa ukatokea huo huo.. 0654705550
 
Kuna asilimia ndogo sana ya kupata mume humu hasa baada ya bandiko hili.....wapo wengi watakaojifanya kina baba huruma ila hawana lolote lengo lao ni kukuumiza then wakucheke.....

You are rait..Nadhani amekupata vizuri..Na wengi uwa hawako serious..Just kuchezea feelings za mtu tu..
 
acha kuwaharibia dili wenzio ww. Waache wajaribu kurusha ndoana huenda anaweza kunasa.

Halafu kwan wa humu sio wanaume? Mbona wengne tumeshaoa na tuna watoto.

Tatizo ni kwamba ninyi wenyewe mliooa mtaenda na kujifanya mko singo na ni wapweke kama yeye...hiyo jinsia weka mbali na watoto asee
 
Tatizo ni kwamba ninyi wenyewe mliooa mtaenda na kujifanya mko singo na ni wapweke kama yeye...hiyo jinsia weka mbali na watoto asee

mmmh! Naona umamua kuwaharibia kabisa wenzio. Hebu kaa kimya bhana unawafukuzia wenzio njiwa
 
Ila siku hizi wakaka hawaeleweki jmn,MTU anakupotezea mda mwisho ananzanyenye wewe Fanya maombi Dada iko siku japo mda ndio huo wakuitwa mama,Mungu akufanyie wepesi ktk hili nmeumia sana iase cjui wanakuaje hawa jamaa hasa hawa town,lkn huko vijijin mbona wanaoa tu bila shida,subiri upate majibu yake sasa utashangaa.
 
Duh bahati ya mtende niPM haraka nisijebadili mawazo.

Mimi ni mwanaume single nina miaka 35.
Elimu kidato cha tatu B,nipi katika mikakati ya kufanya mtihani wa kidato cha nne natumaini tukiungana pamoja utanisaidia katika masomo yangu.
Kazi yangu mwendesha boda boda (yangu sijaajiriwa)
Nina kiwanja bado sijajenga kwakuwa na wewe una kiwanja tutauza kiwanja kimoja halafu tunajenga bila mbinde wala mbwembwe.
Bibie Sonnet niwakati wa kufanya maamuzi magumu sasa ukichelewa chelewa utakuta mwana si wako bahati haidondoki mara mbili.

Nasubiri majibu yako kwa hamu na shauku.
 
Last edited by a moderator:
Mweke wazi mwenzio kwa maana kwa sababu upo naye (hata kama ni long distance) inafanya ngumu kwako kufunguka kwa wengine.
 
Back
Top Bottom