Sifa za Rais anayetufaa TANZANIA!

Nyami2010

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
227
50
Kwa sala na dua, ninaomba Tanzania tumpate Rais mwenye sifa zifuatazo:

1. Awe katili kwa waongo, wapenda rushwa, wezi, mafisadi na wazembe kazini
2. Asiwe tajiri wala masikini
3. Awe na kisomo kuanzia shahada ya uzamili
4. Asitoke kabira lolote maarufu na kubwa nchini
5. Asiwe na umri chini ya miaka 40 na asizidi miaka 50
6. Awe kiukweli ni mtoto wa Mkulima
7. Akiishapata Urais, ahame chama kilichomwingiza madarakani kama alivyofanya Rais Dkt Bingu wa Mutharika wa Malawi, 2005.
10......................
11.....................
12.......................
13......................
14......................
Naomba ongezeni sifa uzipendazo kwa kadili uwezavyo..................
 
jeshi lishike hatamu tu watawala wameshindwa uandaliwe uchanguzi mwingine full stop . halafu tutaweka mhandisi mmoja atawaongozea nchi .maana sasa naona kila ngwini tunaye muweka anashindwa kazi.
 
Ni kweli, Dictator anaweza kutusaidia.........japo wengi tutaumia!

Dictator Idd Amin Dadaa aliua watu wengi kitali Uganda, lakini aliweka misingi bora ya Uchumi kwa kuwafukuza Waasia wanyonyaji Uganda mnamo miaka ya 1970. Rais Y. Kaguta Museveni anatamba juu ya misingi iliojengwa na Marehemu Idd Amin...RIP.
 
we need a dictator for atleast 10 years, ili tuwe kama china na indonesia
wazo zuri tunabembelezana sana tena kama ikifahamika mtu kala rushwa piga risasi kweupe ili tuheshimiane . Vinginevyo tutalia na kusaga meno . Hakuna demokrasia duniani
 
Mbona kikwete na mkapa wametoka makabila madogo lakini wametufikisha hapa tulipo?.......tuangalie kiongozi mweneye sifa za maana sio huo utumbo
 
SIFA ZA MTANZANIA ANAYETUFAA LEO:A S 103:

Haijalishi anatoka familia gani, kabila gani, dini gani , jinsia gani n.k,

Awe mwaminifu, mchapakazi kweli kweli, na aliye tayari kutumia kura yake kuchagua Viongozi bora dhidi ya wenye sifa hafifu bila ushabiki au kufuatanana na nani analiyempa hongo (kubwa). Aidha awe tayari kukataa katakata rafiki yeyote mzembe na au asiye mwadilifu ambaye anashindwa kutekeleza yale tunayokubaliana kwa manufafa ya Taifa.
 
Kwa sala na dua, ninaomba Tanzania tumpate Rais mwenye sifa zifuatazo:

1. Awe katili kwa waongo, wapenda rushwa, wezi, mafisadi na wazembe kazini
2. Asiwe tajiri wala masikini
3. Awe na kisomo kuanzia shahada ya uzamili
4. Asitoke kabira lolote maarufu na kubwa nchini
5. Asiwe na umri chini ya miaka 40 na asizidi miaka 50
6. Awe kiukweli ni mtoto wa Mkulima
7. Akiishapata Urais, ahame chama kilichomwingiza madarakani kama alivyofanya Rais Dkt Bingu wa Mutharika wa Malawi, 2005.
10......................
11.....................
12.......................
13......................
14......................
Naomba ongezeni sifa uzipendazo kwa kadili uwezavyo..................

awe mzalendo, mwenye kupigania Tanganyika irudi ,asiwe mwenye kuongozwa na itikadi na ilani za ccm.

arudishe katiba ya Tanganyika ili kusimamia mambo ya Tanganyika na historia ya Tanganyika.
 
Ndo maana nkasema hii nchi kama slaa hatakuwa rais basi tuwe na dikteta awakamue jamaa!
 
Back
Top Bottom