Sifa za mke nimtakae (Shairi)

Sifa za mke nimtakae (Shairi)

Mie kukuchezea rafu,ubavu huo ntatoa wapi
hapa nilipo nipo dhohofu,kukuwaza kila wakati
Njoo kwangu asali,useme nikupeleke wapi
najitahidi kila hali,uweze kunikumbuka kila wakati

Usiniambie unaanza kunidanganya asubuhi hii.Babu Asprin uliniona wa nini mwenzako namdhoofisha.😀
 
Last edited by a moderator:
Hakika nimekusoma, Ufafanuzi murua,
Fikira zilinihama, nikajua watania,
Mawazo yalishazama, lugha sikuitambua,
Utapata wa kuoa, Mola kishakupangia.

Mola kishakupangia, Utapata wa kuoa,
Wala hautojutia, Raha utajipatia,
Naye atawajalia, bora yenu familia
Utapata wa kuoa, Mola kishakupangia.

Amina amina sana, nasema tena amina,
Amina tena na tena, Tena na tena amina,
Tena nasema amina, Amina ilo amina,
Utapata wa kuoa, Mola kishakupangia.

ODM

Niliomba mwaka jana, ila sasa nishaoa.
Ninamiliki kimwana, toto la kitanzanzania.
Anayo shepu mwanana, kitabia katulia.
Sikupata asosoma, msomi nimemkwaa.

Nyumbani nikimuona, nasahau kutembea.
Maisha yawa mwanana, dodo langu najilia.
Twamuomba maulana, watoto kutupatia.
Sikupata asosoma, msomi nimemkwaa.

By Sauti ya nyikani.
 
Hahaha nacheka sana, Nacheka mimi hahaha,
Umenipata kwa kina, wacha nicheke hahaha,
Sikukupata upana, hahahaha hahahaha,
Hongera kwa kuopoa, kimwanacho maridhawa.

Ila chonde angalia, wakware wengi mjini,
Kazi yao kuvizia, vizuri vilivyo ndani,
Usije hapa kulia, Wamekupora mwandani,
Hongera kwa kuopoa, kimwanacho maridhawa.
 
Najikutaga tu napenda kukukoti.

Napenda ukinikoti,na napenda ukipenda kunikoti..
endekea kunikoti,na usichoke kupenda kunikoti
Amini unanivika koti,kwa kupenda kunikoti..
ntajitahidi nikuvishe koti,ili usiache kunikoti ...
 
Heeeee!!!!!!!!! safi sana, mke hutafutwa kwa nyimbo, huolewa kwa nyimbo na vigelegele na hubembelezwa kwa nyimbo.
 
Hahaha nacheka sana, Nacheka mimi hahaha,
Umenipata kwa kina, wacha nicheke hahaha,
Sikukupata upana, hahahaha hahahaha,
Hongera kwa kuopoa, kimwanacho maridhawa.

Ila chonde angalia, wakware wengi mjini,
Kazi yao kuvizia, vizuri vilivyo ndani,
Usije hapa kulia, Wamekupora mwandani,
Hongera kwa kuopoa, kimwanacho maridhawa.

Hahahahaaa.
Nimekuelewa sana, sitofanya masikhara. Nitamganda kimwana, wasije wakanipora. Nitamtunza kichuna, ili azidi kung'ara. Nashukuru kuopoa, mrembo maridhawa.
 
Hahahahaaa.
Nimekuelewa sana, sitofanya masikhara. Nitamganda kimwana, wasije wakanipora. Nitamtunza kichuna, ili azidi kung'ara. Nashukuru kuopoa, mrembo maridhawa.

Kumjali zingatia, kumlinda kazi yako,
Asijepata kulia, ukimchapa viboko,
Kwako atang'ang'ania, ukimpa penzi lako
Ukimpenda kwa dhati, mkeo atakutii

cc wake wa ujana wangu BADILI TABIA, cacico, Kongosho
bcc shem snowhite, hommie Kaizer
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom