Kwa Miaka minhi Tz tulikua tukifanya Siasa za kistaraabu kwa maana ya vyama vyote luwa huru kufanya Op anuai kwa lengo la kuimarisha vyama vyao, Chaguzi za kistaarabu, Kushindana mwa hoja japo Ccm kwa asili mabavi yalitumika kulinda dola japo kwa asilimia Ndogo.
Awamu ya Tano mambo yakabadirika, Uhasama, Chuki, Mabavu na vitendo vya ukandamizaji kwa vyama shindani vikaongezeka tena kwa nguvu maradufu. Vyama vikanyimwa haki ya kikatiba ya kufanya shughuri zao huku Ccm ikipata haki hiyo. Vinyongo kwa Watz vikawa vikubwa sana na Siasa zikakosa mvuto. Unajua kimsingi uhai wa Chama tawala unaletwa na uhai wa Upinzani madhubuti, Ukikandamiza Upinzani basi na Chama Tawala kinadumaa na kupoteza mvuto.
Ccm ya Samia(Rais) Chongolo na Shaka inarudi katika Misingi ya Awali ya siasa za hoja, Masuala na maendeleo huku vyama shindani vikipewa haki, Uhuru kwa mujibu wa katiba. Tutegemee Utamu kunoga katika siasa zetu.