Siasa za Watanzania Wataweza bila matusi, kejeli?

Mtu_Mzima

JF-Expert Member
Oct 1, 2014
1,163
1,125
Sio wengi wametafakari maana ya muafaka uliofikiwa na huu msemo wa "siasa za kistaarabu" kama wanavyounadi viongozi wakuu wa vyama vya siasa.

Kwa upande wa CCM nawaona haswa wabunge, madiwani na makada wao (haswa UVCCM na UWT) wakipata taabu kwani wamezoea siasa za kejeli, kununua wapinzani nk. Wataweza kusimama majukwaani na kujenga hoja zenye nguvu bila kurusha matusi na kejeli upinzani?

Kwa upande wa CHADEMA, nawaona wamegawanyika makundi mawili; Kundi la Mbowe/Mnyika nk la siasa za kistaarabu na kundi la Lisu/Lema/Heche nk la siasa za ukosoaji hasi.

Upande wa majili wa vyama vya Siasa huko sijui kama hata wameshajitathmini na kuupima huu upepo.

Upande wa Polisi naona wameanza vizuri, ila sijui mambo yakishika kasi na wale wanasiasa ambao wakiona mambo yao yamewaelemea wanakimbiliaga polisi; wakati huo ukifika wataweza kubaki njia kuu?

Vyama vya siasa vinahitaji kujipanga na semina elekezi kwa wagombea wao wajao kwani wengi hawawezi siasa za kistaarabu. Wakitukana jimbo litakuwa wazi.

Maana kuna dhana ya CCM ni untouchable na upinzani ni kutukana tu, hakuna kilichofanyika.

Tusubiri tuone
 
Back
Top Bottom