Siasa zahusishwa vurugu za RUVUMA

Siasa zahusishwa vurugu za RUVUMA

samirnasri

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
1,388
Reaction score
215
kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma ambaye jina lake sikulishika vizuri anasema vurugu zilizotokea leo asubuhi kati ya waandamanaji na polisi na kusababisha vifo vya watu watatu zimesababishwa na imani za kishirikina na siasa ndani yake. Wananchi walikuwa wakiandamana kupinga wimbi la mauaji ya raia yaliyokithiri mkoani ruvuma na kuitaka serikali ichukue hatua.


source: tbc
 
Nimemuona na kumsikia RPC Kamuhanda anaongea pumba tupu...amini usiamini alipotaja siasa alimaanisha CHADEMA...Siku hizi mtu ukitambua haki zako na kuzidai wewe ni CHADEMA na huo ndiyo ukomo wa kufikiri kwa serikali yetu...kinachofuata ni maji washa,mabomu ya machozi na risasi za moto...Ukweli haya ni matunda ya elimu a uraia ambayo imekuwa ikitolewa na CDM kupitia operation Sangara...Kila la kheri CHADEMA.
 
yaani wananchi wakisema 'tunauawa polisi chukueni hatua' kuna ushawishi wa siasa!.......kweli tanzania kuna mambo!naona kamanda alitaka wananchi wakae kimya mpaka pinda aje kulia bungeni.
 
Wanasiasa wengi wamekuwa wabakaji mapinduzi na hoja mbali mbali zinazoanzishwa na wananchi kuidai serikali yao, tabia hii inawakosesha sana wananchi haki zao, kwa kuwa jambo linageuzwa ni la kisiasa na kupoteza malengo ya awali.

Kama huamini angalia moja ya post inaonyesha mana CDM mmoja akishauri slaa na wenzake waende songea kupandisha CV, kwa mtazamo wangu mimi nafikili kuna mambo ambayo wananchi wana haki ya kudai kutoka serikali yao bila kuingiliwa na hawa wanasiasa waroo wa madaraka.
 
Naamini wananchi walioathirika ndo wanaelewa undani wa jambo hili. Uongo wa rpc ndo uhalali wa mauwaji haya? Wana Songea tafakarini na mchukue hatua.
 
Wanasiasa wengi wamekuwa wabakaji mapinduzi na hoja mbali mbali zinazoanzishwa na wananchi kuidai serikali yao, tabia hii inawakosesha sana wananchi haki zao, kwa kuwa jambo linageuzwa ni la kisiasa na kupoteza malengo ya awali.

Kama huamini angalia moja ya post inaonyesha mana CDM mmoja akishauri slaa na wenzake waende songea kupandisha CV, kwa mtazamo wangu mimi nafikili kuna mambo ambayo wananchi wana haki ya kudai kutoka serikali yao bila


kuingiliwa na hawa wanasiasa waroo wa madaraka.

we ni gamba kubwa nimekufuatilia tokea asubuhi kwenye michango yako hakika we ni gamba uchwara
 
wananchi saba waliuwawa kwa siku zisizozidi tano, wananchi wanatoa taarifa polisi, na kuomba ulinzi, hawajawahi kupewa.

Wananchi wameona enough is enough, ngoja tushinikize watuelewe kwamba tunauwawa na tunahitaji ulinzi, matokeo yake, chombo kilichotakiwa kuwalinda in the first place kikawauwa raia qengine watatu!!

Rediculous, badala ya RPC na RC ku-apologize, wao wanaongea kama vile they own the people and they can kill them wherever they want to.

A land of clowns......not named yet, by MMJ.
 
kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma ambaye jina lake sikulishika vizuri anasema vurugu zilizotokea leo asubuhi kati ya waandamanaji na polisi na kusababisha vifo vya watu watatu zimesababishwa na imani za kishirikina na siasa ndani yake. Wananchi walikuwa wakiandamana kupinga wimbi la mauaji ya raia yaliyokithiri mkoani ruvuma na kuitaka serikali ichukue hatua.


source: tbc

Suala la kuua wananchi kwa risasi sasa limekuwa normal kwa Police. There is no justification ya kumpiga risasi mtu anayekurushia mawe.

Wakipigiwa simu kuna majambazi yana silaha yanavunja sehemu wanajivutavuta kwenda ila wananchi wasio na silaha ndiyo wanaona soft target ya kuona kama risasi zao bado zinaua baada ya kuhifadhiwa kwenye maghala muda mrefu bila kutumika.

Vyovyote watakavyoandika hakuna justification ya kutoa uhai wa mtu aliyekaa tumboni kwa mama yake miezi Tisa akahudumiwa kwa miaka 20 au 30 na wazazi wake halafu wewe unakuja kuyakatisha kwa sekunde moja tu ya ku-pull trigger. Kuua mtu ni uamuzi mzito sana ambao unatakiwa kupata baraka za mahakama tu, otherwise uwe ni jambazi usiye na huruma.

Kosa la kumtupia mawe polisi si kifo, hiyo ieleweke. Polisi wanakuwa wavivu katika kutekeleza majukumu yao, wanatumia short kati. Kama watu hao wangekuwa na silaha za moto kweli ningekuwa upande wa polisi 100%. Maana mwenye silaha ya moto akienda Rogue njia pekee ya kulinda wengine ni kumuangusha yeye.

Na hii excuse ya siasa kuchochea fuja indhihirsha wazi kuwa hawa polisi wamekuwa 'Armed wing of a political party in power' wakizidiwa wanaona njia pekee ya kujinusuru ni kuhusisha siasa maana hilo litawafanya waliowateua waone kuwa kuna Mutual benefit kati ya police na wao na hivyo kuwachukulia polisi hatua kunaweza sababisha huko mbeleni wasikubali kutumiwa kukandamiza demokrasia kwa manufaa ya watawala.
 
Hakuna watu wanoniudhi kama wakubwa wa Polisi, ma RPC's na Makamishna walioko Makao,mara zote wanakwepa kuwajibika tu na kuelekeza burden of guilty pahala pengine! Sioni ni vp siasa inaingia katika hili
 
Huu msemo 'HIZO SIASA' au mimi 'SIYO MWANA SIASA' imezooeleka sana kwa Viongozi wetu. Hasa kwa wakuu wa Mikoa,Wilaya na Wababe wetu 'PWOLISH!', mimi sikubariani kabisa ya kwamba jeshi la Pwolish lina linda raia, wameishakua majambazi tu!
 
Mimi nilidhani hii kauli peke yake ingetosha kumuondoa kazini (sio kumhamisha) kwa sababu ameshindwa kabisa kulinda uhai wa raia.

Watu wa Ruvuma wamelazimika kuingia barabarani baada ya mauji ya kinyama yanayofanyika KILA SIKU kwa siku kadhaa sasa. Pamoja na kwamba watu wanatoa taarifa kwa polisi lakini hakuna lolote limefanyika. Leo hii huyu baba anasimama na kusema watu wako barabarani kwa sababu ya siasa?

Huku kama sio ku-victimise watu wa Ruvuma kwa mara ya pili ni nini? Kwanza watu wauawe, na pale wanapopaza sauti za kudai haki yao ya kulindwa atoke kamanda wa polisi na kusema -ah hayo ni mambo ya siasa! Kwa vipi hizi vurugu ni za siasa?
 
Duh kazi kweli. Yaani kila kitu sihasa. Hivi viongozi wanatuona wajinga mpaka lini?
 
Ukweli ni kuwa Polisi wa Ruvuma wameshindwa kazi.
Hawana mbinu zozote za kudhibiti wimbi la mauaji yanayotokea huko, hivyo wametaFUTA utetezi rahisi ambao wanajua wakubwa wa polisi na serikali wataupokea bila hata chembe ya kuhoji!
What do you expect of a group of politicians who can posses Pollonium-210 in their pockets, just to kill one another?..Unadhani suala kuuawa wananchi litawagusa?...Nadhani hata akili zao zimeshapata effect za radiation za pollonium!
 
Hebu turudi kwenye maswali ya msingi,
kwani siasa ni nini?
Kwenye mstari wa kimamlaka, anaripoti kwa nani juu kabisa??
Mfumo wote wa dola ni nini??
Tunafikra finyu sana inapokuja kwenye tafsiri ya neno SIASA!

Hili suala lilipofika hatuhitaji tena majibu toka kwake yeye RPC, tunataka majibu toka kwa mabosi wake.
 
Back
Top Bottom