Sidhani kama kuna kitu kizuri hapa duniani kama kumtumikia Mungu

Kabla ya kuja Mzungu na mwarabu ulikua unamjua huyo Mungu?
Mkuu dini inasambaa dunia nzima siku hadi siku.
Israeli kwa sisi Wakristo ndipo chimbuko la dini yetu.
Tumeletewa na wazungu "Wamissionary" hata ukienda latin america, wapi sehemu yeyoe duniani utaona mzungu kaplay major role kueneza ukristo/Christianity.
Yesu anasema tuieneze injili, tutangaze habari njema kwa watu wote.

Wenzetu waislamu wameletewa na waarabu chimbuko la uislamu ni maeneo hayo hayo ya middle east! dini inaenezwa ulimwengu mzima.
 
Mkuu ukikaa kwenye nchi mojawapo zilizorasimisha utawala wa shetani, hasa ulaya ambako wamesimika na chapa yake ya ushoga, ndo utahisi hali inavyokuwa ngumu kuishi eneo ambalo hakuna uwepo wa Mungu. Yale mahangaiko ya roho na nafsi na hata madhara unayoweza kuyapata katika mwili unakuwa unatamani uondoke mara moja. Ogopa laana ya kujiondoa katika kumtegemea Mungu.

Hamna nchi iliyorasimisha utawala wa shetani. Mungu ana watu wake kila mahali hata pale panapoonekana kuna ushetani Kwa asilimia kubwa ila Mungu yupo na uwepo wake Upo. Sijui wewe unazungumzia nchi gani hiyo?
 
Hahaha...wenye ufahamu wameshanipata
 
Mkuu ukikaa kwenye nchi mojawapo zilizorasimisha utawala wa shetani, hasa ulaya ambako wamesimika na chapa yake ya ushoga, ndo utahisi hali inavyokuwa ngumu kuishi eneo ambalo hakuna uwepo wa Mungu. Yale mahangaiko ya roho na nafsi na hata madhara unayoweza kuyapata katika mwili unakuwa unatamani uondoke mara moja. Ogopa laana ya kujiondoa katika kumtegemea Mungu.
Kukaa nchi za kimaskini ni laana tupu, mawazo yanakua ni kimaskini maskini tu
 
Unaogopa swali 😃😃😃, jibu tu labda nitapata huo ufahamu.
Biblia zimetapakaa kila kona, katafute maarifa humo. Jaribu kufuatilia mafundisho ya mwl. Mwakasege huwa anaongelea maswala mbalimbali ikiwemo laana inayoweza kuipata nchi na taifa
 
Guys sidhani kama kuna kitu kizuri hapa dunia kama kumtumikia MUNGU.
Vitu vyote vya hapa duniani vitapita lakini MUNGU atasimama milele.
Sasa wewe mwenzangu na mimi kwanini usiwekeze kwenye furaha ya milele?
Nani kama MUNGU?
Hakika hakuna.
Yote mtakayo muombeni atawapatieni kwake kuna utajiri wa kutosha tena wa bure usio wa gharama au kulipia.

Natumaini watu wenye akili kubwa watawekeza kwa ajili future na eternity.
Nothing else ni GOD pekee.
Kunafaida gani kuwa tajiri na ukakosa ufalme wa mbinguni sijui ni mathayo ngapi hile naupenda sana
 
Watu wengi wakisikia kumtumikia Mungu mawazo yao yanaenda kwa watumishi wanaosimama kwenye madhabahu kwa ajili ya kuhubiri wanasahau hata wao wanaweza kumtumikia Mungu katika nafasi walizonazo kama wakisimama katika haki, Bilbia inasema .Ufalme wa Mungu si kula na kunywa bali ni haki, amani, furaha katika Roho Mtakatifu WARUMI 14:17
Kwa hiyo kama upo kazini na ukasimamia haki katika kazi unayofanya tayari wewe ni mtumishi wa Mungu unaemwakilisha Mungu katika kazi au biashara yako na wengi watavutwa kwa matendo yako mema
Mstari wa 18 anamalizia kwa kusema 18Kwa kuwa yeye amtumikiae Kristo katika mambo hayo Humpendeza Mungu tena hukubaliwa na wanadamu
 
Kabla ya kuja Mzungu na mwarabu ulikua unamjua huyo Mungu?
Tunashuhudia si tu kile tulichosikia bali pia kile tulichoona. Babu zenu walikuwa na miungu yao iliwafaa nini? Mbona miungu yao haikuwasaidia wasiwe colonized? Mbona miungu yao haikuwapa akili za kujua kuzaa mapacha ni baraka na si laana? Mbona hiyo miungu haikuwapa akili za kujua albinism ni inherited disorder na si laana? Hivi hujui hizo dini za babu zenu ni za kishenzi na mambo mengi ya kishenzi walifanya katika kuitumikia miungu yao na historia inathibitisha hayo? Sisi tunamtumikia Mungu Aliye juu ambaye kwake hakuna ushenzi.
Siku nyingine ka argue wa wenzako mlio gizani
 
Biblia zimetapakaa kila kona, katafute maarifa humo. Jaribu kufuatilia mafundisho ya mwl. Mwakasege huwa anaongelea maswala mbalimbali ikiwemo laana inayoweza kuipata nchi na taifa

Nakuelewa na ninayafuatilia sana mafundisho yake. Ila haimaanishi kwamba Kwa nchi kuhalalisha vitendo vya kishetani nchi nzima inakua haina uwepo wa Mungu. Hata Kama wapo wawili bado Mungu ataendelea kuwa nao. Neno la mtu mmoja sio sheria. Ishi mahali physically ndio utoe judgement sio Kwa Habari za kusikia.
 
Watu wengi wakisikia kumtumikia Mungu mawazo yao yanaenda kwa watumishi wanaosimama kwenye madhabahu kwa ajili ya kuhubiri wanasahau hata wao wanaweza kumtumikia Mungu katika nafasi walizonazo kama wakisimama katika haki, Bilbia inasema .Ufalme wa Mungu si kula na kunywa bali ni haki, amani, furaha katika Roho Mtakatifu WARUMI 14:17
Kwa hiyo kama upo kazini na ukasimamia haki katika kazi unayofanya tayari wewe ni mtumishi wa Mungu unaemwakilisha Mungu katika kazi au biashara yako na wengi watavutwa kwa matendo yako mema
Mstari wa 18 anamalizia kwa kusema 18Kwa kuwa yeye amtumikiae Kristo katika mambo hayo Humpendeza Mungu tena hukubaliwa na wanadamu

Well said.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom