jaffari matimbwa
Member
- Mar 24, 2017
- 23
- 13
Naomba kuliza sifa za kujiunga na chuo cha Hombolo Dodoma kwa kozi development of planning and adminstration.
Kuna chuo cha Hombolo dodoma ambacho kipo chini ya Tamisemi..Naomba kuliza sifa za kujiunga na chuo cha mipango ombolo kwa kozi development of planning and adminstration.
GoodCHUO CHA SERIKALI ZA MITAA
S.L.P. 1125, DODOMA Simu: 026- 2961101 Fax: 026 -2961100,
Barua Pepe: info@lgti.ac.tz
Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa (Hombolo) anakaribisha maombi ya kujiunga na masomo kwa mwaka 2017/2018 katika ngazi ya Astashahada (Certifiacate) na Stashahada (Diploma) kwenye fani zifuatazo:-
1. Utawala katika Serikali za Mitaa (Local Government Administration)
2. Usimamizi wa Rasilimali Watu (Human Resource Management)
3. Maendeleo ya Jamii (Community Development)
4. Uhasibu na Fedha katika Serikali za Mitaa (Local Government Accounting and Finance)
5. Utunzaji wa kumbukumbu (Records, Archives and Information Management)
6. Ugavi na Ununuzi (Procurement and Supplies Management)
SIFA: Mwombaji wa Astashahada (Certifiacate) awe amepata angalau ufaulu wa “D” 4 za Kidato cha Nne na kwa mwombaji wa Stashahada (Diploma) awe amepata angalau ufaulu wa “Principal” moja na “Subsidiary” moja ya Kidato cha Sita AU awe na cheti toka Chuo chochote kinachotambulika na Serikali.
ANGALIZO:
1. Moja kati ya D nne ISIWE ya somo la Dini.
2. Kozi ya Uhasibu na Fedha katika Serikali za Mitaa inahitaji mwombaji awe amefaulu somo la HISABATI katika mtihani wake wa kidato cha nne.
3. Kama mwombaji amefanya mtihani wa kidato cha nne zaidi ya mara moja, aambatanishe nakala za vyeti vyake vya awamu zote za mithani alizofanya.
Fomu zinapatikana:
1. Chuoni, Hombolo
2. Kampasi ya Dodoma Mjini (Area C)
3. Katika tovuti ya Chuo www.lgti.ac.tz
Fomu iliyokwisha jazwa iambatanishwe na malipo ya ada ya maombi ya shilingi 30,000/=kwenye Akaunti Na .50501100209 ya Benki ya NMB DODOMA.
Maombi yatumwe kwa mkono au kwa posta kwenda kwenye anuani ifuatyo:
Mkuu wa Chuo,
Chuo cha Serikali za Mitaa,
S. L. P 1125, Dodoma.
MWISHO wa kupokea maombi ni tarehe 31/05/2017
Kwa maelezo zaidi piga simu namba:
0717 487 420
0754 415 659
0755 241 010
Jaman sa kama una d zakutosha na hiyo ya maths huna ndo hutakiwi kabsa au
Wanataka D 4 kama math ana D anaweza akasomea Human Resources ManagementJaman sa kama una d zakutosha na hiyo ya maths huna ndo hutakiwi kabsa au