Habari zenu mabibi na mabwana
Baada ya kupitia vitabu baadhi nikapata kitu ambacho nimeona nilete kwa ajili ya kujifunza na kuongezeana ujuzi
Kitu chenyewe ni NDOA
=>Ndoa ni muunganiko wa hiyari kati ya mwanaume na mwanamke unaokusudiwa kudumu katika maisha yao yote.
SIFA ZA NDOA HALALI NI ZIPI
=>Ndoa lazima iwe ya hiyari kati ya mwanamke na mwanaume. Udanganyifu, kurubuniwa na ulaghai kunafanya ndoa isiwe halali. Ndoa za kuchaguliwa wenza na ndoa za mikeka hazitambuliwi kisheria.
=>Ndoa ni lazima iwe ya kudumu, ndoa ni lazima iwe ya kudumu vinginevyo kikatokea kifo ama talaka. Ndoa za mikataba hazitambuliwi.
=>Ndoa ni lazima iwe ya jinsia mbili tofauti. Ndoa za jinsia moja hazina uhalali kisheria.
=>Ndugu wa damu au ndugu wa karibu hawaruhusiwi kuoana.
=>Watu wanaotakiwa kufunga ndoa lazima wawe na umri kuanzia miaka 18 na zaidi. Lakini mwanamke mwenye umri wa chini ya miaka 18 anaruhusiwa kuolewa kwa idhini ya baba yake.
=>Kama wafunga ndoa mmoja wao ana ndoa ya mke mmoja basi hawezi kufunga ndoa nyingine. Mtu mwenye ndoa ya wake wengi hawezi kufunga ndoa ya mke mmoja.
=>Kusiwe na pingamizi la aina yeyote na ndoa itangazwe siku 21 kabla ya kufungwa.
=>Mfungisha ndoa lazima awe na mamlaka ya kufungisha ndoa.
=>Lazima wakati wa kufungisha ndoa kuwe na mashahidi wasiopungua wawili.
=>Wafunga ndoa wote lazima wawepo siku ya kufunga ndoa.
MAMBO YATAKAYOFANYA NDOA KUWA BATILI
● Kutoweza kufanya tendo la ndoa.
● Mke kudhihirika kuwa alikuwa na mimba ya mwanaume mwingine.
● Mmoja wa wanandoa kudhihirika kuwa na kichaa au kifafa.
● Mmoja wa wanandoa kudhihirika kuwa alikuwa ana magonjwa ya zinaa.
● Mwanandoa mmoja kukataa kwa makusudi kufanya tendo
la ndoa tangu ndoa kufungwa.
Naomba kuwasilisha.