Siasa za chuki zatikisa Kahama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa za chuki zatikisa Kahama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 18, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=3][/h]

  Na Patrick Mabula, Kahama

  OFISI ya serikali Kata ya Malunga Wilayani Kahama imenusurika kuungua baada ya kuchomwa moto usiku wa manane na watu wasiojulika kutokana na tofauti za kisiasa za viongozi
  wa CCM ndani ya kata hiyo.

  Ofisi hiyo ilimwagiwa mafuta taa na kuchomwa moto usiku wa manane siku ya
  Jumapili kabala ya watu wanaoishi karibu na eneo hilo kuona moto ukianza kuwaka sehemu ya mlango wa mtendaji wa kata hiyo na kupiga kelele.

  Mtendai wa Kata ya Malunga Bi.Sesilia Clement, alisema jana kuwa wachomaji hao kwanza walikusanya karatasi za plastiki na kuziweka katika mlango wa ofisi yake kisha wakamwaga mafuta ya taa na kuzichoma moto lakini wananchi waliwahi na kuuzima.

  Wakisumulia tukio hilo baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo walisema hatua hiyo ilisabishwa na tofauti za kisiasa.

  Bw.Williamu Masalu, alisema tangu uchaguzi umalizike mwaka jana katika kata hiyo kumekuwepo tofauti za kisiasa zinazosababisha matukio ya aina hiyo baada ya Chama Cha Wananchi (CUF) kuibuka na ushindi katika kata hiyo dhidi ya CCM.
   
Loading...