Sifa za mwanaume anayekupenda

Sifa za mwanaume anayekupenda

Na sifa za mwanamke anayekupenda ni zipi?
Maana mimi naona 90%wote wana matatizo mala tu mahusiano yanapoanza
HAkuombi hela masaa yote hela labda akabwe nashida ipo kooni.
Ndio atasema atakupa mawazo chanya ambayo yatakujenga wewe.
Atakujali kwa kidogo alichonacho .
Atakupenda kwa moyo wote lazima akujulie hali na kukudhamini utakuwa mtu special kwake mkiwa pamoja atakuwa mtu mwenyewe furaha na atapenda kukusikiliza .
 
Asante kwa kunifungua,,basi mm naona safari yangu bado sana,
Maana kila ninae kutana nae ni matatizo tu mpaka najiuliza kabla aliishije?
 
Baada ya kumuacha jamaa. Hapo upo kwenye harakati za kutafuta unayempenda, miaka inaenda kila unayempenda anakula mzigo, anasepa. Hapo ndipo huwa mnakumbuka shuka wakati pameshakucha. Unaanza tena kumsumbua jamaa aliyekupenda wakati wewe hukumpenda, tena kipindi hiki unaonesha mahaba niue na jamaa hana feeling tena na wewe. Anabandua kama kawaida yetu. Kisha anatoa pasi kwa wengine nao wapambane
hahahahah ndo khali khalisi ya maisha mkuu. Itabidi tuendelee kuwabandua wale tulio wapendaga mwanzo alafu wakazinguaaa
 
Sifa pekee ya mwanaume anayekupenda ni huwa hachoki kukugonga na huwa hachoki kukumwagia manemane.
 
Hizi zote ndo nazifanya Kwa huyu shost,wakati mwingine anakuwa excited vile nafanya.Naomba Mungu anifikishe salama hii Safar
 
MIPANGO
Mwanaume anayekupenda atakushirikisha kwenye mipango yake hasa ya muda mrefu. Mfano akitaka kununua kiwanja, kujenga nyumba atakuambia na pengine kutaka mchango wako wa hali na mali katika kulifanikisha hilo. Ukiona mwanaume anakuficha mambo yake, tambua kuwa huyo ana walakini kwenye penzi la dhati na la muda mrefu.

ATAONESHA HUZUNI
Katika maisha ya mapenzi kuna wakati wa kuhuzunika. Mwanaume mwenye upendo wa dhati atashirikiana nawe wakati wa huzuni na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unapata furaha.

ATAKUAMINI
Dalili nyingine ya kupendwa na mwanaume ni kuaminiwa kwenye maisha kwa ujumla. Yaani mwanaume anayekupenda hatakuficha kitu, mfano pesa zake, atakupa uhuru kwenye simu yake na kukuamini katika usimamizi wa miradi yake.

ATAKUPA NAFASI
Ninapozungumzia nafasi nina maana atakukaribisha kwake bila hofu na kukupa nafasi ya kuingia na kutoka bila mipaka, atakupa nafasi ya kuweka vitu vyako kwenye kabati na kuruhusu nguo, picha na vitu vyako kuonekana wakati wote chumbani kwake.

UTAKUWA MWANAFAMILIA
Mwanaume aliyefikia chaguo la mwisho kwa mwanamke humshirikisha mpenzi wake kwenye masuala yake ya kifamilia, mfano atamwalika kwenye vikao vya harusi, kipaimara, atatoa nafasi ya kuambatana naye kuona wagonjwa, kusalimia ndugu na atakuwa huru kukutambulisha kwao.

ATAZUNGUMZA NAWE KUHUSU WATOTO
Kwa kuwa wanaume wengi hufikiria kuwa na familia, mwanaume anayekupenda atazungumza nawe mipango ya kupata watoto kwa kuwa atakuwa amekuchagua wewe kuwa mama wa wanaye na atapenda mazungumzo hayo.

ATAKUSAIDIA
Kwa kuwa kukwama ni sehemu ya maisha yetu, mwanaume anayekupenda atakuwa tayari kukusaidia unapokwama. Kila mara atahakikisha kuwa unakuwa na mafanikio na yeye atakuwa tayari kukupunguzia usumbufu wa maisha, kwa kukufuata kazini, kukusaidia baadhi ya mambo na hata ya nyumbani.

ATAJITOLEA
Ninaposema kujitolea ninamaanisha atakuwa tayari kufanya mambo yako na kuyaweka yake nyuma. Kwa mfano akiwa anapenda mpira na siku hiyo kuna mechi, lakini muda huo ukamwambia akufuate kwa mjomba wako atakuwa tayari kuacha furaha yake na kukujali wewe. Huyu ni mwanaume anayekupenda kwa dhati.

ATAAMBATANA NAWE
Wapenzi wengi wasiokuwa na mapenzi ya dhati huona aibu kuambatana na wapenzi wao kwenye mikusanyiko ya watu, lakini mwanaume anayekupenda atafurahia kutoka moyoni kuongozana nawe kwenye halaiki ya watu na kufurahia uwepo wako bila kuona aibu.

Mada hii inaishia hapa, hebu jiulize mwanadada, huyo uliyenaye anakufanyia haya, kama sivyo kwa kiwango kikubwa utakuwa na kazi ya kuhakiki penzi lako na pengine kujenga misingi mipya ya uhusiano wenu kabla haujavunjika.

NB: "Sihusiki juu ya penzi lolote lililovunjika baada ya kugundua kuwa mpenzi wako hana hata sifa moja kati ya hizo 10 hapo juu"
Bull shit *****

Nyie wadada you expect tuwapende tuwajali ata zaidi ya tunavojijali na kujipenda sisi,

An mnatamani hata upendo tnaowapenda nao ndugu zetu wa damu tuhamishie kwenu tuwapende nyie tu & bado mnatusalitu in return,

Most of you ndo mpo ivo, very selfish, roho mbaya, hamtaki kufanya kazi, mwanaume akikwama kdogo tu mnarecruit michepuko on the spot!

Ani nyie target yenu kubwa ni kutunyonya, sio ktusaidia kupiga hatua. You expect more benefit from us, as if you are comodities.

KUTOKA MOYONI NAICHUKIA SANA HII HALI, NAICHUKIA SANA.
 
MIPANGO
Mwanaume anayekupenda atakushirikisha kwenye mipango yake hasa ya muda mrefu. Mfano akitaka kununua kiwanja, kujenga nyumba atakuambia na pengine kutaka mchango wako wa hali na mali katika kulifanikisha hilo. Ukiona mwanaume anakuficha mambo yake, tambua kuwa huyo ana walakini kwenye penzi la dhati na la muda mrefu.

ATAONESHA HUZUNI
Katika maisha ya mapenzi kuna wakati wa kuhuzunika. Mwanaume mwenye upendo wa dhati atashirikiana nawe wakati wa huzuni na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unapata furaha.

ATAKUAMINI
Dalili nyingine ya kupendwa na mwanaume ni kuaminiwa kwenye maisha kwa ujumla. Yaani mwanaume anayekupenda hatakuficha kitu, mfano pesa zake, atakupa uhuru kwenye simu yake na kukuamini katika usimamizi wa miradi yake.

ATAKUPA NAFASI
Ninapozungumzia nafasi nina maana atakukaribisha kwake bila hofu na kukupa nafasi ya kuingia na kutoka bila mipaka, atakupa nafasi ya kuweka vitu vyako kwenye kabati na kuruhusu nguo, picha na vitu vyako kuonekana wakati wote chumbani kwake.

UTAKUWA MWANAFAMILIA
Mwanaume aliyefikia chaguo la mwisho kwa mwanamke humshirikisha mpenzi wake kwenye masuala yake ya kifamilia, mfano atamwalika kwenye vikao vya harusi, kipaimara, atatoa nafasi ya kuambatana naye kuona wagonjwa, kusalimia ndugu na atakuwa huru kukutambulisha kwao.

ATAZUNGUMZA NAWE KUHUSU WATOTO
Kwa kuwa wanaume wengi hufikiria kuwa na familia, mwanaume anayekupenda atazungumza nawe mipango ya kupata watoto kwa kuwa atakuwa amekuchagua wewe kuwa mama wa wanaye na atapenda mazungumzo hayo.

ATAKUSAIDIA
Kwa kuwa kukwama ni sehemu ya maisha yetu, mwanaume anayekupenda atakuwa tayari kukusaidia unapokwama. Kila mara atahakikisha kuwa unakuwa na mafanikio na yeye atakuwa tayari kukupunguzia usumbufu wa maisha, kwa kukufuata kazini, kukusaidia baadhi ya mambo na hata ya nyumbani.

ATAJITOLEA
Ninaposema kujitolea ninamaanisha atakuwa tayari kufanya mambo yako na kuyaweka yake nyuma. Kwa mfano akiwa anapenda mpira na siku hiyo kuna mechi, lakini muda huo ukamwambia akufuate kwa mjomba wako atakuwa tayari kuacha furaha yake na kukujali wewe. Huyu ni mwanaume anayekupenda kwa dhati.

ATAAMBATANA NAWE
Wapenzi wengi wasiokuwa na mapenzi ya dhati huona aibu kuambatana na wapenzi wao kwenye mikusanyiko ya watu, lakini mwanaume anayekupenda atafurahia kutoka moyoni kuongozana nawe kwenye halaiki ya watu na kufurahia uwepo wako bila kuona aibu.

Mada hii inaishia hapa, hebu jiulize mwanadada, huyo uliyenaye anakufanyia haya, kama sivyo kwa kiwango kikubwa utakuwa na kazi ya kuhakiki penzi lako na pengine kujenga misingi mipya ya uhusiano wenu kabla haujavunjika.

NB: "Sihusiki juu ya penzi lolote lililovunjika baada ya kugundua kuwa mpenzi wako hana hata sifa moja kati ya hizo 10 hapo juu"
Napinga hoja huwezi kumwamini mwanamke if humuoa au kumposa
 
Back
Top Bottom