Siasa za Vyama Vingi ni Hatari kuliko hata Mabomu ya Nyuklia.

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Sikujua Lengo la mwanzilishi wa Siasa za vyama Vingi labda kwenye nchi zenye Demokrasia ya Kweli naweza kusema NDIYO.
Ila kwa baadhi ya nchi Siasa za Vyama Vingi zimekua ni kaa La moto,zimekua hatari sana,Ndugu zetu wengi wamepoteza Maisha kwa aina hii ya Siasa,Leo watu wanashindwa kukaa pamoja na kufanya maendeleo kwa ajili ya aina hizi za Siasa,Watu wametengeneza makovu ya Hasira,Chuki,Visasi kwa aina hii hii ya Siasa.

Tukirudi Nyuma kidogo Wazee wetu walikua na Mifumo yako kama vile Ujamaa/Ujima ambapo watu waliishi kwa Amani,ushirikiano,Upendo na Umoja wa hali ya juu,Hata leo ukiangalia makabila yote yenye kufuata hii Mifumo wanaishi kwa Amani sana na upendo wa hali ya juu.

Nchi nyingi leo zimeingia kwenye mifarakano na migawanyiko kutokana na Siasa za Vyama Vingi,Watu wengi wamepoteza maisha kutokana na Aina hii ya Siasa.

Ni bora Baadhi ya Nchi zingeendelea na Ulimbombo na Ulindi kuliko aina hii ya siasa.
 
Back
Top Bottom