kombaME
JF-Expert Member
- Aug 24, 2015
- 2,115
- 2,822
Habarini humu ndani,
Kwanza niweke wazi kuwa mimi ni mngoni, kabila la watu shupavu kutoka mkoani Ruvuma, humu ndani mara kibao nimesoma sisi wanaume wa mikoani kuwasema sana wanaume wa Dar kuwa ni mdebwedo tena tumejikita sana kwamba hawawezi kupiga show ya maana kwa kitanda na eti ni goi goi.
Nikaona kama vile sisi wa mikoani hatuna mantiki kwenye hili, yaani kwenye karne hii ya AIDS tunajisifia ngono? Tunajisifia kula ugali wa dona? So what? Tunajisifia minguvu ya kupigana, nikaona hizi ni sifa zisizo za msingi kabisa.
Baada ya kufanya utafiti kidogo nikapata haya;
1.Dar ni mji wenye kodi za juu sana kuliko mikoani lakini bado watu wa Dar wanaweza kumudu na kuwa na maendeleo kuliko sisi wa mikoani tunaolipa Tsh.20,000 kwa mwezi.
2.Wenzetu wa Dar watoto wao wanalipa nauli kila siku kwenda shule kuanzia shule ya msingi hadi sekondari lakini bado wanamudu gharama hizo wakati huku mikoani hakuna nauli watoto wetu wanashindwa kusoma kisa ukata.
3.Pamoja na Dar kuwepo watu maskini lakini huku mikoani hali ni mbaya maradufu pita vijijin uone.
4.Dar ni mji ambao kila wa mkoani au asilimia kubwa wanapenda kwenda tofauti na wao kupenda kuja kwetu.
5.Watu Dar wanazidi kuwa wengi kuliko kawaida kuliko sehemu yoyote, maana yake ni kuzuri ndio maana wanajazana.
6.Msanii yoyote lazima atapenda kuja Dar kwasababu ni sehemu pekee hata ukiwaambia kiingilio million moja watakuja (refer Zari white part) kiingilio kilikuwa hadi million 3 na bado tiketi ziliisha, pamoja na kodi kuwa juu. Sijui wanapata wapi hela hawa.
7.Matajiri wa nchi ukipanga wa kwanza hadi wa kumi naamini wote watakuwa wanafanya shughuli zao Dar.
8.Timu tatu bora katika nchi hi zinatoka Dar.
Kiujumla ni kwamba Dar wametuzidi sana sisi wa mikoani hili la kujisifia kula dona wao chipsi mayai ni kujifariji kwetu na halina maana yoyote katika kuinua maendeleo ya mikoa yetu, hebu tuangalie wenzetu wanafanyeje kupata maendeleo pamoja na changamoto za ughali wa maisha, yaani ukipita shule za msingi Dar utakuta gari zimepaki nje wakati huku kwetu mkoani hata ukienda shule za sekondari gari ni ya mkuu wa shule tu! Tujiulize tufanye maendeleo tuache majungu na wivu wenzetu wametuzidi sana.
NAWASILISHA!