LUBEDE
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 4,322
- 6,694
Wakuu,katika maisha yangu nilishajiwekea nadhili(kiapo),
kuwa kamwe sitokuja kuchangia harusi wala kutoa sadaka kanisani(mimi ni mkristo).
Mwanzoni nilikutana na vigingi,vikwazo na vitisho kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki,
baada ya kuwapa msimamo wangu,hasa baada ya kuona nina kadi karibia kumi zinataka elfu 50 na 70 na za laki nichangie,
nikapata wazo na akili mpya ya kubadilisha mfumo wa maisha.
Pamoja na kuambiwa kuwa ipo siku na mimi nitapata shida na sitochangiwa,niliamua kuziba pamba masikio na kuisikiliza nafsi yangu,
Nashukuru mungu leo nafunga mwaka wa tatu bila kufanya huo niliouona upuuzi,na hakuna ghasia yeyote iliyonipata,
maana michango yangu niliamua kuielekeza kwa wenye uhitaji wa lazima like magonjwa,elimu,na matatizo ya ghafla(misiba)na mengineyo yasiyo anasa,matokeo yake bado nimeendelea kukubalika zaidi na kuonekana kama Saint kutoka kwa wale walionikatisha tamaa.
Najipongeza kwa kufikisha hii miaka mitatu bila kutoa michango nyonyevu,tukiamua tunaweza,hakuna linaloshindikana!