Siera Leone yatangaza hali ya dharura baada ya kuongezeka kwa vitendo vya ubakaji

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais wa Siera Leone, Julius Maada Bio ametangaza hali ya dharura ya taifa kwa sababu ya kuongezeka idadi kubwa ya ghasia za ubakaji na ngono nchini humo.

Rais Bio alisema mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya mashtaka ya manyanyaso ya ngono dhidi ya watoto atakabiliwa na kifungo cha maisha jela. Zaidi ya kesi 8,000 za awamu ya tatu zinazohusiana na manyanyaso ya kijinsia zilizoripotiwa nchini Siera Leone mwaka 2018 ziliwahusisha watoto.

Idadi kamili ya kesi inadhaniwa kuwa juu lakini mazungumzo kuhusu uhalifu wa ngono kwa jumla yamekuwa mwiko katika taifa hilo lililopo Afrika magharibi. Rais Bio wakati akitangaza hali ya dharura ya kitaifa alisema “Sisi kama taifa, lazima tusimame na kuelezea janga hili”.

Alieleza kwamba hospitali za serikali zitatoa huduma ya bure ya matibabu kwa waathirika wa ubakaji na unyanyasaji wa ngono. Katika kuongezea Bio alisema kitengo maalumu cha polisi kwa waathirika wa ubakaji na ghasia za ngono pamoja na mahakama maalumu zitaanzishwa kuharakisha kushughulikia kesi hizi.

VOASwahili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh Akili za Waafrika bhana wengne wana chinjana huko Njombe, wengne ndo hao wana bakana! HIVI SHIDA NI NINI AU NDO SHIDA UKISHAKUA NA NGOZI NYEUSI TU HADI AKILI INAKUA NYEUSI😒😒😢
 
Back
Top Bottom