GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Hii hali huwa nakutana nayo mara kwa mara siku za Jumapili hasa pale ambapo niwapo ' Ibadani ' kwa kumuona kabisa Mtu anaenda kutoa Sadaka tena akiwa katika ' Mikogo ' yote na tena hatoi Hela ndogo ndogo za ' coins ' bali unaweza kumwona Mtu kabisa anatoa Tsh 5,000/ au Tsh 10,000/ lakini cha kushangaza ibada inapoisha tu na mkitoka mkiwa Kituoni kusubiri Usafiri unakuta ' lijitu ' lile lile lililotoa Sadaka kubwa linakuja ' linakunong'oneza ' sikioni kuwa umlipie nauli ya Tsh 400/ afike huko aendako.
Najua humu ' Jamvini ' kuna Waumini wenzangu wengi hebu tusaidiane katika Je kumaliza Hela yako yote kwa kuitoa kama Sadaka ' ibadani ' kanisani kisha unakuja kusumbua Watu kuwaomba nauli ndiyo imani ya kweli tunayohubiriwa au Waumini wengi tuna ' Pepo ' la Ujinga kama siyo Upumbavu?
Nitashukuru kwa majibu yenu kwani leo nimekwazika mno baada ya ' Njemba ' moja ambayo imemaliza Hela yake yote kwa kutoa Sadaka halafu kaomba nimsaidie nauli hivyo kupelekea kuharibu kabisa ' Bajeti ' yangu hasa ukizingatia maisha ya sasa ni magumu hadi unakuta Mtu hata Chenji tu ya Tsh 50/ unaidai kwa nguvu zote huku ' Mishipa ' yote ya Shingoni ikikusimama.