Yericko Nyerere
Platinum Member
- Dec 22, 2010
- 17,027
- 20,519
Leo naomba nichambue siasa za Kimataifa, nitaangazia hali ya mambo ya siasa Marekani na Ufaransa ambako michakato ya kisiasa inaendelea muda huu kwa vuguvugu kubwa katika ya vyama tawala na vyama pinzani, Ni ajibu wa wanasiasa wetu hasa sisi vijana tunaolitazama taifa letu kama waambata wa kesho ni lazima tuzijue siasa za ulimwengo na mirengo yake.
Kabla sijaeleza na kuanza uchambuzi wangu, naomba nirejee nyuma ili tusivurugane katika tafakuri hii, nafafanua kidogo kwa wale wenzangu ambao kwenye vita ya Urusi vs Ukraine walijicontradict na kujikuta wamechukua upande kwa msingi wa kisiasa, kiitikadi na kiharakati na kisha wakanishangaa mimi nikiwa katika mtazamo tofauti nao.
Hapo nyuma wakati naweka msimamo wangu niliwahi kuwafafanulia kwamba kuna utofauti ambayo ni nyembamba kiasi kwamba watu wenye macho ya tatu tu ndio wanaweza kuuelewa kwamba migogoro ya kimataifa msingi wake ni Nchi vs Nchi = Maslahi. Hapa ili uchambue unalazimishwa sio kujitakia, bali unalazimishwa kwamba lazima usimama kwenye maslahi ya nchi moja katika ya zinazosuguana. Huwezi kuchambua kwa kuangalia vyama, itikadi, harakati au vyovyote vile, isipokuwa ni maslahi ya nchi tu yaani "National Interest".
Na hapa kwenye National interest, kuna kitu cha muhimu cha ndani kabisa kinachoitwa "security". Unapofika hapo huwa hatuangalii siasa, miiko, au maadili ya kimataifa (kimajumui). Hapa ni key codes tu za National interest. ZINGATIA haya ni kwa nchi Huru TATU tu duniani ambazo ni USA + NATO, CHINA na URUSI. Nchi nyingine zimeandikwa tu kwenye Charter 4 ya Umoja wa Mataifa kuwa ni ni nchi huru lakini hazijawa huru na hazitakuwa huru, hazipo kwenye kundi hili japo upende au usipende.
Migogoro ya kisiasa kimataifa, Siasa za Kimataifa. Hapa maranyingi tunachambua mambo kwakuzingatia kwamba Siasa vs Siasa ambapo jibu huwa Itikadi, harakati nk. Huku ndio unaweza ukachambua jambo lolote kwakuwianisha na misimamo ya kiitikadi, ya kisera, na kiharakati, kihaki na mambo kadhaa wa kadha. Hivyo ndio kusema watu wengi Vita ya Urusi na Ukraine wameamua kuchukua upande kwa msingi huu wa kisiasa. Kwangu naona wamepotoka pakubwa. Na hawatapata msimamo stahiki wa kimataifa katika kuyaangaza mambo haya. Wamekosea sana sana.
Tukubaliane kuwa wako sahihi, tuwarejeshe ndani ya Urusi na Ukraine wanafahamu ideologies ya siasa za mataifa hayo kabla hawajachukua upande? Fikiria Sera za kisiasa za Urusi na Ukraine ni za aina moja na tangu Ukraine ijitenge na Umoja wa Kisoviet bado iliendelea kuwa katika siasa za msingi wa Vladimir Ilʹich Lenin, Tofauti ndogo ambayo Bunge la Duma linahodhiwa na Chama tawala huku cha United Russia chini ya Putin na huku vyama vya upinzani vikiwa viti vichache vyenye nguvu ndogo ya kimaamuzi katika Bunge lenye wabunge 450.
Mtiririko wa idadi ya viti Ndani ya Duma uko hivi; United Russia 325 (Putin), Communist party (125), SZZP (57), LDPR (23), Civic platform (1), New party (15), Rodina (1), Party of Growth (1) na Independent (1)
Huku maamuzi ya baraza la Usalama huwa na nguvu kubwa katika siasa za Moscow, Marais wote wa Ukraine waliopita na hata aina ya siasa zilikuwa za Moscow. Ni hivi majuzi tu Zelensk ndie alianza kujaribu kuhamisha siasa na utawala kwenda Magharibi. Kwamaoni yangu kulinganisha vita vya Ukraine vs Urusi na Siasa za CCM na Chadema ni makosa makubwa hasa tukikubaliana dhana ya kwanza juu kwamba National vs National = Interest, na Political vs Political = Ideology.
Twende katika makala ya leo, nchini marekani Kuna mapambano ya hoja za vyama vikuu Demokractic chama kilicho madarakani, na Republican chama cha Rais wa zamani Donald Trump, Republican sasa hivi wanahoja kuu tatu ambazo zinagonga vichwa vya siasa duniani. Kwanza wanayo hoja ya kashfa ya Hunter Biden mtoto wa Rais Biden kufuatia mtoto huyo kufadhili miradi ya Maabara ya silaha za maangamizi za kibaolojia huko Ukraine na madili mengine machafu huko China.
Republican wanaamini sehemu ya chanzo cha vita ni miradi hii michafu ya nyuklia Ukraine ambayo haikuwa approved na mamlaka za Usalama za Marekani, Inaonekana lilikuwa dili la Biden pekee, Republican wanahoji kulikuwa na motives gani juu ya miradi hii? Jibu la Biden ni kwamba yeye hajawahi kuzungumza na mwanae kuhusu miradi hiyo, Republican waneenda mbele na sasa wanao ushahidi wa mawasiliano ya Biden na Mwanae kuhusu hizi dili chafu.
Hoja ya pili ya Republican ni sera ya Mipakani ambapo wao Republican wanaamini Biden amekuja kuvunja sera ya Trump ambayo ilifanikiwa kuzuia Wahamiaji haramu na njia kuu za mihadarati, Republican wameingia field wanazo data sahihi za kiwango cha wingi wa wahamiaji na idadi ya madawa ya kulevya yanayoingia nchini mwao, Na katika takwimu wanasema hadi Biden amalize muhula wake basi 20% ya Wamarekani watakuwa ni wahamiaji haramu. Sasa zinapigwa kampeni za kuandaa mswada wa kutokuwa na imani na Biden (Impeachment). Hii hoja hadi sasa Biden hajajibu
Hoja ya Tatu inahusu mfumko wa Bei nchini Marekani, Republican wanasema vikwazo dhidi ya Urusi havikuzingatia utafiti wa matokeo hasi (consequences) za vikwazo husika. Pili wanasema serikali haijawajibika kurekebisha uchumi baada ya janga la Corona kama ilivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi uliomuondoa Donald Trump, hoja hizi hadi sasa Biden hajajibu.
Kwahiyo utaona katika hoja kuu tatu muhimu kwa siasa za Marekani, Biden amejibu hoja moja tu nayo majibu hayajakidhi hoja ya msingi.
Upande wa Demokractic wamekomaa na kesi ya Trump ya kutuhumiwa kuhamasisha maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi uliomweka madarakani Biden 20 January 2021, kesi imezidi kukomaliwa vilivyo baada ya juzi Trump kutangaza kuwa ataingia ulingoni katika uchaguzi ujayo. Matokeo ya kesi hii ikiwa itathidibitika kuwa Trump alihusika kuchochea maandamano yaliyopelekea kuvamiwa kwa Bunge na kuharibiwa jengo na samani zake, Basi moja kwa moja itamuondolea sifa ya kugombea Urais na hivyo Republican watalazimika kutafuta mtu mwingine.
Vyama vyote vina vyombo vyao vya habari vya Propaganda vinavyopambana kwelikweli, Upande wa Demokractic wanachombo chao kiitwacho MSNBC, Hiki kinatema propaganda za ulimwengu mwingine kabisa, kwanza ni cha kimataifa hivyo matangazo yake yanasilizwa ulimwengu wote, Kinampiga Trump kwa hoja nzito na ngumu kwelikweli kuliko tunavyofikiri na kudhani sisi wa dunia ya tatu.
Upande wa Republican wao wabaungwa mkono na Chombo cha Propaganda kiitwacho FoxNews, Hiki ni chombo cha Kimataifa, chenyewe katika kinapinga kwa nguvu zote sera za Republican za nje ikiwemo vita vya Ukraine na Urusi chenyewe kiko na msimamo tofauti kabisa, Kinapinga sera za Uhamiaji, sera Uchumi na sera ya Ulinzi na Usalama. Na kila sera unapingwa kwa hoja na haijibiwi kwa risasi wala jela wala polisi. Inatakiwa ijibiwe na Biden mwenyewe sio vinginevyo.
Vyama vya siasa Tanzania vina la kujifunza hapa. Tunataka hoja za upinzani zijibiwe. Mfano Juzi Katibu Mkuu wa Chadema Mh John Mnyika ametaka Rais Samia (Serikali) atoe majibu ya kwanini mfumko wa bei nchini ns hatua gani muhimu za kiinchi zinachukuliwa, badala ya kauli ya Makamu Mwenyekiti CCM Bara Mzee Kinana kutaka Mawaziri wakatoe majibu kwake kwanini mfumko wa bei na hatua zipi zinachukuliwa. Nafikiri sasa Chadema inaweza kuja hadharani na Utafiti makini wa kiuchumi na kutoa maoni ya mwelekeo mpya wa kutatua janga hili la mfumko wa bei, Serikali itakuwa na machaguo kukubali ushauri au kukataa lakini Umma utafuata kwenye ukweli utakaotolewa na Chadema.
Kuhusu Siasa za Ufaransa Macron vs Le Pen zinaweza kuamuliwa kwa matokeo ya vikwazo vya Ulaya dhidi ya Urusi, Agenda kuu ni mfumko wa bei na ukosefu wa mafuta na gesi kulikotokana na vikwazo kwa Urusi. Hadi sasa duru ya kwanza tunaona yakuwa Macron ana 27.84% sawa na kura 9,784,985. na Marine Le Pen ana 23.15% sawa na kura 8,135,456. Sasa mchuano wa wawili utaamua nani atashika kiti cha nchi hiyo. Marine Le Pen anaungwa mkono na Kremlin na misimamo yake inaonekana ya wastani, anaamini katika meza ya majadiliano zaidi katika kutanzua migogoro, Huku Macron anaungwa mkono na Washington, Wafaransa wengi wanamini Macron na chama chake cha La République En Marche (LREM) wameidunisha Ufaransa ile ya akina François Mitterrand, Jacques Chirac na Nicolas Sarkozy. Wanaamini Ufaransa imepoteza ushawishi wake kwa sehemu kubwa Duniani na kubaki maeneo yale ya Franco-phone tu. Na sasa inaonekana kunaonekana kuna tumaini jipya kwa Mwanamama Marine Le Pen na chama chake cha National Rall (NR).
Tuna la kujifunza? Ndio lipo tena kubwa!
Kujua zaidi soma Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, na pia soma vitabu vya MTU, Madaraka na Strategy kupitia @yerickonyerereapp kwa 5,000 tu kwa wiki. Nenda Play Store pakua sasa jisajili lipia wiki, mwezi au mwaka ujisomee vitabu vyote Link 👉👉👉Yericko Nyerere App - Apps on Google Play
Contact 0715865544
Na Yericko Nyerere.