KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 10,569
- 21,075
MKOA WETU UNAHITAJI WABUNGE WENYE SIFA HIZI KATIKA MAJIMBO YETU
1. Mbunge mwenye mpango kazi binafsi wa miaka mitano kama mbunge, siyo mbunge wa kujivunia miradi iliyotekelezwa na serikali pasipo yeye kubuni hata mradi mmoja ndani ya Jimbo.
2. Mbunge anayebeba hoja na mahitaji ya wananchi kabla ya kubeba chama chake. Ni lazima ajue anawakilisha wananchi, aelewe kuwa yeye siyo mwakilishi wa chama chake. Ajali wapiga kura.
3. Mbunge aliye tayari kutumia mfuko wa jimbo kutekeleza miradi yenye kuacha alama ya kudumu jimboni kwake, siyo kutumia mfuko wa jimbo kisaniii. Yaani asigawe pesa za mfuko wa Jimbo kama pipi ili kusaka kura za uchaguzi utakaokuwa unafuata.
4. Mbunge aliye tayari kutumia akili kubwa zilizo mtaani (kuna watu wana akili sana huko mitaani) kufanya mikakati ya kuleta maendeleo jimboni, siyo mbunge anayewaogopa watu mwenye akili na mawazo chanya na kuwaona tishio la ubunge wake.
5. Mbunge mwenye kujua changamoto za wananchi kwenye kata zetu zote, siyo mbunge wa kuambiwa kwa kusimuliwa changamoto za jimboni kwake.
6. Mbunge aliye tayari kutumia kipato anachokipata kuwekeza jimboni kwake ili kutengeneza fursa na ajira kwa vijana wa jimboni. Siyo mbunge wa kumaliza muda wake bila hata kufungua hata tu kamgahawa jimboni.
7. Mbunge aliye tayari kuwa mwananchi wa kawaida, siyo mbunge ambaye anadhani ubunge ni daraja la kuwa mtu "special" ambaye hapaswi kushirikiana na kuishi kama wananchi wengine .
8. Mbunge ambaye anafikiwa na makundi yote ya wananchi. Yaani afikike kirahisi na vijana, wazee, kina mama, wasomi na wasio wasomi. Tunahitaji Mbunge wa watu wote siyo mbunge wa kuogopwa kama mfalme.
9. Mbunge ambaye ni wa wanachama na wananchi, siyo mbunge kutoka mfukoni mwa viongozi wa chama. Mbunge lazima awe amepita michujo halali siyo kuletwa kibabe na wenye nguvu.
10. Mbunge ambaye ni mhamasishaji mzuri wa shughuli za maendeleo na za kijamii, siyo mbunge-boss yaani mbunge wa kukaa tu Dar es Salaam na Dodoma na kurudi likizo kutafuta wanaompinga na kumkosoa jimboni.
Soma pia: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025