Siasa za mahaba zitatumaliza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa za mahaba zitatumaliza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiganyi, Aug 10, 2012.

 1. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  KUNA msemo mmoja ninaopenda sana kuutumia kusisitiza hoja katika maongezi, ambao unasema, "Ili uweze kulielewa giza inabidi utoke au uende katika mwanga, na kinyume chake (vice versa)."

  Huwa ninautumia msemo huu kubainisha ‘faida' tuliyonayo baadhi yetu (Watanzania) tulio nje ya nchi yetu. Kwamba, kuwa kwetu huku kwa namna fulani kunatusaidia kuwa kama kile kinachofahamika katika tafiti kuwa ni "participant as an observer," yaani kwa tafsiri isiyo rasmi ‘mshiriki ambaye pia ni kama mwangalizi.'

  Kwa kuwa huku ughaibuni sio tu tunapata fursa ya kulinganisha tofauti ya mambo kati ya hapa na huko nyumbani bali pia tunaweza kuiangalia jamii yetu inayotuhusu lakini tukabaki watazamaji. Hata hivyo, kuna wakati baadhi yetu tulio nje hukumbanana wakati mgumu kuzungumzia mambo ya huko nyumbani, hususan, kutokana na madai kuwa yanayotokea huku hayatugusi moja kwa moja.
  Baadhi ya ‘wapinzani wetu' hudiriki kwenda mbali zaidi na kutulinganisha na Watanzania ‘tusio kamili' kwa maana ya kwamba shida au raha za huku hazitukabili katika namna zinavyowakabili wao.

  Huu ni mtizamo potofu hasa ikizingatiwa kuwa wengi wetu, kama si sote, bado tuna ndugu, jamaa na marafiki huko nyumbani. Kimsingi, kuwa nje ya Tanzania hakumpunguzii mtu Utanzania wake, isipokuwa tu kwa wenzetu wachache ambao kuwa kwao huku kunamaanisha ‘talaka' kati yao na asili yao. Ni katika kuiangalia nchi yetu kwa mtizamo huo wa ‘mshiriki ambaye ni kama mwangalizi' ndipo nimejikuta nikifikia hitimisho kwamba mwenendo wa mambo huko nyumbani una mushkeli.

  Kati ya wiki iliyopita na muda huu ninapoandaa makala hii kumejitokeza matukio kadhaa yanayoweza kuashiria kuwa nchi yetu inakwenda ‘ndivyo sivyo.' Nitatoa mifano machache;

  Habari ambayo imetawala katika vyombo vingi vya habari kwa sasa kuhusu mambo yalivyo huko nyumbani ni hili suala la baadhi ya wabunge kutuhumiwa kupokea rushwa. Habari hiyo inapata uzito mkubwa zaidi pale inapotanabahisha kuwa licha ya baadhi ya wabunge kuandamwa na tuhuma hizo, baadhi ya Kamati za Bunge pia zinatuhumiwa kujihusisha na rushwa, hali iliyopelekea Spika wa Bunge kuamua kuivunja Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.

  Lakini tuhuma hizi za rushwa zimefichua kitu ambacho binafsi ninakiona kama tatizo la msingi katika jamii yetu. Katika siku chache zilizopita, nimekuwa nikitumia muda wangu mwingi katika mtandao wa kijamii wa twitter kuzungumzia tuhuma hizo dhidi ya wabunge, hususan, wale wanaodaiwa kupokea mlungula ili kulifisadi Shirika la Umeme (TANESCO).

  Jumapili iliyopita mmoja wa tunaoweza kuwaita watu maarufu (celebrities) alionekana kuchukizwa na twiti zangu ambazo kimsingi zilikuwa zinaelekezwa kwa mbunge mmoja wa chama cha upinzani ambaye ametangaza dhahiri kuwa ana nia ya kuwa rais wetu huko mbele. Katika mazingira ya kawaida tu, mwanasiasa anayetamka hadharani kuwa anataka kuwa rais ni lazima aangaliwe kwa makini ili wapiga kura wapate fursa nzuri ya kumuelewa.

  Kwa sababu anazozijua yeye binafsi, celebrity huyo wa kike alinivurumishia maneno makali akidai kuwa tuhuma nilizotoa dhidi ya mwanasiasa huyo zina dalili za chuki binafsi, hasa kwa ile haijathibitishwa kuwa mwanasiasa huyo ni fisadi. Lakini kabla sijatulia, mwanamama mwingine msomi na mwenye wadhifa kwenye taasisi moja ya umma naye akanihoji ni mahali gani mwanasiasa huyo ametajwa kuwa ni mwizi. Labda hadi hapa msomaji unaweza kujiuliza kwanini ‘utetezi' dhidi ya mwanasiasa huyo unaonekana kwa jinsia moja tu?

  Huyu mtu wa pili kukerwa natwiti zangu kuhusu mwanasiasa huyo ndiye aliyenigusa zaidi, kwa sababu kimsingi, elimu na madaraka yake yanamweka katika kundi la kijamii linalofahamika kama tabaka la kati. Nilishawahi kuandika katika makala moja huko nyuma kuhusu jinsi tabaka hili la kati linavyoshindwa kuwa kiunganishi cha kupigania maslahi ya tabaka la chini la walalahoi.

  Nilieleza katika makala hiyo kwamba tabaka la kati lingeweza kuwa nguvu muhimu ya kupigania maslahi ya tabaka la chini kutambuliwa, na hatimaye kufanyiwa kazi na tabaka la juu (ambalo hujumuisha tabaka tawala). Nikinukuu maneno ya binti huyo wa pili, alinieleza kuwa "wanamchukia mwanasiasa huyo wajinyonge, kwani njia yake kuelekea Ikulu ipo wazi."

  Niliguswa sana na maneno haya kwa sababu wakati mwanasiasa huyo anaonekana kupata utetezi katika tuhuma zinazomkabili kuhusu kuifisadi TANESCO, sio tu kuna watuhumiwa wengine wasiotetewa bali pia hata huko nyuma baadhi ya wanasiasa waliotuhumiwa kuwa mafisadi hawakuwahi kutetewa kiasi hicho. Japo ninatambua na kuheshimu haki ya kila Mtanzania kumtetea mwanasiasa anayempenda, ukweli ni kwamba licha ya utetezi huo kuwa wa ‘upendeleo' (kile kinachoitwa na Waingereza kuwa ni haki ya upendeleo-selective justice), kwa maana ya kuwa watuhumiwa wengine kwenye kashfa hiyo hawapati utetezi kama ilivyo kwa mwanasiasa huyo, tunapotetea tuhuma za ufisadi kwa vile tu ‘tuna mahaba' na tunaowateta, tunaweza kuwafahamasisha mafisadi wengine waendelee kuitafuna nchi yetu wakijua watatetewa.

  Moja ya mambo yanayokwaza sana maendeleo yetu ni kile ninachokiita ‘siasa za mahaba.' Kwamba mgombea uongozi hapimwi kutokana na sifa na/au uwezo wa kutumikia umma bali kinachoangaliwa ni urafiki, haiba na vitu kama hivyo visivyoweza kuwa vigezo vya uongozi bora.

  Bado ni mapema kutoa hitimisho kuhusu wabunge wanaotuhumiwa kujihusisha na rushwa, hususan hiyo ya kuihujumu TANESCO, ukweli kwamba tuhuma hizo zimewekwa hadharani unaeleza bayana kuwa ufisadi umeingia katika hatua mpya na ya hatari zaidi ambapo baadhi ya watu tuliowakabidhi dhamana ya kutunga sheria (ikiwa ni pamoja na zile za dhidi ya ufisadi) nao ni sehemu ya tatizo la ufisadi.

  Nimebainisha hapo mwanzoni kuwa matukio ya hivi karibuni yanaashiria kwamba hali ya mambo si shwari. Jingine lililonigusa ni suala la mgomo wa walimu ambapo japo kumekuwa na taarifa za kukanganya, kuna dalili kuwa mgomo huo unaendelea. Lakini tukio lililotokea katika shule ya msingi ya Maili Moja, Kibaha, linaweza kutufumbua macho zaidi kuhusu mwenendo wa nchi yetu. Inaelezwa kuwa katika tukio hilo, wanafunzi wenye hasira waliamua kuvurumisha mawe shule yao. Sina hakika kama walifanya hivyo kama ishara ya kupinga mgomo wa walimu wao au kuwaunga mkono, lakini kilicho wazi ni kuwa pindi inapofika mahala wanafunzi wa shule ya msingi wanachukua ‘sheria mkononi' basi ni wazi kuwa Taifa letu limefika mahali pabaya.

  Wanafunzi hawa ndio kizazi cha kesho, ndio mawaziri na wabunge wetu, ndio viongozi wa kesho. Sasa inapofika mahala nao wanaingia katika utamaduni mpya wa ‘vurugu kama ufumbuzi wa matatizo' sijui huko mbele itakuwaje. Majuzi tu tulishuhudia mgomo wa madaktari ambao bado unaelekea kuwa haujaisha kwa utimilifu (taarifa kwenye mtandao mmoja wa jamii inaeleza kuwa baadhi ya madaktari wameonyesha dhamira ya kutaka kurejea tena kwenye mgomo). Kabla hatujasahau kuhusu mgomo huo tunasikia jinsi baadhi ya wabunge wanavyoshiriki kuihujumu TANESCO.

  Wakati huohuo tunashuhudia baadhi ya walimu wakiamua kutimiza azma yao ya siku nyingi ya kugoma. Lakini pengine kubwa na la kutisha zaidi ni taarifa kuwa mmoja wa viongozi maarufu wa dini amekumbwa na kashfa ya shule yake kuiba uniti za umeme wa TANESCO. Haya yote (na mengine ambayo nafasi hairuhusu kuyataja) yanaashiria kuwa hali si shwari huko nyumbani.

  Je, viongozi wetu wanafanya nini kukabiliana na hali hii? Usidhani hiki ni kichekesho lakini siku moja kabla sijaandaa makala hii kulikuwa na taarifa kuwa Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai alionekana anaongea na simu wakati kikao cha Bunge kinaendelea.
  Labda ilikuwa ni simu muhimu kutoka kwa Spika au pengine Rais, lakini taswira ilivyotokana na tukio hilo inaweza kutanabaisha ni jinsi mtizamo wangu kuwa hali ya mambo si shwari huko nyumbani ilivyotofautina baadhi ya viongozi wetu, ambapo hata kwenye majukumu muhimu ya kuogoza Bunge wanamudu kuongea na selula zao.

  Funga kazi ni uamuzi wa Serikali kulifungia jarida la Mwanahalisi kwa muda usiojulikana kwa madai kuwa jarida hilo limekuwa likiandika habari za uchochezi. Katika toleo lililopita jarida hilo kulikuwa na habari kuhusu suala la Dk. Steven Ulimboka na mtumishi wa taasisi nyeti ya serikali alihusishwa nayo. Je, serikali haidhani kuwa uamuzi wake kulifungia jarida hilo unaweza kutafsiriwa kama unalenga kulizuia kuibua ‘makubwa zaidi' kuhusu sakata hiyo?

  Hivi isingewezekana kulifikisha jarida hilo mahakamani ili haki si tu itendeke bali ionekane imetendeka? Na je, uamuzi wa kulifungia unasaidiaje kuzifanya habari zilizoandikwa nalo zionekane ni uchochezi tu.

  Nimalizie kwa kutoa rai ya haja ya mjadala wa kitaifa kuhusu hatma ya Taifa letu. Tunakoelekea si kizuri. Na hili la mjadala si kuhusu tabaka tawala (walio katika bunge, serikali, nk) bali pia kuna haja ya mjadala wa kitaifa kuhusu nafasi ya tabaka la kati katika kuhamasisha, kutetea na hata kupigania maslahi ya tabaka la chini la walalahoi linaloelekea kuachwa bila mtetezi wala msomaji.
  Tanzania ni yetu sote. Tuweke kando siasa za mahaba, tuepuke kutanguliza maslahi binafsi badala ya maslahi ya Taifa, tutatue tofauti zetu (migomo, nk) kwa njia za kidiplomasia, na kubwa zaidi tuungane kwa pamoja kuhangaikia kuipeleka nchi yetu katika mwelekeo sahihi.

  Inawezekana, timiza wajibu wako.
  Raia Mwema - Siasa za mahaba zitatumaliza
   
 2. W

  Wajad JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 20, 2012
  Messages: 1,131
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 180
  Naomba msamaha, nimeshindwa kuchangia bcoz nimesinzia katikati ya mada wakati nikiisoma.
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kiganyi Ngoja nitarudi baadaye kama itaendelea kuwepo kwasababu mods hawachelewi
   
 4. Neiwa

  Neiwa JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 730
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Kiganyi sijui kwa nini ila leo naona nipo na wewe zaidi (lol) usije tu ukaniongeza kwenye list kama dada wa 3 kumtetea jamaa. Hilo aside... Hapo ni wazi wamuogelea Zitto na sitakuwa surprised kama huyo celebrity ni Wema na huyo msomi mtoa elimu kwa higher learnig students wa wa UDSM.

  Hata hivo hapo kwenye blue kidogo papo loose.. hujapakaza vizuri sababu ume diverge wazo ulilotaka kuandika ambalo kwa upande wangu naona lilikuwa na mantiki zaidi na ukaishia kuelezea huyo dada wa pili kwa mapana. Nilipenda sana nisikie huko ughaibuni mkiongea nao response ipo vipi...

  Hata hivo wazo langu katika hilo, hujatenda haki kwa sampuli 2 tu kuamua kuwa anatetewa na iwe conclusive kupata heading yako ya "Siasa za Mahaba".

  You and I know kuna WATU (wanaharakati, Political Critics na Politicians) wakitoa mawazo yao katika ulingo wa siaza it holds water na hali wengine wakiongea (ambao ni majority) huwa tu kama kelele Fulani, kama hizo ulizotaja hapo juu – sio sababu ya dharau; ila tokana na ukweli hio majority mara nyingi sana wapo kimkumbo/emotion/brainwashed zaidi, for huwa hawajuhi hasa wanachoongelea ni nini or kwa nini hasa aongea hivo…
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. I

  IDIOS Member

  #5
  Aug 10, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Duh! Makala nzuri na yenye kufundisha hakika. Najua baadhi ya wachangiaji watabeza makala hii, yauri yao kwa kuwa hawajitambui mchango wao katika kuirekebisha nchi yetu.

  Tanzania siasa za mahaba zipo hakuna wa kubisha katika hili atakaye bisha ctaweza kumuelewa hata kidgo.

  Nitarudi baadaye wakuu.
   
 6. t

  thatha JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mkuu umeongea vizuri, ila makala yako hii ingefaa kama ungeipost kwenye mtandao mwingine wa kijamii tofauti na JF kwa vile hapa, JF ni mahali pa kupotezea muda tu. Ni mtandao wa CHADEMA. sasa usitegemee upost Makala kwenye mtandao unaomilikiwa na chama cha Siasa ukapata michango yenye kujenga badala ya kuponda Serikali, matusi na kashfa.
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  tehe , tehe, tehe. Halima Mdee vs Joshua Nassari, SLAA vs Mshumbuzi, Chiku Abwao vs MB, n.k. Hii makala bwana imesimama.
   
 8. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  ameandika ***** wa kutosha kuwasha wajinga wenzie
   
 9. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,636
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kiganyi naona semina elekezi ya Thatched house imekuingia vizuri sana, kwani tatizo la Mh Zitto kutangaza nia yake ya kugombea urais 2015 ni nini?Hapa sio tu siasa za mahaba pekee bali hata udini,ukabila,majitaka na ukanda haunna nafasi katika jamii yetu ya Tanzania tunayoitaka.Suala la uhuru wa mtu binafsi ama kikundi kutoa maoni ni haki ya kila mwanachama,shabiki na mtanzania mwenye upeo,mawazo na fikra huru. Ninashauri wengine wenye uwezo wajitokeze ili wigo wa kumpata mgombea bora kwa 2015 uongezeke.
   
 10. maria pia

  maria pia JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 516
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hebu nionyeshe japo vigezo viwili vinavyoonyesha kuwa huu mtandao ni wa cdm ilihali hum yanaongelewa mambo mbalimbali?
   
 11. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Naunga mkono hoja.
   
 12. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,105
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  watz wenyewe wa kujadili mustakabali wa taifa wapi? Hawa unaoamka asubuhu unawakuta kwenye vibanda vya magazeti wanaangalia ijumaa,kiu, uwazi? Wanapenda sana kusikia sijui wema kukutwa uchi,., nani kapigwa mtungo!! Hii nchi ni ya ajabu sana! Madaktari wenyewe walikuwa wanakataa kuzungumzia sasa nadhani sasa wamejifunza kwamba siasa ndo mkwamishaji wa fani zao. Ukitaka kufanya watu wajadili mustakabali wa taifa huna budi kuwafanya wajue haki na wajibu wao kwanza.
   
 13. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Mike Mushi ni jina la kichaga.
   
 14. maria pia

  maria pia JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 516
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  u have a point,ila itafahamika tu!
   
 15. maria pia

  maria pia JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 516
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Na wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri!
   
 16. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,640
  Likes Received: 16,593
  Trophy Points: 280
  Tukiwa na Uchung na Nchi yetu basi mambo ya chama yatawekwa kando.Tunashindwa kuwaondoa viongozi wa bovu sababu hatuna mshikamano kama taifa.Tunahitaji Upinzani kwa kila hali ili tuweze kusaidiana katika uongozi wa nchi yetu.Kila mmoja wetu ni kiongozi katika nafasi yake.
  Mie ninaimani sana katika vijana walio na wanaomaliza vyuo vikuu leo,baada ya kuona shida ziliwakumba wakati wakiwa vyuoni basi huwa ninawaza wanauelewa na uchungu wa kubadilisha mambo huku duniani.
  Lakini mbaya zaidi ni pale huyu kijana msomi akipata nafasi ya kazi basi ni wakati wake wa kula na kufanya ufisadi wote anaouona ofisi ile ya serikali.
  NIngewasihi sana vijana utajiri utakuja kwa kufanya kazi kwa nguvu na kumwogopa mungu.Kiongozi anayetakiwa na Tanzania yetu ni yule tu atakayemuogopa Mungu aliyemuumba kuliko chochote kile,zaidi ya hapo hakuna kitu.
   
 17. i

  ishisabita Member

  #17
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inashangaza...am so baffled with two issues, firstly this article was written in weekly newspaper(raia mwema) by one Tanzanian currently living in Scotland...i think it was published last month....the one who brought it here(even if He is the one who wrote before) should have acknowledged the source of this article.

  secondly it looks some of us here in this forum dont like to read newspapers.


  all in all,sexual loyalty is deeply entrenched and exercised by majority of politicians who dont carry genuine missions in serving our community.
   
 18. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #18
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  kwenye makala hiyo chadema inahusikaje? kama unapoteza muda mbona kila mara naona comment zako humu? au na wewe hauko serious? Come on stop nonsense JF ni kisima cha maarifa kwa taarifa yako waulize wenzio
   
 19. Kulikoni Ughaibuni

  Kulikoni Ughaibuni JF-Expert Member

  #19
  Aug 10, 2012
  Joined: Dec 12, 2007
  Messages: 235
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Asante kwa ku-repost,ila nadhani ingekuwa vyema ungebainisha kuwa makala husika imenukuliwa kutoka Jarida la Raia Mwema kama ilivyo hapa Raia Mwema - Siasa za mahaba zitatumaliza

  Again,asante kwa ku-repost
   
 20. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #20
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Kiganyi, uwe unarudi Bongo mara kwa mara na utashangaa sana mambo hapa.
  Uliyoyaaandika yameshapitwa na wakati kwa hivi sasa, na huyo mwanasiasa kijana ameshajitetea mwenyewe.

  Bongo tambarare bwana ila kunaligi isiyoisha kati ya vyama vikuu vya kisiasa, asiyeujua mchezo anaishia kamsitu kadogo nje ya DSM kanaitwa Mabwe Pande.

  Bongo poa sana, mafisadi huku hawashitakiwi, na wale wadhaniwao kuwa mafisadi wanatetewa na Marais, nchi nzuri sana hii muwe mnarudi rudi kuona maedneleo ya foleni zetu.
  Kuna kila aina ya gari likipita kwa mwendo wa pole , kuanzia Vogue hadi Ferrari-mikokoteni, bBajaji na Guta ndo usiseme, zimeruhusiwa kupita katikati ya barabara na hazimpishi mtu isipokuwa msafara wa Rais.

  Bongo tambarare njooni tu.
   
Loading...