Siasa za Upinzani Tanzania ni za kitoto sana!

Musoma

Senior Member
Oct 12, 2010
137
221
Kweli nimeamini njaa ni kitu kibaya sana! Njaa inaweza kumfanya Profesa awe na upeo mdogo wa kufikiri kuliko "teja" la pale Kinondoni Studio!

Eti Profesa Lipumba ametengua barua yake ya kujiuzulu na kujirudisha kwenye Uenyekiti wa Chama cha CUF bila maamuzi ya vikao wala kupitia mchakato wa uchaguzi!
Hivi Profesa Lipumba alipojiuzulu Uenyekiti ,Chama cha CUF si kilikaa na kumpata kaimu Mwenyekiti ambaye yuko mpaka sasa Mhe.Twaha Taslima.Sasa inakuwaje Profesa mzima anafanya siasa "pori " kama hizi!?
Zitto Zuberi Kabwe naye ukimsikiliza kwa makini ni kama ana- pre empty mazungumzo yake aliyofanya na viongozi fulani wakubwa ndani ya CCM kuhusu Rais John Magufuli!
Kauli kama vile, alienda Rwanda kujifunza namna ya kudhibiti wapinzani na demokrasia (hapa lazima ujue Zitto anamfurahisha nani), si rahisi kuanzisha vita ya kidiplomasia kwa kiongozi makini bila sababu!
Kauli yake nyingine ya kitoto ni ile ya eti CCM imdhibiti mwanachama wake na ikishindwa watamdhibiti wao! Na ya mwisho ni ile kauli ya Magufuli atakuwa Rais wa term moja!

Zitto fanya siasa acha sasa kucheza ngoma za kulipwa!
 
Kweli nimeamini njaa ni kitu kibaya sana! Njaa inaweza kumfanya Profesa awe na upeo ndogo wa kufikiri kuliko "teja" la pale Kinondoni Studio! Eti Profesa Lipumba ametengua barua yake ya kujiuzulu na kujirudisha kwenye Uenyekiti wa Chama cha CUF bila maamuzi ya vikao wala kupitia mchakato wa uchaguzi! Hivi Profesa Lipumba alipojiuzulu Uenyekiti ,Chama cha CUF si kilikaa na kumpata kaimu Mwenyekiti ambaye yuko mpaka sasa Mhe.Twaha Taslima.Sasa inakuwaje Profesa mzima anafanya siasa "pori " kama hizi!? Zitto Zuberi Kabwe naye ukimsikiliza kwa makini ni kama ana- pre empty mazungumzo yake aliyofanya na viongozi fulani wakubwa ndani ya CCM kuhusu Rais John Magufuli! Kauli kama vile,alienda Rwanda kujifunza namna ya kudhibiti wapinzani na demokrasia (hapa lazima ujue Zitto anamfurahisha nani),si rahisi kuanzisha vita ya kidiplomasia kwa kiongozi makini bila sababu! Kauli yake nyingine ya kitoto ni ile ya eti CCM imdhibiti mwanachama wake na ikishindwa watamdhibiti wao! na ya mwisho ni ile kauli ya Magufuli atakuwa Rais wa term moja! Zitto fanya siasa acha sasa kucheza ngoma za kulipwa!

Katika wanasiasa ambao hapa Tanzania sijawahi kuwa trust ni Zitto. Zitto ni mwanasiasa opportunist, ambae yupo tayari kufanya lolote kutetea ugali wake na si maslahi mapana ya Taifa. Zito ni bora atambue kuwa, sisi watanzania tumesoma pattern ya siasa zake, na tumeshajiridhisha pasi na shaka kuwa Siasa zake msingi wake ni tumbo lake mwenyewe na si vinginevyo.

Naomba pia nimfahamishe Zitto kuwa, sisi watanzania, tuna imani kubwa na Raisi wetu, na Morally ZZK hawezi kulinganishwa na Magufuli, kwa positions ambazo alishashika Magufuli, you can imagine angekuwa ni zitto angekuwa ameshapiga deals kiasi gani. Ndugu Musoma, tujiulize mwaswali haya

1. Je, Zitto kabwe, anawaambia CCM wamdhibiti mwanachama wao kwakuwa anadhibiti wapinzani?. Ni kweli msingi wa huu ushauri wake unaweza kumshawishi kiongozi yeyote wa CCM auzingatie?. Unamaanisha nini Muheshimiwa?

2. Je, Mh.Zito, anatuambia kuwa Rais wetu mpendwa atakuwa wa kipindi kimoja kwa sababu anadhibiti Upinzani?. Anatuambia upinzani uliodhibitiwa ndio utakao mtoa ikulu?. Kama upinzani umedhibitiwa utawezaje kumuondoa Rais Madarakani ndani ya term moja, wakati vipindi vyote ambavyo marais hawakwenda Rwanda na kujifunza na mna ya kudhibiti upinzani, na hakukua na Jitiada maksudi za kudhibiti upinzani na upinzani ulishamiri lakini haikutokea Rais akatawala kwa Term moja???. Unamaanisha nini Muheshimiwa?

Zitto, tambua kuwa katika viongozi ambao watavunja record kwa kuchaguliwa na wananchi wengi ni Mh. Magufuli ktk uchaguzi wa mwaka 2020. Magufuli amefanikiwa kuinyang'anya CCM ndani ya mikono ya Wafanya biashara wakubwa waliokuwa wakiinyonya Tanzania kwa gharama ya Maisha ya watanzania masikini waliowengi. Sisi tunamuunga mkono, na tunamkubali sana.

Acha double agency kaka.
 
Kama ni za kitoto kwanini mnawaogopa? anaegopa sku zote n mtoto.Toa maelezo tujue kati ya upinzani anayeandamwa na polisi kila sku au CCM anaejificha nyuma ya polisi ni nani mtoto?
 
Kama ni za kitoto kwanini mnawaogopa? anaegopa sku zote n mtoto.Toa maelezo tujue kati ya upinzani anae andamwa na polisi kila sku au ccm anaejificha nyuma ya polisi ni nani mtoto?
Hawaogopwi bali ni watoto wajinga ambao wakiachwa bila mkong'oto hawachelewi hata kunya sebuleni, lazima wadhibitiwe !
 
Kweli nimeamini njaa ni kitu kibaya sana! Njaa inaweza kumfanya Profesa awe na upeo mdogo wa kufikiri kuliko "teja" la pale Kinondoni Studio! Eti Profesa Lipumba ametengua barua yake ya kujiuzulu na kujirudisha kwenye Uenyekiti wa Chama cha CUF bila maamuzi ya vikao wala kupitia mchakato wa uchaguzi! Hivi Profesa Lipumba alipojiuzulu Uenyekiti ,Chama cha CUF si kilikaa na kumpata kaimu Mwenyekiti ambaye yuko mpaka sasa Mhe.Twaha Taslima.Sasa inakuwaje Profesa mzima anafanya siasa "pori " kama hizi!? Zitto Zuberi Kabwe naye ukimsikiliza kwa makini ni kama ana- pre empty mazungumzo yake aliyofanya na viongozi fulani wakubwa ndani ya CCM kuhusu Rais John Magufuli! Kauli kama vile,alienda Rwanda kujifunza namna ya kudhibiti wapinzani na demokrasia (hapa lazima ujue Zitto anamfurahisha nani),si rahisi kuanzisha vita ya kidiplomasia kwa kiongozi makini bila sababu! Kauli yake nyingine ya kitoto ni ile ya eti CCM imdhibiti mwanachama wake na ikishindwa watamdhibiti wao! na ya mwisho ni ile kauli ya Magufuli atakuwa Rais wa term moja! Zitto fanya siasa acha sasa kucheza ngoma za kulipwa!
Mti wenye matunda ndio hupopolewa nawe, La Zitto sikubaliani na wewe ila kwa Prof ni sawa ma mimi linanipa tabu kidogo.
 
Hawaogopwi bali ni watoto wajinga ambao wakiachwa bila mkong'oto hawachelewi hata kunya sebuleni, lazima wadhibitiwe !
Neno dhibiti, ni kupambana na MTU na kumtukiza asifurukute, ila MTU huyo ananguvu sawa na wewe na si mtoto. Hivyo wapinzani wananguvu kama watawala, ndio maana watawala wanaangaika nao. Ingekuwa ni watoto wangeachwa tu.
 
Hakuna anayewaogopa bale wanaelekezwa namna ya kufanya siasa zenye mustakabali mwema kwa Tanzania Mpya tuitakayo.
Siasa wanazofanya akina Zitto na wenzake za kiharakati, zilishapitwa na wakati. Siasa za kuonesha kuwa hawaogopi wala kuheshimu chochote hatuzihitaji kwa sasa kwani tunajenga mwelekeo mpya wa taifa letu.
 
Katika wanasiasa ambao hapa Tanzania sijawahi kuwa trust ni Zitto. Zitto ni mwanasiasa opportunist, ambae yupo tayari kufanya lolote kutetea ugali wake na si maslahi mapana ya Taifa. Zito ni bora atambue kuwa, sisi watanzania tumesoma pattern ya siasa zake, na tumeshajiridhisha pasi na shaka kuwa Siasa zake msingi wake ni tumbo lake mwenyewe na si vinginevyo.

Naomba pia nimfahamishe Zitto kuwa, sisi watanzania, tuna imani kubwa na Raisi wetu, na Morally ZZK hawezi kulinganishwa na Magufuli, kwa positions ambazo alishashika Magufuli, you can imagine angekuwa ni zitto angekuwa ameshapiga deals kiasi gani. Ndugu Musoma, tujiulize mwaswali haya

1. Je, Zitto kabwe, anawaambia CCM wamdhibiti mwanachama wao kwakuwa anadhibiti wapinzani?. Ni kweli msingi wa huu ushauri wake unaweza kumshawishi kiongozi yeyote wa CCM auzingatie?. Unamaanisha nini Muheshimiwa?

2. Je, Mh.Zito, anatuambia kuwa Rais wetu mpendwa atakuwa wa kipindi kimoja kwa sababu anadhibiti Upinzani?. Anatuambia upinzani uliodhibitiwa ndio utakao mtoa ikulu?. Kama upinzani umedhibitiwa utawezaje kumuondoa Rais Madarakani ndani ya term moja, wakati vipindi vyote ambavyo marais hawakwenda Rwanda na kujifunza na mna ya kudhibiti upinzani, na hakukua na Jitiada maksudi za kudhibiti upinzani na upinzani ulishamiri lakini haikutokea Rais akatawala kwa Term moja???. Unamaanisha nini Muheshimiwa?

Zitto, tambua kuwa katika viongozi ambao watavunja record kwa kuchaguliwa na wananchi wengi ni Mh. Magufuli ktk uchaguzi wa mwaka 2020. Magufuli amefanikiwa kuinyang'anya CCM ndani ya mikono ya Wafanya biashara wakubwa waliokuwa wakiinyonya Tanzania kwa gharama ya Maisha ya watanzania masikini waliowengi. Sisi tunamuunga mkono, na tunamkubali sana.

Acha double agency kaka.

Hapo ndipo tutakapotofautiana, JPM ameitoa CCM ipi katika mikono ya wafanyabiashara wakubwa?? Tuache nadharia tuwe realistic hebu nipe ushahidi unaothibitisha CCM haiko kwenye mikono ya wafanyabiashara wakubwa, unafahamu namna ambavyo matajiri hufanya kazi zao ndani ya CCM? kwa taarifa yako matajiri hupandikiza vibaraka wao kwenye CCM na mwisho wasiku huwatumia nasiokuwepo direct.

Binafsi nilimpigia kura JPM nikitegemea atafanya kitu kwa kudeal moja kwa moja na wahusika wakweli wa matatizo ya tanzania yaani kifupi kuvaa mabomu lakini kinyume chake naona anazunguka mbuyu na kuwaandama ambao hawana madhara aka vidagaa, hata ukiangalia kiundani utakuta ni kama ameshasalender kwa hao wafanyabiashara wakubwa maana bado tunaona wanafanya yakwao kila kukicha au wewe huwaoni akina MANJI na Mo dewji wakiendelea kupaa??.

Unalijua swala la wafanyakazi wasio na vibali na ambao hawastahili kufanya Tanzania lilivyo anza kwa mbwembwe tukaamini tatizo linamalizwa au kupunguzwa lakini kila kukicha wahindi,makaburu, nk wanamiminika shamba la bibi.

Kinachoendelea ni kama show off tu kutuaminisha mambo yanaenda huku chini ya carpet mambo yanasonga tu kwa wenyewe,tofauti ya huyu na JK ni huyu kupiga sana kelele na kuongea kwa kutufurahisha na matukio ambayo yanalipuka kwa ajili ya show off lakini mwisho wa siku kama mtu mwenye akili timamu jiulize TATIZO HUSIKA LINAKUWA LIMEISHA NA MSINGI WAKE UPO KWA FUTURE YA TAIFA?
 
Hakuna anayewaogopa bale wanaelekezwa namna ya kufanya siasa zenye mustakabali mwema kwa Tanzania Mpya tuitakayo.
Siasa wanazofanya akina Zitto na wenzake za kiharakati, zilishapitwa na wakati. Siasa za kuonesha kuwa hawaogopi wala kuheshimu chochote hatuzihitaji kwa sasa kwani tunajenga mwelekeo mpya wa taifa letu.

Muelekeo upi mbona mimi sioni kinachoendelea zaidi ya kelele tu? Embu nionyeshe huo muelekeo basi. Kwa kuangalia miezi sita na zaidi tuambiane kipi kimefanyika kwa future ya taifa hili?
 
Umechanganya habari kabisa mpaka kuchangia inakuwa ngumu.Ungechagua suala moja ukalitungia hadithi
 
Muelekeo upi mbona mimi sioni kinachoendelea zaidi ya kelele tu? Embu nionyeshe huo muelekeo basi. Kwa kuangalia miezi sita na zaidi tuambiane kipi kimefanyika kwa future ya taifa hili?
Kama huna macho ya kuona nami sina uwezo kukuonesha kitu ambacho huwezi kukiona.
 
Hapo ndipo tutakapotofautiana, JPM ameitoa CCM ipi katika mikono ya wafanyabiashara wakubwa?? Tuache nadharia tuwe realistic hebu nipe ushahidi unaothibitisha CCM haiko kwenye mikono ya wafanyabiashara wakubwa, unafahamu namna ambavyo matajiri hufanya kazi zao ndani ya CCM? kwa taarifa yako matajiri hupandikiza vibaraka wao kwenye CCM na mwisho wasiku huwatumia nasiokuwepo direct.

Binafsi nilimpigia kura JPM nikitegemea atafanya kitu kwa kudeal moja kwa moja na wahusika wakweli wa matatizo ya tanzania yaani kifupi kuvaa mabomu lakini kinyume chake naona anazunguka mbuyu na kuwaandama ambao hawana madhara aka vidagaa, hata ukiangalia kiundani utakuta ni kama ameshasalender kwa hao wafanyabiashara wakubwa maana bado tunaona wanafanya yakwao kila kukicha au wewe huwaoni akina MANJI na Mo dewji wakiendelea kupaa??.

Unalijua swala la wafanyakazi wasio na vibali na ambao hawastahili kufanya Tanzania lilivyo anza kwa mbwembwe tukaamini tatizo linamalizwa au kupunguzwa lakini kila kukicha wahindi,makaburu, nk wanamiminika shamba la bibi.

Kinachoendelea ni kama show off tu kutuaminisha mambo yanaenda huku chini ya carpet mambo yanasonga tu kwa wenyewe,tofauti ya huyu na JK ni huyu kupiga sana kelele na kuongea kwa kutufurahisha na matukio ambayo yanalipuka kwa ajili ya show off lakini mwisho wa siku kama mtu mwenye akili timamu jiulize TATIZO HUSIKA LINAKUWA LIMEISHA NA MSINGI WAKE UPO KWA FUTURE YA TAIFA?

Ndugu Samurai, inafahamika wazi namna ambavyo wafanyabiashara walijipenyeza ndani ya CCM ili waweze ku influence maamuzi juu ya sera zinazowahusu in their favour. Sikumaanisha kuwa wafanyabiashara walikuwa ndo wanasiasa moja kwa moja. Ndugu tambua mfanya biashara anahangaika ku maximize profit, kuna namna ya kufanya hivyo kwa njia halali, lakini wafanya biashara hawa walikuwa wanafanya hivyo kwa kukwepa kodi na kulindwa na hao mamluki. Tunatambua ni nini magufuli amefanya juu ya hili la ukwepaji wa kodi, na nafikiri hata wewe unatambua kuwa mfanyabiashara anapolazimika kulipa kodi wakati hakuzoea kufanya hivyo, hawezi kufurahi, na kama hajafurahi lazima atajitoa kwenye kufadhili chama kwakuwa kimeshindwa kulinda maslahi yake. Lakini tunatambua kuwa, mfanya biashara akilipa kodi, mwananchi wa kawaida ananufaika namna gani, kama huelewi hili ni pm nikufahamishe. Kufanya huku kuna signify kukiondoa chama chini ya influence za wafanyabiashara kwa interests zao, na kukirudisha kwa wananchi kwa maan ya kua kinasimamia maslahi ya Taifa zima na hasa wananchi wa kawaida.

Ndugu Samurai, nia ya Magufuli, si kuwafanya Matajiri wawe Masikini, hapana. Kwa hiyo hainishangazi kuona kwamba MANJI na Mo dewji wakiendelea kupaa, kwani kuna tatizo gani wao wakiendelea kupaa lakini wakiwa wanalipa kodi yao kihalali??. Wakiendelea kulipa kodi yao kihalali, kupaa kwao ni manufaa kwa taifa, kwakuwa kila wanapoendelea kuwa matajiri, ndivyo kodi wanazolipa zinapoendelea kuwa kubwa. So, binafsi na hata magufuli angependa kuona tunakuwa na watu kama hao wengi, lakini utajiri wao waupate kwa njia halali na walipe kodi.

Samurai, si kwamba Tanzania haitaki kuwa na watu kutoka nje, tunataka watu hao waje wafanye shughuli zao kihalali. Magufuli hakuwahi kuwapiga ban watu kutoka nje kuingia nchini, amesimamia hao watu waje kwa kufuata taratibu. Hakuna tatizo kama wanaingia nchini kwa kufuata taratibu, Japo nina shaka na maana yako unaposema wanamiminika nchini,,,,this is exageration.

Ndugu yangu tambua kuwa tatizo tulilokuwa nalo lilikuwa ni kubwa mno, mabadiliko halisi utayaona baada ya kipindi kifupi. Si sahihi kuona significant changes ndani ya kipindi cha miezi kadhaa.
 
Back
Top Bottom