Sifa za mke nimtakae (Shairi)

Sifa za mke nimtakae (Shairi)

Joined
Jan 24, 2015
Posts
29
Reaction score
20
NATAKA KUOA:

Naogopa majaribu, kuoa nimenuia.
Kwa kukwepa maswahibu, yaliopo kwenye ndoa.
Nimepanga taratibu, sifa za anae faa.
Natafuta wa kuoa, mdada alo na sifa.

Namtafuta bubu, awe na kiziwi pia.
Huyu huwa hana gubu, hatosikiza umbea.
Nitaziepuka tabu, tutadumu kwenye ndoa.
Natafuta wa kuoa, mdada alo na sifa.

Vipofu wataratibu, namba mbili wafatia.
Huwa hawana ghadhabu, nyumbani wanatulia.
Hawaoni vya ajabu, tamaa zawakimbia.
Natafuta wa kuoa, mdada alo na sifa.

Walemavu nao jibu, namba tatu napatia.
Wao wastaarabu, upendo umewajaa.
Bubu nilomuhesabu, nikikosa nitaoa.
Natafuta wa kuoa, mdada alo na sifa.

Wasomi sitojaribu, sitaki kuwasikia.
Mara kukesha clabu, nyumbani tamthilia.
Yes no kwangu tabu, la tano nimeishia.
Natafuta wa kuoa, mdada alo na sifa.

Wa Forum ni adhabu, upweke naukataa.
Achati na Nyani Gabu, chit chat akeshea.
Nisije kupata gubu, peke yangu kuongea.
Natafuta wa kuoa, mdada alo na sifa.

By. Sauti ya nyikani.
 
shair safi kabisa!!!
wanakuja wenye hizo sifa

Nilipo mtaja bubu, si kwamba hawezi sema.
Ila ni mtaratibu, haneni kwa kulalama.
Ni mke mwenye adabu, anamuhofu kalima.
Natafuta wa kuoa, mdada alo na sifa.

Kipofu namaanisha, hatotazama wenzangu.
Mimi peke namtosha, ahahi na ulimwengu.
Sote twapanga maisha, kwa kutanguliza Mungu.
Natafuta wa kuoa, mdada alo na sifa.

Nikisema mlemavu, si kwamba hatotembea.
Ila kwangu ka ubavu, anatunza familia.
Sio kokolo la nyavu, mitaani zoazoa.
Natafuta wa kuoa, mdada alo na sifa.
 
Heri ninakutakia, Kwa kuweka yako nia,
Mola atakujalia, Mke atakupatia,
Mwenye huba na tabia, Upendo tafurahia,
Utapata wa kuoa, Mungu ukimhusisha.

Mungu ukimhusisha, Utapata wa kuoa,
Hautapata garasha, utapata mwenye nia,
Ulemavu kuhusisha, Mungu unampangia?
Utapata wa kuoa, Mungu ukimhusisha.

Mwanamke wa kuoa, Si bidhaa ya dukani,
Kwamba unajitwalia, kwa tamaa ya machoni,
Hakika utajutia, utaumia moyoni
Utapata wa kuoa, Mungu ukimhusisha.

Na Babu ODM,
Kaunta ya Juu
Fesibuku Pub
Boko Basihaya
Dar Es Salaam
 
Ukitaka kuoa oa tu,acha kuchunguza kuku,
ukimpenda muoe,omba mungu akutunuku,
ndoa zina mengi,usidhani ni kula kuku
wanaofaa wako wengi,acha upukupuku.....
 
Nilipo mtaja bubu, si kwamba hawezi sema.
Ila ni mtaratibu, haneni kwa kulalama.
Ni mke mwenye adabu, anamuhofu kalima.
Natafuta wa kuoa, mdada alo na sifa.

Kipofu namaanisha, hatotazama wenzangu.
Mimi peke namtosha, ahahi na ulimwengu.
Sote twapanga maisha, kwa kutanguliza Mungu.
Natafuta wa kuoa, mdada alo na sifa.

Nikisema mlemavu, si kwamba hatotembea.
Ila kwangu ka ubavu, anatunza familia.
Sio kokolo la nyavu, mitaani zoazoa.
Natafuta wa kuoa, mdada alo na sifa.

Hakika nimekusoma, Ufafanuzi murua,
Fikira zilinihama, nikajua watania,
Mawazo yalishazama, lugha sikuitambua,
Utapata wa kuoa, Mola kishakupangia.

Mola kishakupangia, Utapata wa kuoa,
Wala hautojutia, Raha utajipatia,
Naye atawajalia, bora yenu familia
Utapata wa kuoa, Mola kishakupangia.

Amina amina sana, nasema tena amina,
Amina tena na tena, Tena na tena amina,
Tena nasema amina, Amina ilo amina,
Utapata wa kuoa, Mola kishakupangia.

ODM
 
Ukitaka kuoa oa tu,acha kuchunguza kuku,
ukimpenda muoe,omba mungu akutunuku,
ndoa zina mengi,usidhani ni kula kuku
wanaofaa wako wengi,acha upukupuku.....

Mbona unanichezea rafu wewe mwanaume? The Boss
 
Last edited by a moderator:
Asante but ya kwako yametimia hadi nimeshangaa
una kitu kuhusu mashahiri....kipaji kilichojificha hivi....
hongera sana..usiache kuendeleza kama hivi

Kama bia zitaniruhusu......

Afu mashairi hayalipi kiviiiile....

Maisha yametuchakachua, tunahangaikia njuruku tu. Vipaji vinapotea.
 
Kama bia zitaniruhusu......

Afu mashairi hayalipi kiviiiile....

Maisha yametuchakachua, tunahangaikia njuruku tu. Vipaji vinapotea.


Mdogomdogo kama hivi,kuwapa wajukuu urithi
tukiendeleza fani kama hivi,hata kukagua kwa urahisi..
na hiyo faida pia,sio bia tu na njuluku
washairi nao pia,wadada huwatunuku .....
 
Back
Top Bottom