Siasa za majitaka zimeanza kuchukua kasi CHADEMA baadhi ya viongozi wanaitwa masalia wakati ni viongozi wa juu wa chama this is bad either we fire or w retain naogopa kuna watu wanatumika kudisqualify baadhi ya viongozi kwa kuwaita wasaliti na wengine waonekane wanajengeka chama nyumba moja kugombania fito kwanini.
Ukiwa mtaani hasa maeneo ya mijini ni dadra sana kusikia mtu anaisifia CCM, wapo watu wanapenda CCM iendelee kuwa madarakani ingawa watu hao huwa hawasemi wazi. Unaweza ukawaona kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia Nick names.
Zifuatazo ni sababu zinazofanya baadhi ya Watanzania kulilia CCM ibaki madarakani pamoja na umasikini, ufisadi uliokithiri kufikia hatua ya kushika nafasi ya pili kwa ufisadi Afrika mashariki, point moja tu baada ya uganda.
1. Watu hao kwa sasa wananufaika na mfumo wa sasa, kwani ni mfumo ambao uko loose,kundi hili ni waajiriwa serikalini. Wafanyakazi wa Serikali wamefanikiwa kuvuna pesa za wizi serikalini wanaomba hali iendelee kuwa kama ilivyo, CCM iendelee kutawala .
Wengi wetu tunawafahamu rafiki zetu walioko serikalini bila kujali kuwa wana nafasi za juu au za chini wamefanikiwa kutajirika ghafla, tunawafahamu lakini hakuna mahali pa kuripot kwakuwa system nzima ni Corrupt.
2. Wako wafanyabiashara wanaokwepa kodi, serikali imegubikwa na rushwa kwa hiyo hawawezi kukusanya kodi, kila kitu kinakwenda kwa dili au ten %. Hawa nao wanasema kidumu chama cha mapinduzi
3. Wako ambao wamezaliwa kwenye familia tajiri, wakiamka asubuhi wanajiuliza ama wale soseji au mayai. Friji zao Zimejaa kuku, samaki nk. Pia wanachagua watoke na aina gani ya gari. Kundi hili halifahamu vizuri umasikini uliowagubika watanzania, shida wanazisikia kwenye vyombo vya habari, maisha yao hawajichanganyi na masikini kabisa, wanasoma shule na vyuo vya kitajiri kwa hiyo umasikini hawaujui. Kwa hiyo hawaoni kosa la CCM
4. Masikini lakini wanaipenda CCM mpaka kesho. Kundi hili liko vijijini. Linaipenda CCM kwa sababu ya kukosa elimu ya uraia, au hawapati habari kabisa. Shughuli yao kubwa ni kulinda nyani wasivamie mashamba yao. Kundi hili halijui maana ya maendeleo, wanatamani hata shule zisiwepo ili watoto wachunge ng'ombe na kulima, wakivuna mazao ya kutosha wakala wakashiba hata kama hawana shilingi ya kununua ndala wao usema CCM oyeeeee
5. Kuna kundi ambalo lenyewe limedanganywa kwa uvumi au kwa mazoea tu. Kwamba bila CCM kutakuwa na vita, linasema CCM imenilea hadi hapa nilipo. Kundi ili liko tayari kuchagua hata fisadi au jiwe ilimradi tu atokee CCM. Kundi hili linafahamu kabisa kuwa serikali haifanyi vizuri lakini kwa mazoea lenyewe limeendelea kuomba CCM ibaki madarakani ili amani iendelee kuwepo.
6. Imani. Kundi hili ni mchanganyiko wa wasomi na wasiosoma. Hawa kwa sababu ya imani kali kwa dini limehamua kuweka dini mbele lakini maendeleo baadae. Kundi hili linafahamu kabisa madudu ya CCM lakini limeendelea kuwa na msimamo kwa CCM. Kundi hili udanganywa kirahisi kwa propaganda za CCM kwamba Chama fulani ni cha dini fulani. Bila kujali msitakhabali wa nchi uamua kushabikia CCM lakini baada ya miaka mitano huwa halioni mabadiliko ya kmaendeleo. Kundi hili ndilo linalochelewesha mapinduzi ya nchi, kundi hili ukesha likiomba CCM iweke mtu wa dini yake bila kujali uwezo wa kiongozi husika.
7. Mafisadi papa. Hili ni kundi ambalo ni chafu kabisa, halina hata dini. Limeiba pesa nyingi za Watanzania bila kujali kuwa kila siku kuna masikini wanakufa kwa kukosa dawa mahosipitalini. Kundi hili kwa kutumia nguvu ya pesa za wizi linatamani ligawie kila mtanzani laki moja ili wapigie kura CCM. Kundi hili linahitaji CCM idumu ili lipate security ya mali zake, liko tayari hata kuua au kung'oa mtu kucha anaehatarisha CCM kuanguka. Linahofu kuwa chama kingine kikiingia madarakani litafilisiwa na kupelekwa mahakamani. Ni kundi lenye nguvu kubwa hata sasa ndani ya CCM