Sifa za Mwanamke na familia bora

chrischagama

Member
Apr 26, 2020
7
8
Kwa watu wanasema ndoa ni kama ngome iliyotekwa waliomo ndani wanatamani kutoka lkn waliokuwa nje wanatamani kuingia.

Labda nikuambie kitu ndoa ni tamu sana ikipata mwanamke mwenye hekima na mwanaume mwenye akili."kila mwanamke mwenye hekima hujenga nyumba yake lakin aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe"(mithali 14:1)kumbe ndoa ni mwanamke akitaka itakuwepo asipotaka haitakuwepo.So wanaume tuwe makini na wanawake tunaowaoa.Ndo kwanza nachomekea tu...tuendelee

1) Mwanamke bora hatakiwi kumlinganisha mumewe na mwanaume wake wa zamani. Akifanya hivyo ni sawa na kumdhalilisha tu maana huyo mwanaume wake wa zamani kashaachana nae hivyo hata na yeye ataachwa tu.

2) Mwanamke bora hakikisha usimruhusu yeyote kumuhudumia mumeo wakati wewe ukiwa nyumban, ndo màana mwanaume alikuoa so ni jukumu lako hata rafiki zako usiruhus wafanye hivyo.

3) Mwanamke bora hatakiwi kuwa na matumizi ya ovyo,ishi kulingana na urefu wa kamba ya mumeo.Kumbuka kutafuta si kutafutana. Usimtafute mumeo kwa matumizi yasiyo ya lazima heshimu jasho lake na utajionea upendo Mara dufu.

4) Mwanamke bora hutimiza hitaji la mumewe kwa kutomnyima tendo la ndoa. Unajua sisi wanaume kisayansi muda mwingi tunaliwaza hilo tendo so ukimnyima wewe itamlazimu akalitafute kokote kule.Kumbuka mumeo sio tohashi.

5) Wazazi na familia yako hawana maamuzi juu ya ndoa yako. Kama ukitaka kuwasaidia ndugu zako wasaidie hukohuko walipo maana wakati mwingine sio kila mwanafamilia anakutakia jema si unawajua mawifi.

6) Mwanamke usiwe na haraka kuondoka kujipamba.Unajua wewe ni ua kwa mwanaume wako hujui mumeo anakutana na wanawake wangapi waliojipamba na wakapambika hivyo jiweke vizur ili mumeo akupende haswaaaa!

7) Unapozungumza na mumeo hakikisha unaacha mambo mengine na kumsikiliza yeye wakati wote si unajua ukifanya hivyo mumeo atajua unamjali na wewe ni mke msikivu.So hata simu zima wakati huo ni wakujenga mambo.

8) Pia kuwa makin na maakuli unayompa mumeo. Sisi wanaume bana twapenda kula sana hivyo hakikisha unampikia msosi mzur na apendezwe nao kila siku.Upendo hapo lazma uzidi.

9) Usifichue udhaifu wa mumeo kwa familia yako ama rafiki zako,utaharibu. Pia hata mnapozozana kidogo hakikisha sio hadharani.

10) Pia mpende Mungu wako si unajua Mungu wetu ni mwenye wivu, shauri lako. Asanten wapendwa wote na mbarikiwe na mjenge familia zilizo bora mpaka mshangae wenyewe.
 
Wenye hizo sifa tajwa hapo katika Uzi wako ..... Wengi walisha kufa katika WW2 ...amebakia 1 tu ambaye ni Mke wangu
 
Back
Top Bottom