Siasa za mahaba zitatumaliza

Mkuu Kiganyi, umegusia siasa za mahaba lakini tatizo wewe umedanganywa ukauvaa mkenge wa siasa za chuki pasipo sababu. Mkuu mi nakuomba ujaribu tena kufuatilia topic zilizohusu hiyo ishu ya rushwa humu ndani ndo utajiridhisha kuwa kilichopo hapo ni tuhuma za kumlazimisha mtu kuwa ana hatia halafu zikawa surported na ushabiki mwingi. huo ushabiki ndo uliwapoteza watu wasiofuatilia mambo kwa undani na kuishia kumzushia huyo mwanasiasa kuwa alihusika kwenye rushwa. kwa jisi suala lilivyo, NAKUAPIA MKUU, PIGA UA HIYO ILIKUWA NI KUCHAFUANA KISIASA. Fuatilia kama nilivyokuomba, utabaini ukweli, ukishindwa nikumbushe nikuweke sawa kwa nia nzuri tu, ili tuwe tunayachuja mambo badala ya kushabikia bila kujua undani wake.
 
Mwandishi ameelezea vizuri sana kwa mtazamo wake,na ukweli utabaki palepale kuwa hao waliokuwa wakitweet naye ni kati ya wanawake ambao usiku na mchana wanaomba wanaume walio karibu nao wafanikiwe ili na wao wapate nafasi za upendeleo,uchaguzi wa UWT umetueleza mengi sana tunasikia tu huyu alikuwa wa KK,baadaye akaenda kwa Londa na sasa yuko kwa cigwiyemisye,na mwingine unasikia bila Spika mstaafu asingekuwa hapo,na hiyo ni mifano tu ya siasa zetu za mahaba.Lakini historia inaeleza wazi kuwa kuna Kaisari wa Roma ya zamani ambaye aliachana na mkewe sababu tu mkewe ametuhumiwa kuwa si mwaminifu.Na alipoulizwa ni kwa nini kamuacha mkewe sababu ya tuhuma akajibu kwa sababu yeye ni mke wa Kaisari hatakiwi kutuhumiwa.Tukirudi kwetu hawa viongozi tulio nao walitakiwa wawe wawazi na wafanye kazi kwa bidii na kuwajibika ili kuondoa uwezekano wa kutuhumiwa.Na kama tuhuma zitajitokeza basi ni vyema kiongozi huyo akajiudhulu ili kupisha uchunguzi dhidi yake na si kusimama kibabe kudai ushahidi..
 
Back
Top Bottom