mtundu27
Member
- Jul 17, 2018
- 78
- 123
Habarini wadau.
Wengine ni wageni humu ila nafurahia kuwa sehemu ya jf maana hakika ni platform inayosaidia kuelimishana na kuhabarishana.
Kuna jambo limekuwa linanitatiza kwa muda katika nchi yetu so nimeona tujaribu kuelimishana kwa hili ntakalochangia.
Katika miaka ya 70 na 80, Tanzania kama nchi nyingi zilizokuwa na mrengo wa kikomunisti, uongozi ulijikita katika udikteta hata kama haukuwa rasmi ila matendo na viashiria vyote vilikuwepo pamoja na kauli mbiu iliyotumika sana kipindi hiko, ya 'zidumu fikra za mwenyekiti'.
Ni miongo kadhaa imepita na tulianza kusogea katika kujijengea mfumo mzuri wenye demokrasia ambao naamini baada ya miaka kadhaa tungekuwa mahala pazuri.
Cha kusikitisha sijui ni uduni wa fikra au ni kukumbatia mshahara, katiba inaminya kwa wazi kabisa katika mambo ya msingi ilhali upendeleo wa wazi kabisa ukienda kwa chama cha kijani kinachosupportiwa na dola ya nchi.
Hivi kweli katika dunia ya sasa wagombea wapite bila kupingwa?
Wanasheria maarufu duniani waliwahi kusema, injustice anywhere is injustice everywhere, na hii hali inashamiri kila kukicha, cha kusikitisha watu wenye maisha duni ndio wanaokumbatia huu ujinga wakishapewa viposho wakapige makofi.
Kigamboni nasikia mkutano wa mbunge umesambaratishwa kwa kile kinachosemekana ni maagizo kutoka juu.
Amani hii naona watu wanaichezea kweli. Kukandamiza wengine ndio wanaona ni haki yao.
Katika vituko vinavyoendelea ni kile cha mwenyekiyi uvccm kuwa na nguvu katika kutekeleza majukumu yake kuliko kiongozi wa upinzani , (KUB).
Inasikitisha kwa kweli.
Watu waliopevuka, wenye maendeleo pamoja na exposure kama rais obama, ameliweka wazi hili, kuwa unawezaje kusema umeshinda kwa 90% huku wengine unawanyima fursa ya kufanya siasa kwa usawa.
Mawazo hayawezi kulingani maana kila mtu ameumbwa tofauti, na kukosoana kwa nia ya kujenga (constructive criticism) ndio msingi sahihi wa kujenga nchi.
Ila mtu hazina anaifanya kama personal bank account, anachota anavyojisikia huku akikamua wananchi kodi kila kona, na hapo hapo wawakilishi wa wananchi wanaotoa hizo kodi nao wakizibwa midomo.
Embu ndugu zangu, tushauriane the way forward maana hakika hili linaumiza.
Tuepuke matusi, tujadiliane kwa misingi bora.