Sifa za mwanaume anayekupenda

Sifa za mwanaume anayekupenda

Joined
Sep 25, 2018
Posts
53
Reaction score
134
MIPANGO
Mwanaume anayekupenda atakushirikisha kwenye mipango yake hasa ya muda mrefu. Mfano akitaka kununua kiwanja, kujenga nyumba atakuambia na pengine kutaka mchango wako wa hali na mali katika kulifanikisha hilo. Ukiona mwanaume anakuficha mambo yake, tambua kuwa huyo ana walakini kwenye penzi la dhati na la muda mrefu.

ATAONESHA HUZUNI
Katika maisha ya mapenzi kuna wakati wa kuhuzunika. Mwanaume mwenye upendo wa dhati atashirikiana nawe wakati wa huzuni na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unapata furaha.

ATAKUAMINI
Dalili nyingine ya kupendwa na mwanaume ni kuaminiwa kwenye maisha kwa ujumla. Yaani mwanaume anayekupenda hatakuficha kitu, mfano pesa zake, atakupa uhuru kwenye simu yake na kukuamini katika usimamizi wa miradi yake.

ATAKUPA NAFASI
Ninapozungumzia nafasi nina maana atakukaribisha kwake bila hofu na kukupa nafasi ya kuingia na kutoka bila mipaka, atakupa nafasi ya kuweka vitu vyako kwenye kabati na kuruhusu nguo, picha na vitu vyako kuonekana wakati wote chumbani kwake.

UTAKUWA MWANAFAMILIA
Mwanaume aliyefikia chaguo la mwisho kwa mwanamke humshirikisha mpenzi wake kwenye masuala yake ya kifamilia, mfano atamwalika kwenye vikao vya harusi, kipaimara, atatoa nafasi ya kuambatana naye kuona wagonjwa, kusalimia ndugu na atakuwa huru kukutambulisha kwao.

ATAZUNGUMZA NAWE KUHUSU WATOTO
Kwa kuwa wanaume wengi hufikiria kuwa na familia, mwanaume anayekupenda atazungumza nawe mipango ya kupata watoto kwa kuwa atakuwa amekuchagua wewe kuwa mama wa wanaye na atapenda mazungumzo hayo.

ATAKUSAIDIA
Kwa kuwa kukwama ni sehemu ya maisha yetu, mwanaume anayekupenda atakuwa tayari kukusaidia unapokwama. Kila mara atahakikisha kuwa unakuwa na mafanikio na yeye atakuwa tayari kukupunguzia usumbufu wa maisha, kwa kukufuata kazini, kukusaidia baadhi ya mambo na hata ya nyumbani.

ATAJITOLEA
Ninaposema kujitolea ninamaanisha atakuwa tayari kufanya mambo yako na kuyaweka yake nyuma. Kwa mfano akiwa anapenda mpira na siku hiyo kuna mechi, lakini muda huo ukamwambia akufuate kwa mjomba wako atakuwa tayari kuacha furaha yake na kukujali wewe. Huyu ni mwanaume anayekupenda kwa dhati.

ATAAMBATANA NAWE
Wapenzi wengi wasiokuwa na mapenzi ya dhati huona aibu kuambatana na wapenzi wao kwenye mikusanyiko ya watu, lakini mwanaume anayekupenda atafurahia kutoka moyoni kuongozana nawe kwenye halaiki ya watu na kufurahia uwepo wako bila kuona aibu.

Mada hii inaishia hapa, hebu jiulize mwanadada, huyo uliyenaye anakufanyia haya, kama sivyo kwa kiwango kikubwa utakuwa na kazi ya kuhakiki penzi lako na pengine kujenga misingi mipya ya uhusiano wenu kabla haujavunjika.

NB: "Sihusiki juu ya penzi lolote lililovunjika baada ya kugundua kuwa mpenzi wako hana hata sifa moja kati ya hizo 10 hapo juu"
 
Naunga mkono hoja.hii nayo ni katiba ya mahusiano..well said...ni mwendo wa kupimia tu..vigezo hivyo...
 
Kwa mujibu wa maendeleo ya maisha ya binadamu mapenzi (kupendana) si kipaumbele tena kama ilivyokuwa miaka iliyopita. Huwa nawashauri sana mabinti zangu kukazania kuweka bidii ili waweze kumudu maisha yao kwa kujitegemea wenyewe badala ya kutegemea wanaume maana mifumo ya maisha inabadilika kwa kasi ya hatari


Nchi kama Japan ndoa si kipaumbele kabisa kwa miaka hii ya leo, kila mmoja anapambania maisha yake
 
Exactly.Nitayafanya hayo yote siku nikimpata mke.

Natafuta mke wa kumfanyia hayo.
 
Na sifa za mwanamke anayekupenda ni zipi?
Maana mimi naona 90%wote wana matatizo mala tu mahusiano yanapoanza
 
Hutujui wanaume naweza nikaigiza yote hayo shida nipate papuchi

Watu tunaigiza hadi kuoka tunaenda kanisani kwako ili mradi tufunue tusepe wengine tunatoa kifunga uchumba cha kuzugia kabisa cha msingi omba mungu umpate mkweli
 
Umeongea points za maana kabisa ila sijajua unawaongelea wanawake wa nchi gani!

Hapa Bongo ukifanya hayo yote utaishia kuumizwa tu.
 
hapo kwenye nafasi ya kuweka vitu vidogo vidogo kama nguo ,,
hio ndio staili mpya ya kuhamia......
 
Nashukuru Mungu nilie nae vyote ivyo anatimiza....
 
Kupata kitu Lazma utoe kituu..

Je nyinyi mnatoa nn in return..??!!
Au mnataka one way tuuu
 
Back
Top Bottom