MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,238
- 50,415
Huwa napata shida sana nikiona Wakenya wanzangu humu wakiponda nchi yetu huku wakidai kwamba tupo nyuma sana kidemokrasia na kwenye mambo mengi. Lakini kwa baadhi yetu ambao tumepata fursa ya kuzitembelea nchi zote majirani kama vile Sudan Kusini, Uganda, Ethiopia, Tanzania, Burundi, Rwanda na Kongo huwa tunawashangaa sana hawa Wakenya wasiokua na shukrani hata kidogo.
Nimeona sehemu kauli za mkuu wa mkoa Dar es Salaam, kwamba kasema ".., Ninao uwezo wa kumfukuza mtu yoyote ndani ya mkoa wangu kwa masaa ninayotaka mimi na asiondoke na chochote zaidi Ya ndala alizovaa." - Paul Makonda, RC, Dar-es-salaam
Tundu Lissu: Makonda hana mamlaka anayojidai nayo ya kuhamisha watu
Sasa nawaza hapa gavana wa Nairobi leo hii akatumia maneno kama hayo, aisei sidhani kama hata anaweza kuvumilia moto unaoweza kumkuta maana atapondwa hadi hata na wafuasi wa chama chake. Kule Bongo hata kuna mbunge yule wa Arusha yupo jela siku nyingi kisa kasema ameota ndoto kumhusu rais, wakati hapa kwetu rais mnampa majina ya kila aina ila yote anaona sawa na kuwachekea tu.
Wakenya ambao hujifanya kichaa na kuponda nchi yetu mfikirie sana, hama nenda uishi hata miezi michache ndani ya hizi nchi majirani uone ukirudi utakua umetia akili. Ilitugharimu sana kufikia hapo tulipo, baadhi yetu nikiwemo tilipgwa mabomu ya machozi na kuumizwa sana kipindi tunapambana kupigania hii demokrasia ambayo tunajivunia leo. Kila Mkenya alihusika kwa namna moja au nyingine.