Sifa za mtu anayefaa kuwa kiongozi

Sifa za mtu anayefaa kuwa kiongozi

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,027
Reaction score
20,413
ZIJUE SIFA ZA MTU AFAAYE KUWA KIONGOZI

Yeyote anaweza kuwa kiongozi lakini si Kila mtu anaweza kuwa kiongozi Bora, Bali washikaji wengi wamekuwa Viongozi kwa kulindwa na mifumo tu hata Kama wamekosa sifa kabisa.

Kalamu ya Mwana wa kasomi, kwa tafakuri ya kina inabainisha hapa sifa za Mtu kuwa kiongozi Bora ambazo akiwanazo anaweza kuwa kiongozi bora sana nazo Ni hizi zifiatazo;

1. AWE NA UWEZO
Sifa kuu ya mtu kuwa kiongozi Bora ni kuwa na uwezo wa kuyatenda kwa weledi yale yanayoihusu nafai anayoiendea, hii tunamaanisha uwezo wa kiakili n akimwili yaani ,awe na afya njema ya mwili na afya ya ubongo. Mtu asiye na uwezo wa kumudu majukumu na mikikimikiki ya nafasi yake hafai hata kidogo kuwa kiongozi wa nafasi hiyo.

2. AWE MKWELI
Ukweli Ni sifa muhimu Sana kwa mtu kuwa kiongozi Bora, awe mtu anayezungumza na kutenda yale ambayo akili yake inayaamini kuwa ndio ukweli na ayatende kadiri ya uwezo wake wote. Mtu yeyote ambaye ukweli umemtoka, mnafiki anayehadaa watu huku ameficha agenda anazojua yeye hafai na ni hatari kumwacha katika ofisi za umma.

3. ASIWE NA NDIMI MBILI
Msimamo na unyoofu wa maamzi na matendo Ni sifa muhimu Sana kwa mtu kuwa kiongozi Bora na akaleta tija, hakuna Jambo linavunja heshima ya mwanasiasa ama kiongozi wa taasisi yoyote kama kusema hiki leo n kesho kusema tofauti na hicho huku mitandao na akili za watu Bado zinakumbuka matamko yake ya awali. Mtu yeyote kigeugeu anayepeperuka Kama bendera kwa kutamka tamka tu na kugekia huku na kule Ni hatari Sana na jamii inao wajibu wa kumkana kwa vitendo kwa kupinga unafiki wake hadharani.

4. ASIZOELEE ULEVI
Kiongozi Bora ni mtu ambaye anapaswa kutokuwa wa kulewa na Mambo yote Kama vile kulewa madaraka, kulewa vilevi Kama pombe na madawa ya kulevya, asilewe umalaya nk. Mambo haya huondoa heshima kwa mtu huyo na huathiri uwezo wake wa kufanya maamzi sahihi na yenye maadili. Msela mlevi wa madaraka, anayetukana na kuumiza watu, anakanyaga katiba na kuongoza taasisi kwa utashi wa matakwa yake binafsi hasi hata kidogo kumiliki ofisi ya umma ama ya taasisi kwani athari zake Ni kubwa.

5. ASIYAENDEE MAPATO YA AIBU
Kiongozi Bora anapaswa kuwa mtu anayeyachukia MAPATO ya aibu anayopewa kwa mgongo wa uovu, rushwa, vyeo vya kupeana kishikaji na kuumiza wengine, ufisadi, kujinufaisha na Mali za umma kwa maslahi binafsi, Kula njama na kujivisha ukuu na heshima isiyoendana na uhalisia, kujiwekea Kinga nyingi dhidi ya taratibu za kuajibishwa ili Mambo yake yawe huru hata Kama atatenda tofauti. Mtu asiyeona haya kusimama mbele ya watu na kujiita mtetea wanyonge huku anawaumiza, asiyeona Soni kupokea rushwa kutoka kwa beberu na kuwafukuza wananchi kwa kubomoa nyumba zao ili beberu aliyemhonga afanya biashara zake, mtu asiyeona haya kutumia ofisi ya umma kwa maslahi yake binafsi Ni kama Simba aliyekabidhiwa kulinda mbuzi huku akiwafanya kuwa chakula chake ili aendelee kuishi awalinde wasidhurike.

Baada ya Tafakuri nzito hii ya Mwana wa Kasomi, unadhani wewe mwenye mamlaka uko sawasawa kuwepo hapo kutokana na matendo yako? Kama jibu Ni siyo badilika na Kama huwezi achia ngazi, je wewe unayetamani kuwa kiongozi umeona mapungufu yako? Jisahihishe ungali katika maandalizi, Bali wale WASIO na hizi sifa na wangali mamlakani wanapaswa kukosolewa na kulazimishwa kujirekebisha kwa maslahi ya jamii zetu, Tafakuri jenzi na ndivyo.
 
Hiyo namba 3 inamhusu kabisa Prof. Ndalichako! Wakati wa Magufuli aliunga mkono kuanzishwa kwa somo la Historia! Baada ya kifo chake, na yeye akabadili gia angani kama walivyofanya wanafiki wenzake akina Kigwangala, nk.

Na hiyo namba 2, inamhusu kabisa Rc Antony Mtaka baada tu ya kumpiga ngumi za uso Prof. Ndalichako kupitia matamshi yake.
 
Hiyo namba 3 inamhusu kabisa Prof. Ndalichako! Wakati wa Magufuli aliunga mkono kuanzishwa kwa somo la Historia! Baada ya kifo chake, na yeye akabadili gia angani kama walivyofanya wanafiki wenzake akina Kigwangala, Msukuma, nk.
Huyu bibi kimsingi hafai kabisa kuwa Waziri ni mtu wa hovyo sn
 
Kwa Tanzania lazima uwe mwizi wa hela za uma, uwe mwongo, uwe na benki account nje ya nchi, ujali familia yako tu, tumia hovyo Mali za uma eg geuza bombardier liwe presidential jet.

Ujue kuua wenzako Kama wakuchelewesha kula mali za uma, jifanye mcha mungu kweli kweli.
 
Hiyo namba 3 inamhusu kabisa Prof. Ndalichako! Wakati wa Magufuli aliunga mkono kuanzishwa kwa somo la Historia! Baada ya kifo chake, na yeye akabadili gia angani kama walivyofanya wanafiki wenzake akina Kigwangala, nk.

Na hiyo namba 2, inamhusu kabisa Rc Antony Mtaka baada tu ya kumpiga ngumi za uso Prof. Ndalichako kupitia matamshi yake.
Ndo viongozi wetu wa kibongo walivyo.
 
Hapo kwenye ndimi mbili ndio hasara kubwa Taifa hili lililoipata kipindi hiki. Jambo hili linahitaji maombi ya nguvu ili tuvuke.
 
Kiongozi anatakiwa awe na sifa ambazo mtu wa kawaida naatakiwa awe nazo.

Mtu wa kawaida hatakiwi kuwa muongo basi ndivyo kiongozi hatakiwi nae.

Mtu wa kawaifa hatakiwi kuwa mla rushwa basi na kiongozi hatakiwi pia.

Mtu wa kawaida hatakiwi kuwa kigeugeu basi kiongozi nae pia hatakiwi.

Mtu wa kawaida hatakiwi kuwa kiburi basi kiongozi nae hatakiwi pia.

Maana yangu ni kwamba viongozi wanatakiwa waandaliwe na tabia hizi tokea watoto wakue nazo ili hizi tabia zikite katika mishipa ya damu zao yawe ndo maisha yao na isiwe maigizo.

Mkianza kugawa sifa za kiungozi na sifa fulani basi mnaanza kupuuza malezi ya utotoni mpaka ujanani.

Kila sifa hapo ianzie utotoni alikolelewa bila hivyo hakuna tija itakayopatikana katu.
 
Ndio maana kuna nchi kiongozi anaandaliwa toka akiwa mtoto
 
Sifa za kuona sifa za anayetakiwa kuwa kiongozi bora, Mwandishi hana hiyo sifa, Orodhesho la sifa zinazomfaa kiongozi bora kwa mjibu wa chapisho hili, tatizo ni kwamba, ukweli huwa haupendwi, zimeandikwa sifa za kawaida saaana,

Sifa mhimu sana na ya kawaida nayo imesahaulika, kiongozi mwenye macho ya tai, mwenye kuona mwanzo wa tatizo na mwisho wake pia
 
Asante mkuu kwa nyongeza
 
Hiyo namba 3 inamhusu kabisa Prof. Ndalichako! Wakati wa Magufuli aliunga mkono kuanzishwa kwa somo la Historia! Baada ya kifo chake, na yeye akabadili gia angani kama walivyofanya wanafiki wenzake akina Kigwangala, nk.

Na hiyo namba 2, inamhusu kabisa Rc Antony Mtaka baada tu ya kumpiga ngumi za uso Prof. Ndalichako kupitia matamshi yake.
1. Ndungai
2. Kabudi
3. Dr Gwajima
4....
5....
 
1. AWE MCHA MUNGU
2. AWE NA UWEZO
3. AWE MKWELI
4. ASIWE NA NDIMI MBILI
..........................

............................
.........................
 
Back
Top Bottom