Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 375,677
- 870,373
Mahusiano ya nchi na nchi, urafiki ama uadui, ushirikiano katika maswala ya ulinzi sayansi teknolojia hata kijamii na biashara hutegemea sana mtazamo wa kiongozi wa juu
Marafiki na maadui wa kipindi fulani cha uongozi hawawezi kuwa marafiki au maadui wa kipindi kingine... Kila mmoja ana mitazamo yake na vipaumbele vyake ....
Awamu hii ya uongozi imeunganisha kitu kilichoshindikana hapo mwanzo.... Hiki si kingine bali ni usafiri wa moja kwa moja kwa njia ya barabara toka Tanzania Dar es salaam mpaka Kigali Rwanda
Tunaweza kuliangalia hili kwa macho ya juu juu kwakuwa tu kulikuwa na usafiri wa anga kati ya nchi hizi mbili....lakini hili ni la kimataifa zaidi
Kiuhalisia kuna mahusiano mapya kati ya Rwanda na Tanzania tofauti na hapo nyuma, na hata marais hawa wawili waneshatembeleana na kusaini mikataba kadha mikubwa na midogo ukiwemo wa ujenzi wa reli ya kisasa kati ya nchi hizi mbili
Urafiki wetu pia umeimarika na bwana Museveni wa Uganda na bwana Edogan wa Uturuki.... Ni jambo jema lakini tusisahau Kuwa ndege wafananao huruka pamoja