Siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NASSARY EGM, Apr 8, 2012.

 1. N

  NASSARY EGM New Member

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 3, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siasa ni mchezo ambao kila mtu anaupenda hasa wale wakereketwa wa siasa hata mimi pia nimkereketwa wa siasa lakini kunajamba ambalo nimeliona katika siasa ya Tanzania kwa hili lazima niwe wazi kuwaeleza wanasiasa wa kitanzania hasa chama tawala. kwanza nakipongeza Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa ushindi wa kishindo walioupata hapa Arumeru Mashariki kwenye uchaguzi mdogo. nikweli tulikuwa tumechoka ahadi za uongo za Chama Cha Mapinduzi, na kwa ajili ya tatizo kubwa la CCM la kusema uongo mbele ya wananchi wa Arumeru Mashariki kimewagharimu sana CCM hili ni anguko kubwa la CCM na niishara ya kubwa ya mwaka 2015 kuwa CCM isipokuwa makini itakuwa nimwisho wa utawala wao. Makampeni meneja wa alikuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM walikuwa wakituambia tumchague Siyoi kwani nichaguo la Kikwete wengine walisema tumchague Siyoi ili tumfute machozi je? hizi ndo sera sa CCM? Sasa kunakitu nimeona kwa kuwa Siyoi alikuwa chaguo la Mheshimiwa Kikwete, na hakupata kura za Wanaarumeru hii ni ishara yakutosha kuwa Kamati kuu ya CCM isipokuwa makini katika kumchugua mtu anayekubalika katika kugombea urais mwaka 2015 basi anguko lake litavunja record zote Africa na hata Duniani kwani. Huu ni ushauri wa bure kwa CCM na yeyote ambaye atasoma na anauwezo wa kuonana na washauri wa CCM awape ujumbe huu na ushauri huu wa bure wasipoukubali ni raha sana kwa CHADEMA kwani ule ukombozi ambao CHADEMA kinataka kuufanya Tanzia basi muda utakuwa umewadia. MWESHIMIWA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ALIFAHAMU HILI.
   
Loading...