Sifa 15 za kijana ambae hayuko tayari kuoa

ze jj

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2012
Posts
522
Reaction score
630
SIFA 15 ZA KIJANA AMBAYE HAJAKOMAA KWA AJILI YA NDOA
♨♨♨♨♨♨
1. Anaigiza maisha. Anataka kuonekana amefanikiwa kimaisha, hajui kuwa anajidanganya mwenyewe.

2. Hana mipango inayoeleweka, anajua kuzungumza lakini matendo ni sifuri, hajui kwamba kuanza mahusiano ni kubeba majukum.

3. Anataka ngono kabla ya ndoa, akipewa anasema binti hana hofu ya Mungu, asipopewa anatishia kuvunja mahusiano au anaanzisha mahusiano na msichana mwingine.

4. Ana wivu unaowaka kama moto wa nyika, anaweza kumkataza mchumba wake asiongee na mwanaume mwingine, au asifanye kazi kwa sababu boss wake anamtaka au kwa sababu anahisi kazi ile amepewa na 'mwanaume' .

5. Ana hasira mithili ya mbogo aliyechokozwa, anaweza kumpiga mpenzi wake au kumtukana. Ni katili, mdhalilishaji na anapenda kusikilizwa kwa kila amri atoayo.

6. Hajui lolote kuhusu Mungu, na hana muda wa kutafakari habari za Mungu.

7. Ni Tegemezi, anategemea wazazi au kupiga 'mizinga' kwa ndugu na marafiki ili kumudu mahitaji yake ya kila siku.

8. Si mtoaji kwa sababu hana kitu cha kutoa, ukimweleza shida yako hashindwi kukwambia we unapenda pesa, au anaweza kusema, 'Mi sio babako'

9. Anapowaza kuhusu ndoa anawaza ngono tu, hafikirii kuhusu majukumu ya kulea familia na mipango ya maendeleo ya familia.

10. Hajui kusifia, anachojua ni kukosoa tu. Anataka kupewa sifa zote hata ambazo hastahili.

11. Hujiona bora kuliko wengine na mara nyingi anapenda kushindana na watu bila sababu.

12. Anapenda maisha ya maonesho (show off) : anaweza kupiga picha kwenye gari ya rafiki yake akaandika status, my new ride, anaweza kutamani hata kuombea mkopo; akipanda ndege basi hawezi kuwa na story nyingine zaidi ya safari ya angani. Akipata fursa ya kupiga picha na mtu maarufu basi anadhani na yeye ni maarufu na anadhani mafanikio ya mtu yule yamehamia kwake.

13. Mvivu, hawazi juu ya kesho yake. Anaanza mradi na kuishia mwanzoni (sio njiani) kwa sababu lengo ni kuwanasa wanawake wapumbavu.

14. Anashinda online anachat, na anajua wazi hakuna biashara anayofanya mtandaoni. Mitandao ya kijamii imeteka maisha yake, haongezi tija wala maarifa ya msingi kwa maisha yake.

15. Anazijua sifa zote za wife material lakini hana sifa hata moja kuwa husband material.

[HASHTAG]#AMKA[/HASHTAG] KIJANA JITAMBUE#
 
SIFA 15 ZA KIJANA AMBAYE HAJAKOMAA KWA AJILI YA NDOA
[emoji621][emoji621][emoji621][emoji621][emoji621][emoji621]

Kweli kabisa
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2] duuh.
 
Umeyajuaje yote hayo kama na wewe sio mhusika wa kwanza..halafu usifosi watu wafanane, utofauti ndio radha ya dunia..
 
Ngoja watoke misa ya kwanza wanakuja.

Subiria apo hapo utawataka leo.
 
Huo si utafiti ila ni mtazamo wako wewe unaotokana na uzoefu wako kwa jamii unayoishi nayo.

Hatahivyo umegusa kundi kubwa la Vijana.

Mtu anaweza kuwa na maisha ya kuigiza ili apate wa kumuoa...lasivyo hataoa au atachelewa sana kuoa. Hii ilianza tangu zamani ambapo kijana wa zamani anaenda kwa rafiki yake na kuomba hata suti, viatu, baiskeli au saa tu ili akienda kwa baba mkwe aonekane ana nafuu ya maisha kisha anatorosha mwanamke na kuoa kabisa.

Wanawake hao ndio mama zetu wa leo.

Suala la kupiga mizinga kwa Wazazi au ndugu pia inategemea na sababu. Wengine ni kutokana na kukosa ajira ilihali ni wasomi na siku hizi hata vibarua tu mtaani hawapati. Hivyo bora apige mizinga mpaka mambo yatakapokaa sawa, kuliko akaibe, akajihusishe na haram ama akafanye dhuluma kwani huko atakufa.

Kujihusisha na mambo ya Mungu mfano Ibada, utoaji sadaka n.k ni NEEMA sio MAAMUZI (Wakristo walioshiba vizuri wanaelewa hili)

Pia hakuna guarantee kuwa mtu akioa hayafanyi hayo, Wapo waliooa ila wana sifa hizo.

All in All, tabia huwa zinabadilika ama zinabadilishwa. Mtu anaweza kuwa na tabia flani ila akioa anabadilika moja kwa moja.

Pole kwa hii risala.

Jumapili njema.
 
Umesema kweli, Nina ndg yangu yupo second year ana 23 uloandika hapo juu karibu yote yanamuhusu basi namuonea sana huruma sielewi ni balehe ama ni nini, jiandae kwa povu lkn
 
Kwa hali ilivyo vijana wengi wa kizazi cha dot.com ndio wapo hivyo. Instagram,facebook,snapchat kuuza sura na kuruka club kazi za kueleweka hakuna bas tafrani. Wengi wamejiajiri kwenye uzinzi yani kula cha mkongo na kukomesha wanawake huku wakiwabadili. Kutengeneza pesa hawawezi tena baada ya dili kufungiwa.
 
Back
Top Bottom