Sifa za mwanaume anayekupenda... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sifa za mwanaume anayekupenda...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by chriss brown, Dec 18, 2011.

 1. chriss brown

  chriss brown JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  ANAVYOTAZAMA
  Mwanasaikolojia Zick Rubin kutoka Chuo cha Havard nchini Marekani aliwahi kusema kwamba watu wanaopendana hutumia asilimia 75 kutazamana kuliko wasiopendana, ambao kiwango chao ni asilimia 30-50.

  Hii ina maana kwamba mwanaume anapotumia muda wake mwingi kumtazama msichana na kugeuka taratibu kuangalia vitu vingine kama mtu asiyependa kuacha kumwangalia, ujue anampenda.

  MIPANGO
  Mwanaume anayekupenda atakushirikisha kwenye mipango yake hasa ya muda mrefu. Mfano akitaka kununua kiwanja, kujenga nyumba atakuambia na pengine kutaka mchango wako wa hali na mali katika kulifanikisha hilo. Ukiona mwanaume anakuficha mambo yake, tambua kuwa huyo ana walakini kwenye penzi la dhati na la muda mrefu.

  ATAONESHA HUZUNI
  Katika maisha ya mapenzi kuna wakati wa kuhuzunika. Mwanaume mwenye upendo wa dhati atashirikiana nawe wakati wa huzuni na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unapata furaha.

  ATAKUAMINI
  Dalili nyingine ya kupendwa na mwanaume ni kuaminiwa kwenye maisha kwa ujumla. Yaani mwanaume anayekupenda hatakuficha kitu, mfano pesa zake, atakupa uhuru kwenye simu yake na kukuamini katika usimamizi wa miradi yake.

  ATAKUPA NAFASI
  Ninapozungumzia nafasi nina maana atakukaribisha kwake bila hofu na kukupa nafasi ya kuingia na kutoka bila mipaka, atakupa nafasi ya kuweka vitu vyako kwenye kabati na kuruhusu nguo, picha na vitu vyako kuonekana wakati wote chumbani kwake.

  UTAKUWA MWANAFAMILIA
  Mwanaume aliyefikia chaguo la mwisho kwa mwanamke humshirikisha mpenzi wake kwenye masuala yake ya kifamilia, mfano atamwalika kwenye vikao vya harusi, kipaimara, atatoa nafasi ya kuambatana naye kuona wagonjwa, kusalimia ndugu na atakuwa huru kukutambulisha kwao.

  ATAZUNGUMZA NAWE KUHUSU WATOTO
  Kwa kuwa wanaume wengi hufikiria kuwa na familia, mwanaume anayekupenda atazungumza nawe mipango ya kupata watoto kwa kuwa atakuwa amekuchagua wewe kuwa mama wa wanaye na atapenda mazungumzo hayo.

  ATAKUSAIDIA
  Kwa kuwa kukwama ni sehemu ya maisha yetu, mwanaume anayekupenda atakuwa tayari kukusaidia unapokwama. Kila mara atahakikisha kuwa unakuwa na mafanikio na yeye atakuwa tayari kukupunguzia usumbufu wa maisha, kwa kukufuata kazini, kukusaidia baadhi ya mambo na hata ya nyumbani.

  ATAJITOLEA
  Ninaposema kujitolea ninamaanisha atakuwa tayari kufanya mambo yako na kuyaweka yake nyuma. Kwa mfano akiwa anapenda mpira na siku hiyo kuna mechi, lakini muda huo ukamwambia akufuate kwa mjomba wako atakuwa tayari kuacha furaha yake na kukujali wewe. Huyu ni mwanaume anayekupenda kwa dhati.

  ATAAMBATANA NAWE
  Wapenzi wengi wasiokuwa na mapenzi ya dhati huona aibu kuambatana na wapenzi wao kwenye mikusanyiko ya watu, lakini mwanaume anayekupenda atafurahia kutoka moyoni kuongozana nawe kwenye halaiki ya watu na kufurahia uwepo wako bila kuona aibu.

  Mada hii inaishia hapa, hebu jiulize mwanadada, huyo uliyenaye anakufanyia haya, kama sivyo kwa kiwango kikubwa utakuwa na kazi ya kuhakiki penzi lako na pengine kujenga misingi mipya ya uhusiano wenu kabla haujavunjika.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  jamani!
  Sifa za mwanamke asiyekupenda
  sifa za mwanamme anayekupenda

  so kind of u, nikisema ntaonekana feminist
   
 3. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,052
  Likes Received: 3,083
  Trophy Points: 280
  Love is nature and we men (people) hav variations...a pyscologist can differ with me in perceptions though we can both succeed in love affairs as well...
   
 4. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  1.Umetaja sifa tumezisikia, je kama asipooma na kula chakula cha usiku haina shida sivyo?

  2.Wanawake wengi siku hizi wameweka pesa mbele, je kama mimi sina pesa za kumpa mpenzi wangu ni kigezo kuwa simpendi?

  Nawasilisha
   
 5. chriss brown

  chriss brown JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pesa haijatajwa hapo mkuu,soma vizuri,mapenz siyo pesa.kaa ukilijua hilo.
   
 6. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Huo utafiki ni wa Marekani. Kibongobongo mwanamke ukimfanyia hayo anakupanda kichwani. Huku ni mwendo wa makofi.
   
 7. sister

  sister JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,027
  Likes Received: 3,933
  Trophy Points: 280
  huyo atakuwa limbukeni wa mapenzi
   
 8. Baba Erick

  Baba Erick JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ni kamba mpya au?
   
Loading...