Siasa zetu zinatuponza. Tumshauri Rais kuhusu Covid-19

pureman2

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
1,494
2,538
Kupitia forum hii ya JF naomba kuwasilisha ushauri wangu.

Kwa mjibu wa katiba yetu Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ndio mfariji mkuu, na kwa msingi huo naomba kumshauri raia namba moja Mh. John P. Magufuli.

Rais wetu licha ya kuwa Msukuma mwenzangu, yeye pia ni mwana Chato mwenzangu na jirani yangu hivyo kwa mila zetu nawajibika kumpa ushauri kwa nia njema kabisa.

Mh. Rais, Ushujaa wako, misimamo yako, na uzalendo wako kwa taifa hili kwa sasa ni dhahiri, sio ndani ya mipaka ya nchi yetu tu bali katika kanda na jamiii ya kimataifa sifa na haiba yako imejulikana. Umeongoza vita ngumu nyingi, umepambana sana, nyingi umeshinda na nyingi utazishinda, ila natamani katika kutuongoza katika vita ya mapambano juu ya adui maradhi ya COVID-19 ni maombi yangu kama ilivyo kiu ya watanzania wengi kuona ukituvusha kwa ushindi bila maumivu makubwa. (Mungu tusaidie)

Bila shaka kama mmoja wa wananchi na kiongozi mkuu wa taifa hili unatambua na kufuatilia vyema kuwa kumeibuka hofu waliyonao Watanzania juu ya ungonjwa wa kupumua unaoripotiwa kuchangia kupoteza maisha ya wananchi wengi kuanzia mwishoni mwa mwaka jana hadi sasa . Tumesikia na kushuhudia vifo vya ndugu, wazazi wetu, majirani, wafanyakazi wenzetu na wafanyabiashara wenzetu, wakufunzi wa vyuo, wachungaji na mapadri wakiripotiwa kuwa wamefariki kufuatia kuugua kwa muda mfupi na maradhi yaliyoambatana na changamoto za upumuaji.

Kwa kuwa jamii yetu ni sehemu ya dunia kumekua na wasiwasi kuwa huenda maradhi haya yakawa ni ugonjwa wa COVID-19 ambao pia umeripotiwa duniani kote kusababisha vifo kwa zaidi ya watu milioni 2, na zaidi ya watu milioni 107 wakiwa wameshaugua ugonjwa huo toka ulivyoripotiwa kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka 2019 kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo huko jimbo la Wuhan China.

Kwa mara kadhaa Mh. Rais umekaririwa na vyombo vya habari ukizungumzia ugonjwa huo na kuitaka jamii kuchukua tahadhari na huku ukibainisha msimamo wako kuwa mapambano dhidi ya ugonjwa huu nilazima yazingatie kumtanguliza Mungu mbele. Hivi karibuni tena umekaririwa ukiwatupia lawama baadhi ya watanzania wenzetu walioenda nje ya nchi kupatiwa chanjo iliyosemekana kuruhusiwa kutumika katika mataifa mengine hasa ya Ulaya na America kuwa uenda waliporudi wametuletea maradhi haya na tena ukatilia shaka kuwa wametuletea virusi vipya vilivyo mutate kutoka katika virusi vya awali. Lakini kwa sehemu flani serikali unayoiongoza kupitia wizara ya Afya haijajitokeza wazi na kuja na kauli ya serikali juu ya uwepo wa janga hili hapa nchini.

Mwanzoni mwa wiki hii kupitia Bunge linaloendelea Dodoma kwa nyakati kadhaa baadhi ya wabunge walikaririwa wakikikupongeza kwa msimamo na njia uliyoitumia na unayoitumia hadi sasa kupambana na changamoto hii kuwa ni bora na iendelee. Mmoja wa wabunge hao ni Mh. Mch Gwajima ambaye yeye alienda mbali zaidi hata kuitisha kuwa social distancing haifai na vyema maisha yakaendelea kama kawaida. Kama shujaa alipigiwa makofi na baadhi ya wabunge wakiashiria kukubaliana na mtazamo wake na hoja yake kubwa ya msingi ikiwa hofu ya Corona ina nguvu kuliko uhalisia wa ugonjwa COVID-19 yenyewe.

Kwa utangulizi huu niruhusu sasa nitoe maoni na ushauri wangu kwako:

i) Mosi, umewahi ona wapi kuwa hofu ya ugonjwa inawafanya watu kupata changamoto ya upumuaji na hata licha ya kufika maeneo ya kutolea huduma za afya mtu huyo anapoteza maisha gafla? Msingi wa swali hili ni kuwa wasiwasi utaendelea na kuzidi kuongezeka hadi vyombo vyenye dhamana na kusimamia afya ya watanzania vitakapojitokeza na kudhibitisha kisanyasi tatizo hili ni nini hasa na sio kubashiri tu kuwa ugonjwa wa matatizo wa upumuaji!

ii) Baadhi ya viongozi katika sekta ya afya wamekuwa wakikaririwa wakisema sio kila mtu mwenye changamoto ya upumuaji ana Corona -Huu ni ukweli kabisa kwani magonjwa mengi tu yanaambatana na changamoto ya upumuaji ikiwemo Bacteria/virus/ fungal -pneumonia, maladhi ya moyo, figo, kansa na hata TB. Ila ebu tujiulize kwa kuwa dunia haijaanza leo na katika mifumo yetu ya kutolea huduma tunakusanya takwimu za vyanzo vya maradhi na vifo , je hayo maradhi tuliyoyazoea huwa yanaathili watu kwa kiwango gani?(prevalence) na chance ya kusababisha vifo vya gafla/muda mfupi iko vipi?(death rates).

Takwimu huwa hazisemi uongo , wataalamu wetu wafanye uchambuzi yaani death audit ya vifo vinavyotokea kwenye jamii na vituo vya kutolea huduma za afya na comparison ifanyike kwa kutumia takwimu za vifo zilizokusanywa na kutunzwa kwenye mifumo yetu ya afya, na ikiwa kuna utofauti mkubwa watueleze utofauti huo chanzo chake ni nini? je kuna tatizo kwenye hospitali zetu au kuna adui maradhi mpya kaingia nchini na hatujatambua ni nani na yuko wapi na anaathiri akina nani zaidi?

iii) Kutokana na ukimya ulipo wa mamlaka za serikali na matamshi ya kiujumla jumla kuwa wananchi wachukue hatua-mwitikio umekuwa mdogo sana ukilinganisha na namna taifa lilivyoshikamana mwaka jana. kipindi kile toka waziri wa afya, viongozi wa dini, mabarozi na wananchi tuliimba wimbo mmoja na matokeo tuliyaona ya mwitiko na ushiriki wa pamoja kama jamii juu ya adui Corona. Tofauti na kipindi hiki, hakuna wahamasishaji wa kitaifa, na kila mwananchi anachukua hatua zake as individual na sio "public approach".

kwa msingi huu ni vigumu kupata matokeo makubwa kupitia "individual approach" katika kukabiliana na ugonjwa wa mlipuko. Mfano wazee wetu wanashinda nyumbani , sisi kutwa nzima tuko shughurini amabako hakuna taadhari za pamoja , tukiambukizwa huko tukirudi nyumbani tunawaambukiza waliobaki nyumbani. kwa namna hii mbona tutaisha?...Mh. Rais naomba utusaidie kuhamasisha taifa tuwe na collective public approach.

iv) Ni ukweli usiopingika kuwa kwa kufuata kanununi za kisayansi zinazopendekezwa na shirika la Afya duniani (WHO), mapambano juu ya virusi vya Corona yanahitaji raslimali pesa . kwa vipindi kadhaa serikali imekua ikikiri kuwa haina pesa za kuwafungia watu ndani, watanzania hawa masikini watakufa kwa njaa. Ni kweli uchumi wetu ni mdogo ila kulinda maisha ya watu wetu ni jukumu letu la msingi na tunawajibika kufanya hivyo.

Sote tunakubaliana "nothing is worthy more than life". Mh. Pamoja na uchumi wetu mdogo ebu tuhimizane kama jamii kutumia resources zetu kufanya hata mambo ya msingi kama kupima nani ameathirika , kuwapatia PPE watoa huduma ambao ni asikali wetu walio mstari wa mbele, tuwakinge kwa chanjo makundi yaliyo kwenye hatari zaidi, kununua dawa na vitendanishi vinavyotumika kuwahudumia wagongwa serious wa COVID-19, kuhamasisha jamii kufuata kanuni za afya kama kuhepuka misongamano, kunawa mikono kwa maji tiririka, uvaaji wa barakoa tulizozitengeneza wenyewe n.k.

Katika hili tunaweza kukubali kutofautiana ila naamini kwa kushirikiana na dunia tunaweza zipata resources za kufanikisha mambo haya na dunia ikaona na kutunza record kuwa tumewajibika kama nchi kuhifadhi maisha ya watu wetu. Tunaweza tusifanye mambo haya yote kwa ubora na uwezo kama walionao nchi za magaharibi ila kwa sehemu kubwa tutakua tumechangia kuhepuka vifo na hatari za uchumi za muda mrefu zinazoweza kujitokeza. kama observations tunazoziona wanokufa wengi ni watu wazito katika jamii zetu ambao ndio rasilimali watu na wataalamu wetu ambao hatuna luxury ya kupoteza nguvu kazi hii ya taifa kwa kutochukua hatua za pamoja kama taifa.

Mwisho ni maombi yangu Mungu akupe utulivu, umakini, mafunuo, uthubutu na roho safi ya kujali maisha ya wananchi wa taifa hili ambao Mungu amekupa neema ya kuwa kiongozi wetu. Mungu akusaidie sana mfariji mkuu, raia namba moja wa taifa hili na Rais wetu mpendwa na mwana Chato mwenzangu.

Waione washauri wote wa Rais
Waione wawakilishi wa wananchi
Waione wananchi wa kawaida wa Taifa hili

Ni mimi mwanachato mwenzako.
 
Rais wenu hashauriki, ndio maana katengeneza mazingira ambayo viongozi na watumishi wote wa umma wanaishi kwa kutegemea ameamkaje siku hiyo.

Mtu anaye dictate hata upatikanaji wa Meya au haaiyeheshimu mamlaka za serikali za mitaa(local government) unategemea atakuwa na mtu wa kumshauri kweli?
 
Asante mleta mada someni ni muhimu.

1. Corona ni gonjwa serious, tumuombe Mungu atunusuru.

2. Kila mmoja achukue wajibu binafsi kujilinda na kuwakinga wengine.

3. Kwa kuwa ni garama kubwa tutumie kila tiba asili iliyothibitika, lishe nk.

4. Serikali itimize wajibu wake wa msingi kuwa na mpango dhabiti na sio kukwepa wajibu.
 
Rais wenu hashauriki, ndio maana katengeneza mazingira ambayo viongozi na watumishi wote wa umma wanaishi kwa kutegemea ameamkaje siku hiyo.

Mtu anaye dictate hata upatikanaji wa Meya au haaiyeheshimu mamlaka za serikali za mitaa(local government) unategemea atakuwa na mtu wa kumshauri kweli?
Lingaliko tumaini. People do change
 
Ugonjwa tumeshaumaliza kwa maombi, wananchi tembeeni kifua mbele Corona haina chake Tz.... ila nawasihi zingatieni ushauli wa watalaam wa afya!!
 
Ugonjwa tumeshaumaliza kwa maombi, wananchi tembeeni kifua mbele Corona haina chake Tz.... ila nawasihi zingatieni ushauli wa watalaam wa afya!!
Kauli tata na zinazokinzana.

Tuache kutoa Kauli Kama hizi na tujikite kufanya kazi kwa weredi . Wizara ya Afya isijifiche nyuma ya Kauli Kama hizi bali ijitokeze na kuongoza mapambano
 
Hata kama nitadedi na coona lakini ningefarijika sana kama jiwe angepigwa na hii kitu tumfukie chini, yule mwehu mjengoni atandikwe tumfukie down, Yule mlima korosho akutwe amekauka na yule maza mzenji andei na dipotivo la coruna hapo tutachukua hatua za kuokoa wengine
 
Hata kama nitadedi na coona lakini ningefarijika sana kama jiwe angepigwa na hii kitu tumfukie chini, yule mwehu mjengoni atandikwe tumfukie down, Yule mlima korosho akutwe amekauka na yule maza mzenji andei na dipotivo la coruna hapo tutachukua hatua za kuokoa wengine
Mungu hutuhurumia sote
Tuvumiliane na kuombeana
 
Back
Top Bottom