Siasa za nchini... HAKUNA Kitu!

Siasa za nchini... HAKUNA Kitu!

Magoo

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2011
Posts
448
Reaction score
79
Mimi siyo muumini wa chama chochote cha siasa bali mara zote nimekuwa nikiangalia mgombea mwenye uelekeo wa kiuwajibikaji ila hakuna hata mmoja aliyefikia robo ya matarajio yangu na wapiga kura wenzangu kwake, nimekuwa nikijiuliza tatizo liko wapi na sasa ninaelekea kupata majibu..

1. CDM wanasubiri tukio/janga kuwafumba macho wananchi baada ya hapo hakuna jipya hatuoni positive outcome mfano swala la Mawaziri wizara ya Elimu, Dowans Nk.. please acheni yote safisheni wizara ya elimu, elimu ndo kila kitu taifa la wajinga halina uwezo wa kupambanua mambo harakati za mafanikio hazitafanikiwa kamwe bila wasomi wa kutosha mlianza vyema kuanzia elimu ya chini mpaka juu hakuna kitu..acheni porojo zisizo na msingi simaminieni hawa watu wawajibike.

2. CCM imeshika dola ila hakuna awajibikaye kwa ajili ya wananchi kila mmoja anajineemesha na jeuri hakuna mfano.. leo hii nauli daladala hadi 1o0,000 kwa mwezi hakuna anayejali kima cha chini mshahara 150,000 maisha gani haya??? waalimu mmewapeleka vituo vya kazi no mshahara huu ni unyanyasaji wa hali ya juu... vyuo vikuu vya umma havina wahadhiri no one cares... Tunapumbazwa na mambo ya Rwakatale na Kabanda ili mfunike yale yanayogusa maendeleo ya jamii .


3. Wananchi teteteeeh "wenye nchi" tunawajibika kwa hali duni tuliyonayao tumekuwa watu wa kushabikia vyama kila mmoja akidai chama chake ni bora zaidi ya kingine inanishangaza sana (bila kuangalia kwako wewe ama ndugu yako) njaa uliyonayo, huna maji safi na salama, umeme kwako ni kitendawili, kilimo wafanya kwa mikono, watoto shule imeshindikana ada iko juu, hata aliyesoma ajira hakuna ni tabu tupu kwako

Kwa wananchi ni dhahiri chama tawala kimeshindwa kazi na CDM pia sioni nafuu yao ni wakati wa kuangalie wale wenye nia ya dhati ya kututoa hapa tulipo na tuwasapoti. Tunaitaji kuwapush hawa tulio nao (CDM et al.,) waweze kutetea maslahi yetu na siyo kusifia tu wakati hawakamilishi yale ya muhimu kwa ajili ya wananchi. Kama mtu haendi sawa awe Zitto, Lissu Mbatia ama yoyote tusifumbe macho tupige kelele kwao waamke na kutusimamia ipasavyo kwani nguvu yetu itasikika kupita kwao. Waanze na hili la nauli pamoja na elimu
 
Kama huwa hawakidhi hata robo ya matarajio yako, Unaonaje wewe ukajitokeza kuchukua nafasi za hao wanasiasa?
 
Back
Top Bottom