Sifa zipi anatakiwa kuwa nazo Rais wa Tanzania ya sasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sifa zipi anatakiwa kuwa nazo Rais wa Tanzania ya sasa?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Tabutupu, Jan 10, 2017.

 1. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2017
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,649
  Likes Received: 4,390
  Trophy Points: 280
  Hivi kwa dunia ya sasa na Tanzania ya Leo, ukipewa nafasi uandike kwenye katiba sifa au vigezo ambavyo unaona Rais anatakiwa kuwa navyo ungeweka vipi, mfano elimu yake, ukomavu kiasiasa, kiuongozi, kidiplomasia, etc.

  Yapo maeneo mengi ambayo kwa viongozi tulionao yanapwaya, mfano; Kuna mmoja anaamini kukuza demokrasia ni kukuza uchumi, lakini mwingine anaamini hata bila demokrasia uchumi utakua. Hii ni mitazamo tuu japo sijajua kama inatokana na uelewa mdogo wa eneo LA uchumi kwa maana kubwa au ndogo.

  Wewe unafikiri ni sifa zipi Rais wa Tanzania ya leo anatakiwa kuwa nazo ili kuifanya Tanzania iwe mfano katika kila eneo duniani?
  From Uongozi Institute


  Matusi mwiko..
   
 2. makilo

  makilo JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2017
  Joined: Dec 15, 2015
  Messages: 960
  Likes Received: 1,513
  Trophy Points: 180
  Hata Tukimwambia hatosadiki
   
 3. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2017
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,357
  Likes Received: 6,539
  Trophy Points: 280
  Ukawa watakwambia awe na sifa za makamanda wao kama Lema, sugu na kubenea.
   
 4. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2017
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,649
  Likes Received: 4,390
  Trophy Points: 280
  hii haina maana tunataka sifa za mkuuu, bali hata atakaye kuja , cha msingi tuweke hapa sifa za Rais tumtakaye
   
 5. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2017
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,649
  Likes Received: 4,390
  Trophy Points: 280
  ukawa inakujaje hapa Stroke?
   
 6. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #6
  Jan 10, 2017
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,092
  Likes Received: 11,230
  Trophy Points: 280
  Anaefuata katiba na sheria..
   
 7. H

  Hamza Ayub Member

  #7
  Jan 10, 2017
  Joined: Nov 24, 2016
  Messages: 6
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Mwenye msimamo katika maamuzi yake bila kuvunja Sheria
   
 8. MKWEPA KODI

  MKWEPA KODI JF-Expert Member

  #8
  Jan 10, 2017
  Joined: Nov 28, 2015
  Messages: 18,143
  Likes Received: 36,859
  Trophy Points: 280
  Awe na uwezo wa kuelezea mito na vijiji vya bukoba kwa ufasaha kama vile mto ngono, kijiji cha katerero n.k.

  Awe na uwezo pia wa kuhamasisha wananchi kufyatua watoto ili wapate elimu bure
   
 9. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #9
  Jan 10, 2017
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Mkuu umejua ningekutukana tuu.Haya maswali mbona sio ya msingi sana kama kuhoji matamko ya wasomi walio wababishaji kama matapeli mjini.
   
 10. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #10
  Jan 10, 2017
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,649
  Likes Received: 4,390
  Trophy Points: 280
  tz tunashida, anyway nafikiri elimu inabidi kiwe kigezo cha mwisho maana hatujaona ikitekeleza wajibu wake katika jamii yetu.
   
 11. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #11
  Jan 10, 2017
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,649
  Likes Received: 4,390
  Trophy Points: 280
  Ongalia maelezo ya mkapa
   
 12. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #12
  Jan 10, 2017
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Mkuu tatizo sio elimu tuu,tupo katika mzunguko mbaya, elimu ili k uiboresha kunahitajika pesa, pesa inahitaji elimu, elimu i nahitaji afya, afya inahitaji pesa na chakula, vyote vinahitaji maadili, maadili nayo yanahitaji elimu.Havitakaa vipatikane vyote kwa mwendo huu.
   
 13. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #13
  Jan 10, 2017
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,649
  Likes Received: 4,390
  Trophy Points: 280
  nadhani mchakato wa kuwapa viongozi ndio hauja kaa sawa..
   
 14. brayzeking

  brayzeking JF-Expert Member

  #14
  Jan 10, 2017
  Joined: Jun 23, 2016
  Messages: 271
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Utawala bora unaofata sheria na katiba ya nchi
   
 15. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2017
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,736
  Likes Received: 1,447
  Trophy Points: 280
  Asante mleta hoja,

  1. Kwanza huwezi kupata kiongozi sahihi au bora kwa njia mbovu au za kubahatisha. Kwa hiyo mahali pa kuanzia ni kwenye Katiba ya nchi, halafu sheria na kanuni za namna ya kumpata Rais nk. Pia huwezi kupata viongozi wazuri na bora kwenye vyama vya siasa ikiwa Katiba ya Nchi ni mbovu. Kwa sababu kwanini vyama viweke vigezo ambavyo kwenye mizani ya Taifa ni irrelevant? Hivyo umagumashi na ubovu unatapakaa na kusambaa toka Juu kabisa mpaka kwenye vyama vya siasa hadi ngazi za msingi/shina. Mwisho wa siku ni ubovu, kushindwa, umaskini, ujinga nk

  2. Tanzania, kama zilivyo nchi nyingi inahitaji kiongozi/mtu bora na sahihi kwa wakati sahihi ili kuwa Rais ili twende mbele na kupata maendeleo halisi na sio ya kwenye makaratasi na majukwaa. Kiongozi lazima atokane na Watanzania na miongoni mwa Watanzania. Shida yetu kubwa hatuna taasisi rasmi na zenye uwezo wa kuandaa viongozi. Pia hatuna uwezo na utashi wa kupembua watu.

  Kwa mfano CCM, ni chama kikongwe na kinajipigia chapuo kuwa huwa kina utaratibu na mafunzo ya kuandaa wanachama na makada wao kwa nafasi za juu kama Urais. CCM ilitupa Mwinyi, Mkapa, Kikwete na sasa Magufuli. Je ina la kujivunia? Ilipotupa Mwinyi baadaye ikaja ikatuambia Mkapa ndio the best. Ilipotupa Kikwete ilituhakikishia atafanya wonders lakini sasa inatuambia Magufuli ndio the best!??!. Miaka imepita, umaskini, ujinga na maradhi bado vinatutawala na kututafuna kama Taifa. Matokeo ya huo "uandaaji na michujo" kwa Taifa ni hasi (negative). Hali hiyo hiyo iko CHADEMA, CUF, ACT nk. Matokeo hayaleti matumaini kuwa tutakaa tupate kiongozi bora na sahihi kwa njia hizi. Kumbukeni "Insanity is doing same things (again) and expect different results"

  3. Tanzania lazima ibadilike kimuundo na ki-utawala. Serikali 3 ni jibu la wengi, lakini pia je mwaonaje kama Tanganyika ingetawaliwa kifalme? Hilo laweza kuwa jibu sahihi kwa sababu hii demokrasia yetu (toka 1992) ni "fake" i.e. ya makaratasi na majukwani tu lakini haina uhusiano wala utashi na hali halisi na mahitaji yetu na haitufikishi mbele kwenye malengo yetu na kwa spidi sahihi.

  Hivi unawezaje kusema kuwa Wenyeviti wa Vijiji/Mitaa/Vitongoji wawe washiriki wa vikao tu lakini Watendaji (watumishi wa Serikali kwa ngazi hizo) ndio everything halafu uniambie tuko siriaz au eti demokrasia ina nafasi nchi hii? Unawezaje kuwapa nguvu ma-RC, ma-DC , ma-DED na hapohapo kuwadhalilisha na kuwaminya Wabunge na Madiwani ambao hasa ndo wawakilishi "sahihi" wa Wananchi? Demokrasia yetu ni mfu na ya ovyo kabisa.

  Ndio maana nachokoza fikra na mawazo (kwa wale wenye uwezo na nafasi ya kufikiri tu) je kwanini tusifikiri nje na mbali ya boksi kuhusu namna ya kujitawala?

  4. Baada ya hapo juu, Rais lazima awe na uwezo (naturally gifted and learned), awe mwenye weledi na uzoefu mpana wa uongozi na siasa, asiwe mbinafsi, asiwe mbaguzi, awe na upendo na mnyenyekevu, mwenye hekima na busara, awe na hofu ya MUNGU kweli.
   
 16. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2017
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,649
  Likes Received: 4,390
  Trophy Points: 280
  mkuu , big up, nimeupenda mchango wako ambao umegusa karibia kila kitu, Swala LA katiba nadhani ndio msingi wa kila kitu. Ngoja waje wengine tuone michango yao.
   
Loading...