Wana jamii.
Nimesoma katika economic forum na kuona BP imeamua kuuza hisa zake zote ilizokuwa inamiliki katika BP Tanzania kwa mwekezaji mwingine na hivyo kujitoa rasmi katika umiliki wa kampuni hiyo ndani ya Tanzania.
Na sababu walizobainisha ni kwa kuwa biashara ya mafuta inaendeshwa kisiasa zaidi na mamlaka za Tanzania na kwa kuwa wao hawakuwa tayari kugombana na mamlaka hizo ndani ya TZ wameamua kujitoa rasmi kwa kuuza hisa zao zote 50% kwa kampuni nyingine.
My Take: Je ni wapi waTZ watapata mafuta kwa ajili ya magari yao yasiyochakachuliwa? na vipi mafuta ya ndege itakuwaje?
Nawapa Pole wa Tz na kuwapongeza BP kwa kujali ubora wa bidhaa zenu.
Naomba kueleweshwa inamaana nembo ya bp sitoiona tena katka vituo vya wese!
Inabidi wawekezaji wa ndani wajitahidi, tusipate impact yeyote negative kutokana na maamuzi hayo. Hata hivyo Tanzania sasa hivi inawawekezaji wengi sana wakubwa katika sector ya mafuta tuna waarabu wengi tu na wazawa wengi wameibuka katika miaka ya hivi karibuni kama akina Ridhwani KikwetteKuna taarifa kwamba ccm wameingia mkataba na kampuni ya camel oil, huenda ndiyo itapewa jukumu la kuhakikisha mafuta yanapatikana kwa wingi wa kutosha!!
Vile vile tumeambiwa TPDC wameshafungua tender kwa ajili ya kupata kampuni itakayofanya biashara ya mafuta na COPEC kwahiyo hilo gap la BP linaweza kuzibwa na COPEC!!
Suala la kuchakachua mafuta halihusu depots, uchakachuaji unafanyika mahali pengine kabisa na vijiwe vya kuchakachua vinafahamika.
We pita tu barabara ya morogoro kati ya kibaha na chalinze uone utitiri wa vituo vya mafuta na maukuta marefu yaliyojengwa nyuma ya vituo ama kuzunguka vituo, uone misururu ya malori ya mafuta, then ujiulize ni biashara gani inafanyika humo?
Kwa hatua hii ya BP kuna uwezekano wa nchi kukumbwa na matatizo ya upatikanaji na ubora wa mafuta.
Mafuta yasiyochakachuliwa na usimamizi mbovu tu wa serikali ya ccm, unajua kule depot hakuna mafuta yanachakachuliwa,deal hizo zinapigwa mitaani/vituoni so wakisimamia yatapatikana tu. Lkn pia kujitoa kwao ni pigo kwa ajira za wabongo waliokuwemo nk
Naomba kueleweshwa inamaana nembo ya bp sitoiona tena katka vituo vya wese!